Elections 2010 Webmaster na PRO wa NEC wawajibishwe

Mashayo

Member
May 29, 2007
22
0
Inasikitisha sana kuona website ya tume ya uchaguzi inakosa matokeo rasmi ya uchaguzi licha ya maafisa mbalimbali wa tume hiyo kuyatangaza rasmi matokeo ya majimbo mbalimbali.

Wakati nafungua tovuti hii nilitengemea kukuta ukurasa wa 'Live Results' matokeo yake nimekosa hata wa 'Yesterday Results'.

Kama waandishi wa habari pamoja na baadhi ya watu binafsi tayari wana soft copy ya matokeo ya majimbo mbalimbali (majimbo zaidi ya 44 hadi sasa), ni nini kinachowazuia webmaster au PRO wa NEC kuyaweka kwenye website ya tume?

Watanzania walioko nje ya nchi ambao hawakamati Chanel Ten, ITV na TBC watajuaje matokeo? Mtu ambaye alikuwa anaangalia TV simu yake ikaita gafla akirudi atajuaje matokeo au mnataka ariwaindi 'Re-wind' TV?

Au na kwenye ku-upload matokeo kuna vifaa mnangojea bado havijafika...? acheni kutuabisha watanzania. Kazi ya ku-upload file la matokeo inaweza kufanyika hata kutumia simu ya mkononi. Pia kwa kompyuta ya kizamani kabisa itakuchukua kama sekunde 55 hivi. Kifaa kinachoitajika hapo ni kompyuta na internet tuu.

Can you imagine website ya tume hata News Update ya kutangaza hatma ya uchaguzi wa Zanzibar haina? au inaamaana hamjui kuwa Dr. Sheini ashatangazwa kuwa Rais mteule Zanzibar?

Hivi nyie watendaji wa NEC, hamjisikii aibu kuona watu wanatafuta matokeo rasmi kwenye blog na website binafsi wakati nyie mpo na uwezo wa kuyaweka hewani mnao? Hamuoni hatari ya kitakachotokea endapo yatapotoshwa? Hivi mkilipwa mshahara au allowance kwa kazi ambayo hamkufanya mtajisikiaje?

Hivi mnajisikiaje kuona blog na tovuti za watu binafsi zimesheheni matokeo uchaguzi ya majimbo mbalimbali alafu ya TUME ya Taifa haina? Pia mnajiskiaje kuona Raisi wa Nchi anazungumzia maswala ya mkonge wa taifa, e-government, seacom na n.k alafu nyie hata ku-update website at the right time kunawashinda? kama mmezidiwa na kazi ni vyema mka outsource webmaster mapema.

Kama kuna mtu nimemkwaza naomba anisamehe, lakini nimeandika hivi kwa uchungu sana. nimekasirika sana kuona uzembe wa mtu mmoja au wawili (NEC staff) unasababisha mamia ya watanzania kupoteza muda mrefu kwenye Internet kusechi google.com na blog mbalimbali kutafuta matokeo ya uchaguzuzi. Kwani hao wenye blogs wameweza wananini na nyie staff wa NEC mshindwe kwanini
 
Okay okay.

Hivi wanaofanya kazi NEC huwa wanajishughulisha na nini baada ya uchaguzi kwisha, ukianchia mbali uandikishwaji wa wapiga kura ambao nao hufanyika kwa msimu.
 
wizi mtupu. Nadhani kuna haja ya kuwaajiri kwa mkataba wa mwaka 1 wa uchaguzi kuliko ilivyo sasa wana ajira ya kudumu. Sasa hivi uchaguzi umeisha hawana kazi tena watakuwa ofcni wana sign in na kukaa wakipiga story mpaka saa nane wana sign out.
 
Inasikitisha sana kuona website ya tume ya uchaguzi inakosa matokeo rasmi ya uchaguzi licha ya maafisa mbalimbali wa tume hiyo kuyatangaza rasmi matokeo ya majimbo mbalimbali.

Wakati nafungua tovuti hii nilitengemea kukuta ukurasa wa 'Live Results' matokeo yake nimekosa hata wa 'Yesterday Results'.

Kama waandishi wa habari pamoja na baadhi ya watu binafsi tayari wana soft copy ya matokeo ya majimbo mbalimbali (majimbo zaidi ya 44 hadi sasa), ni nini kinachowazuia webmaster au PRO wa NEC kuyaweka kwenye website ya tume?

