WEE BINTI JIFUNZE MAJUKUMU ANZA NA VITU VIDOGO VIDOGO VILIVYONDANI YA UWEZO WAKO!

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,464
Kama ambavyo mtoto mdogo huanza kujifunza kutembea kwakutambaa anza kujifunza kujitegemea kwa kufanya vitu vidogo lakini vya muhimu katika familia. Inawezekana umeolewa, hujaolewa bado unaishi kwenu au umepangisha lakini hujachukua majukumu ya kujitegenea.

Lakini inawezekana hivyo vitu tayari kuna mtu mwingine anavifanya, hiyo isikupe moyo na kuamua kumiuachia. Lipia bili za maji mwenyewe, bili za umeme mwenyewe, nunua chakula na hapa simaanishi kuleta matunda na nyama hapana!

Namaanisha chakula, kama mchele wa kutumia mwezi nyumbani, unga na vitu kama hivyo. Hii itakupa picha majukumu yakoje, itakupa picha ni kitu gani kinahitajika ili muishi. Kama unaishi nyumba ya kupanga basi changia kulipia kodi na kama mnasomesha basi lipia ada za watoto au wadogo zako.

Unaweza kuniuliza, vipi kama kipato chako ni kidogo sana au kama hufanyi kazi kabisa kwa wale walioolewa ni mama wa nyumbani. Ni kuambie kitu unaweza kujifunza kujitegemea hata kama hufanyi kazi na kuingiza chochote au unaingiza kidogo.

Tatizo kubwa ni kwamba wanawake wengi huwaachia watu wengine kufanya kila kitu, na wakati mwingine hata hawajui kitu husika kinafanyikaje. Mfano mnasomesha lakini hujui hata ada inalipwaje, mtoto akija ni kwa Baba yake anampa hela wanamalizana.

Vitu vikiisha ni kumuambia Baba anatoa hela vinanunuliwa, bili ya umeme hujui inalipiwa wapi, mwenye nyumba hujui analipwa kodi saa ngapi. Kwa maana kua mume akiondoka wewe unakua mgeni kabisa unaanza kujfunza hivyo vitu upya, hujui hata uanzie wapi?

Kwa maana hiyo basi hembu anza kujua hivyo vitu, mnajenga hembu simamia, jua bei ya tofali na patanisha bei hata kama hulipi wewe, watoto wanaenda shule chukua fomu, jua ada na chukua pesa kalipe wewe, bili za umeme zimekuja kalipe wewe, maji na kodi ya nyumba lipa wewe na ongea na Baba mwenye nyumba wewe.

Hapa inawezekana hutoi pesa lakini unafanya hivyo vitu wewe, hii itakufanya kuwa mwanamke, kuacha kuwa yule mtu anasema muambieni Baba yenu kwani Baba asipokuepo watamuambia nani. Kama unapata kidogo basi changia kwa hicho kidogo.
 
Back
Top Bottom