Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,218
Unakuta websites hasa zinazohusika na mambo ya kielimu au matokeo ambazo wengi wanazitegemea mfano ya TCU kila siku ukifungua ipo vilevile labda baada ya wiki au siku kadhaa ndio utakuta kitu kipya..ni wataalam hamna au? Webs nyingine za vyuo mbalimbali na taasisi za kielimu zinazembea hivi hawajui inatukera sana? Nawashauri wajitahidi kupost vitu vipya na habari mpya daily ili kuvutia wasomaji. Webs nyingine zinafunguliwa na watu wengi kipindi cha matokeo tu au kipindi cha ujazaji wa forms tu, hapo hawajui kuweka adds kwa kuweka wasomaji wengi. Kwa mtazamo wangu mimi bora hata web ya bodi ya mkopo wanajitahidi kuweka matokeo yao easy kufungua no need ya kudownload unasoma online hata kwa mobile. Mf leo wameweka kipya, na hata jana wame-update. Jamani hizi webs tuziweke katika hali ya kimataifa sio kuweka tu web ilimradi uwe nayo kama wengine, cha msingi wa-update kila siku na kuweka vionjo vizuri ili tuwe na mazoea ya kuzifungua. Natumaini wameipata.
(N.B-Kama kuna website ya TZ unayoisifia/usiyoisifia list it)
(N.B-Kama kuna website ya TZ unayoisifia/usiyoisifia list it)