Website Kwaajili ya Watu Wenye Sura Zenye Mvuto Pekee

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18
</SPAN>


Tovuti ya Beautifulpeople.com inayosajili watu wenye mvuto pekee

Tovuti kwaajili ya kutafuta wachumba ambayo huwatenga watu wenye sura mbaya zisizo na mvuto imezidi kukua na wanachama wake wamezidi kuongezeka.


Pamoja na kupigiwa kelele kwa kutengeneza matabaka ya watu, website kwaajili ya kutafuta wachumba ambayo huwatenga watu wote wenye sura mbaya ambazo hazina mvuto, imezidi kukua na kufungua matawi zaidi ya tovuti hiyo kwenye nchi mbali mbali duniani.

Beautifulpeople.com inasisitiza kuwa mtu anayetaka kuwa mwanachama wa tovuti hiyo lazima atume picha yake kwanza ili wanachama waliopo waijadili kama ana sura yenye mvuto aruhusiwe kuwa mwanachama.

Kutokana na njia hiyo inayotumika kupata wanachama, ni mtu mmoja tu kati ya watano wanaotamani kujiunga na tovuti hiyo ndiye hufanikiwa kukubaliwa kujiunga na kundi la watu wenye mvuto duniani la tovuti hiyo.

Tovuti hiyo ilianzishwa miaka michache iliyopita nchini Denmark na baadae ilifungua matawi yake nchini Uingereza, Japan na Marekani na sasa imeamua kuruhusu wanachama toka nchi zote duniani.

"Kama utaenda baa na kuamua kumtongoza mtu lazima utamchagua yule aliyekuvutia, huwezi kwenda kwa mtu mwenye sura mbaya asiye na mvuto", alisema Greg Hodge mwenye umri wa miaka 34 ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa tovuti hiyo.

"Watu wamechoka kupoteza muda na pesa kukutana na watu ambao hawana mvuto wowote wa kimapenzi", alisema Greg.

Hadi sasa tovuti hiyo ina jumla ya wanachama 180,000 ambao wanakubalika na tovuti hiyo kama watu wenye mvuto.


 
Mvuto zaidi-Gharama zaidi!

After all, kigezo cha mvuto wa Sura mi naona kama hakitoshelezi kwa watu wote!..

Hivi hawa hawajui kwamba kuna midada ambayo anapocheka ni kama analia, lakini mpeleke kwenye shughuli, nakwambia utauza simu.
 
Mvuto zaidi-Gharama zaidi!

After all, kigezo cha mvuto wa Sura mi naona kama hakitoshelezi kwa watu wote!..

Hivi hawa hawajui kwamba kuna midada ambayo anapocheka ni kama analia, lakini mpeleke kwenye shughuli, nakwambia utauza simu.
Ha ha ha! Hiyo kweli mkuu
 
Nikituma picha yangu watachoma hapo hapo! Embu nicheki hapa kwenye hili pozi.

6715d1258702308-website-kwaajili-ya-watu-wenye-sura-zenye-mvuto-pekee-choka-mbaya.jpg
 
nguli jamani mbona umeharibu siku yangu wewe haa hiyo picha gani lakini

Umenisononesha sana umenibagua kumbe ndio maana get tugeza huji ungekuja ungekaa mbali na mimi ndio matatizo ya nternet hayo hujui unaechati naye yukoje.
 
Back
Top Bottom