Wee....Rudisha Nyara za Serikali!

Atanaye

Senior Member
Oct 31, 2007
153
8
Raia wa Kongo anaswa Dar na nyara za Serikali

2008-01-25 18:33:26
Na Emmanueli Lengwa, Temeke

Mtu mmoja mwenye asili ya Kikongo, aliyetajwa kwa jina la Andason Kasongo, 46, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kukutwa na nyara mbalimbali za Serikali.

Kamanda wa Mkoa Kipolisi Temeke, Emmanueli Kandihabi amesema Mkongo huyo alikamatwa jana mishale ya saa 3:00 asubuhi katika eneo la Tandika, Jijini.

Kamanda Kandihabi amezitaja nyara hizo za Serikali alizokamatwa nazo mtuhumiwa kuwa ni ngozi moja ya chui, ngozi ya fisi pamoja na mkia mmoja wa nyumbu.

Kwa mujibu wa Kamanda Kandihabi, mtu huyo alipohojiwa hakuweza kueleza alikozipata nyara hizo.

Aemsema polisi bado wanaendelea kumshikilia Mkongo huyo kwa mahojiano zaidi na kuwa wanatarajia kumfikisha mahakamani Jumatatu.

SOURCE: Alasiri

Kamanda Kandihabi amezitaja nyara hizo za Serikali alizokamatwa nazo mtuhumiwa kuwa ni ngozi moja ya chui, ngozi ya fisi pamoja na mkia mmoja wa nyumbu.

Hivi hizi nyara Serikali wanafanyia nini? Madogoli! Siri sasa zinafichuka.

Kwa mujibu wa Kamanda Kandihabi, mtu huyo alipohojiwa hakuweza kueleza alikozipata nyara hizo.

Sijui mie nicheke? ttt...Jamaa inavyooneka ni mshirikina, tehehehe
Nakuomba wewe mkongo uturudishie Nyara zetu za Serikali!:mad:
 
Back
Top Bottom