Mpo wanaJF.
Leo nina kero kubwa sana kutoka kwa mama mchungaji yule.
Tuna kikundi cha wanawake mtaani kwetu cha kusaidiana katika mazuri na mabaya na pia tunakopeshana japo hatuna kibali rasmi kutoka kwenye mamlaka za serikali zinazoruhusu kukopeshana.
Mama mchungaji huyu ni mwanachama mwenzetu. Anachokera huyu dada yaani analazimisha members wote tumumchukulie kama "mama mchunguji" wanavyomchukulia kule kanisani kwake SDA.
Mama mchungaji hatoi michango yake ya ada ya michango mingine ya lazima kwa wakati, akikumbushwa anaanza kufoka na kutushangaa kuwa yaani hatuoni aibu kumdai tumeshindwa nini kumlipia hadi asomeke ana deni!!! (sijui nani amlipie kwa usawa huu wa JPM).
Mama mchungaji sie wengine tukiwa na sherehe siku za Jumamosi kwa imani yake hawezi kuhudhuria lakini yeye akiwa na sherehe yake siku ya Jumapili wanachama wanaposhindwa kuhudhuria kwa kubanwa na shughuli za kanisani ananuna na kutishia kusitisha uanachama kwa madai kwamba watu hawapendani na hawashirikiani kwa dhati wameshindwa kwenda kwake siku ya Jumapili na hali ni siku ya mapumziko!
Mama mchungaji akiomba mkopo kama akiambiwa asubiri pesa ziko kwenye mikono ya wanachama wengine hawajarejesha bado, anasema, "hivi mmeshindwa kunitafutia kwa namna yoyote ile hiyo pesa ninayoitaka nikamalize shida yangu".
Pale kwenye kikundi tuna wanachama ambao wana abudu pamoja na mama mchungaji, wakiona ana mapengo kwenye ada yake wakimlipia siku wakimdai, anawashangaa utasikia kwa mfano "hata wewe Miss Natafuta unadiriki kunidai?!!
Nyie wa mama mchungaji na wa mama askofu, jirekebisheni kama mmeamua kuingia kwenye hivi vikundi vyetu vya "kimataifa" basi mhakikishe mko tayari kutimiza na kufuata sheria, kanuni, sera, taratibu na masharti yote ya kikundi husika, kama hamuwezi undeni vikundi vyenu msitukere sie.
Mbaya zaidi tukimaliza vikao akiona sie wengine tunaagiza "kahenken" ana maindi.