Ndachuwa
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 6,269
- 4,559
Ni week end ya pekee kwa kinamama wa Tanzania baada ya Mh. Anna Makinda kuchaguliwa kuongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza. Ni week end ambayo haitakaa ifutike katika historia ya Tanzania kwani hapatakuwepo mama mwingine zaidi ya Mh. Anna Makinda kuwa mwanamama wa kwanza kushika wadhifa wa spika. Ni mategemeo yangu kuwa kunzia mtoko wa leo (Ijumaa) jioni mpaka Jumapili kwa furaha mliyonayo kinamama wallet za waume zenu hazitafunguliwa muwapo kwenye sehemu za starehe. Onyesheni uwezo wenu kwa kutulisha na kutunywesha angalau week end hii tu kudhihirisha furaha mliyonayo baada ya mwenzenu kuukwaa uspika.
Mimi namtakia Mh. Anna Makinda afya njema aweze kuliongoza Bunge letu lifanye vizuri kazi yake ya kusimamia serikali kwa miaka mitano ijayo
Mimi namtakia Mh. Anna Makinda afya njema aweze kuliongoza Bunge letu lifanye vizuri kazi yake ya kusimamia serikali kwa miaka mitano ijayo