Watanzania walioko nje ya nchi ambao hawakamati Chanel Ten, ITV na TBC watajuaje matokeo? Mtu ambaye alikuwa anaangalia TV simu yake ikaita gafla akirudi atajuaje matokeo au mnataka ariwaindi 'Re-wind' TV?

Au na kwenye ku-upload matokeo kuna vifaa mnangojea bado havijafika...? acheni kutuabisha watanzania. Kazi ya ku-upload file la matokeo inaweza kufanyika hata kutumia simu ya mkononi. Pia kwa kompyuta ya kizamani kabisa itakuchukua kama sekunde 55 hivi. Kifaa kinachoitajika hapo ni kompyuta na internet tuu.

Can you imagine website ya tume hata News Update ya kutangaza hatma ya uchaguzi wa Zanzibar haina? au inaamaana hamjui kuwa Dr. Sheini ashatangazwa kuwa Rais mteule Zanzibar?

Hivi nyie watendaji wa NEC, hamjisikii aibu kuona watu wanatafuta matokeo rasmi kwenye blog na website binafsi wakati nyie mpo na uwezo wa kuyaweka hewani mnao? Hamuoni hatari ya kitakachotokea endapo yatapotoshwa? Hivi mkilipwa mshahara au allowance kwa kazi ambayo hamkufanya mtajisikiaje?

Hivi mnajisikiaje kuona blog na tovuti za watu binafsi zimesheheni matokeo uchaguzi ya majimbo mbalimbali alafu ya TUME ya Taifa haina? Pia mnajiskiaje kuona Raisi wa Nchi anazungumzia maswala ya mkonge wa taifa, e-government, seacom na n.k alafu nyie hata ku-update website at the right time kunawashinda? kama mmezidiwa na kazi ni vyema mka outsource webmaster mapema.

Kama kuna mtu nimemkwaza naomba anisamehe, lakini nimeandika hivi kwa uchungu sana. nimekasirika sana kuona uzembe wa mtu mmoja au wawili (NEC staff) unasababisha mamia ya watanzania kupoteza muda mrefu kwenye Internet kusechi google.com na blog mbalimbali kutafuta matokeo ya uchaguzuzi. Kwani hao wenye blogs wameweza wananini na nyie staff wa NEC mshindwe kwanini

Pole sana Mashayo, naelewa hasira yako and I sympathise with you. Msingi wa tatizo la utendaji katika serikali ya Tz ni kuwa watendaji wa ngazi ya juu wamechakachuliwa akili zao na ubora wao (competence). Ukiwa na akili huteuliwi na ukiwa mtendaji bora huteuliwi kuwa mtendaji wa ngazi ya juu. Wanataka watu wajinga wajinga au legelege tu ili waweze kuwaburuza. Legelege akipewa madaraka ya juu naye anahakikisha kuwa aliye chini yake ni legelege zaidi yake ili naye aweze kumburuza, na huyu naye hivyo hivyo. Mtindo huu umejenga mfumo wa utendaji ambao mchambuaji mmoja mtanzania ameuita "successive incompetence". Mtindo huu umeanza tangu nyakati za awamu ya kwanza kwa hiyo utendaji umekuwa ukididimia awamu moja baada ya nyingine hadi sasa unaelekea kwenye SIFURI hasa katika yale majukumu yake ya msingi ya kulinda MALI, UHURU na UHAI wa kila raia.

CCM nayo imekumbwa katika mfumo huo huo na hivyo viongozi wake wamechakachuliwa kwa akili zao na utendaji wao katika yale maeneo muhimu kwa maendeleo ya taifa ndiyo maana ni muhimu sana kubadilisha chama kinachotawala ili kuweka uwezekano wa kubadilisha utendaji wa Serikali na taasisi zake, kutoka kiwango ambacho kwa sasa kinachokaribia sifuri na kuanza kuboresha utendaji huo.
 
Ile site yao ni ya Joomla. haifai kwa tume kama ile. hata wangeweka matokeo pale ni rahisi sana kuwa-hacked! Hamna kitu pale
 
Duh ndugu, hiyo habari ya legelege kuajiri legelege kama unao ushaidi wa kutosha basi taifa lishaingia doa. Manake wakati nasoma hii thread yako nimeshtuka hadi nikaskia nywele zinataka kusimama.

Bila kusahau naomba turushie huo uchambuzi wa "successful incompetence" manake japo sijauona natumain utafaa sana kutumika kutia chachu kwenye maeneo mengine ya maendeleo haswa haswa katika taaluma ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom