Website ya CHADEMA na Application ni muhimu sana

Zanaco

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
1,621
1,581
Habari wadau,

Nimetafuta website na app ya CHADEMAkwenye Play Store sijapata; kama kuna mtu anayo anitumie link niipitie kuna kila sabu ya Lissu kutumia website na app kuwafikia watu wengi ndani na nje.

1. Website kwajili ya Live Stream

2. Michango ya Kampeni yote kupitia kwenye website

3. Weka gateways zote kuanzia Tigo Pesa, Master cord, Visa Card, America Express, Bitcoin

4. Wanachama wote tutajisajili na kulipa michango kila mwezi kila inapotakiwa

5. Wenye card za kupiga kura tuta-register naku login kwakutumia card zetu

6. Idadi ya wapiga kura wa Lissu inaweza kujulika kupitia kwenye website na app mapema

7. Lissu ataweza kujua wangombea ngazi tofauti kupitia kwenye website nakuwasiliana nao moja kwa moja

8. Malalamiko

9. Taarifa mbalimbali zitatumwa kupitia kwenye website

Na mengine mengi kupitia kwenye website mpya ya kisasa yenye kuwa secured na hackers wa mtandaoni ili kila kitu kiende kidigitali.
 
Kitengo cha mawasiliona kama kunashida njoo hapa janvini tuwapige msasa Mh Lisu akiwa ikungi alisema tujipange sio lelemama kuwaondoa wezi wa kura inatakiwa kuwazidi kete kiteknologia
 
Website ni lazima kitengo cha habari ni lazima watupe ufafanuzu kwani Chadema haina website hili nijambo la kushangaza sana tunataka Lisu ashindeka uchaguzi huu
 
Idara ya habari chadema haipo active sana
Ikiwashinda kutengeneza watuachie sisi wapenzi wa Lisu tutaitengeza bure naitakua na kila kitu Lisu ni Raisi wetu wote wasiona na vyama ccm na wana Chadema. Msije mkatuTengenezea website za local kama za Serikali tunataka website za kisasa kalii inaendana na wakati.
 
Bavicha pia nawashangaa sana kwakubweteka mnashindwa kututengezea website ya kisasa mnagoja Tundu Lisu atengeneze .
1.Lipia domain (www.chadema.tz au .com) kwa mwaka 30,000 Tsh
2.Hosting kwa mwaka (130,000Tsh au pungufu inategemea na kampuni )
3.Kisha chagua WordPress ni bure, utapata plugins kibao za bure na kulipia tengeza gate ways tuchange hela ya kampeni mapema iko secure sio site ya local
4.Tengeneza App kali tu download kwenye simu zetu
 
Ikiwashinda kutengeneza watuachie sisi wapenzi wa Lisu tutaitengeza bure naitakua na kila kitu Lisu ni Raisi wetu wote wasiona na vyama ccm na wana Chadema. Msije mkatuTengenezea website za local kama ze Serikali tuna website za kisasa kalii inaendana na wakati.
Kabisa
 
Mkisha host website kua makini sana akikisha mnatumia developers waku hire online kwanfano Freelancer Envato au Upwork waambie tunataka website ya WordPress kisha wape maelekezo mnataka kuwe na nini ndani ya website kisha wape access ya Control Panel wapige spana msitafute developers wa bei rahisi tafuta bei kubwa kuna wamerekani wahindi waingereza wanapiga spana hatari.
 
Asente mkuu nimepata iko vizuri sana kuna mambo machache sana yaku boresha.
1.Inatakiwa kua secured
2. Mkiweza kutoa neno (or) kwenye doamin itakua vizuri zaidi itaoneka bila shida
3. kunatakiwa kuwe na sehemu ya ku login watu wote, kwakutumia email ,namba ya simu , card ya mpiga kura au card ya uwanachama wa chadema.
4.Kila users anatakiwa kuwa na wallet kwajili ya malipo mbalimbali kama michango ada za uwanachama na nk
5.Weka njia za kawaida za malipo na card za mbenk ili users waliko ndani na nje ya nchi wasiapte shida ku top up balance kwenye account zao na kufanya malipo
6.Akikisha wesite ina rusha matangazo moja kwa moja bila kutegemea chanzo kingine kama YouTube na Vimeo nk
7.Tengeneza App ya hii website
8.Wanachama tulioko Tanzania wenye sifa za kupiga kura tupewe form kwenye account zetu tujaze majina mkoa wila mpaka vituo
tuliko jiandikisha.
9.Wana ccm wenye taarifa za siri nao wawekewe mazingira ya kumtumia ujumbe Lisu moja kwamoja kupitia kwenye site bila kuvuja.
Kuna mambo mengi sana mnapaswa kufanyika kabla ya kampen kuanza.
 
Back
Top Bottom