We jamaa, nakupenda ujue

Mchumba

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
276
260
Wana MMU kuna guy humu ndani yaani nimetokea kumpenda kitambo mno, ngoja tu leo niamue kufunguka.

Jamaa mwenyewe anatumia avatar ya madenge,kila nikilikariri ID yake inanipotea kichwani.

Wajameni naombeni mumfikishie huu ujumbe popote pale alipo kwani anakaumiza haka kamoyo kangu.

Ni mtu wa jokes sana kwenye comments zake kama ilivyo avartar yake, ila inaonekana ni mtu intelligent sana, majukwaa anayopendelea ni MMU, SIASA, UCHUMI, PHOTOS, CHIT CHAT na JOKES.

Nimemuwinda kule kwa wakubwa tangu 2012 nimpe za uso namna anavyonitesa mie ila haonekani.

Naomba mnisaidie kumfikishia huu ujumbe popote pale mtakapomuona.

We jamaa acha kunitesa, nishakupenda ujue.
 
mmmh naona umeamua kujilipua. ngoja nianze kumsaka popote alipo aje hapa....zama za uwazi hizi kisa cha kufa na jakamoyo? maisha yenyewe mafupi haya....
Maumivu ya moyo yakizidi inabidi ujilipue tu mwaya...lol
 
Mchumba, kuna mtu mmoja humu anaitwa asigwa!!

nahisi yeye ndiye ana kiavatar cha madenge akiwa anajishika kichwani hivi kama sijakosea!!

haya jiandae kula pendo!
 
Last edited by a moderator:
Wana MMU kuna guy humu ndani yaani nimetokea kumpenda kitambo mno, ngoja tu leo niamue kufunguka.

Jamaa mwenyewe anatumia avatar ya madenge,kila nikilikariri ID yake inanipotea kichwani.

Wajameni naombeni mumfikishie huu ujumbe popote pale alipo kwani anakaumiza haka kamoyo kangu.

Ni mtu wa jokes sana kwenye comments zake kama ilivyo avartar yake, ila inaonekana ni mtu intelligent sana, majukwaa anayopendelea ni MMU, SIASA, UCHUMI, PHOTOS, CHIT CHAT na JOKES.

Nimemuwinda kule kwa wakubwa tangu 2012 nimpe za uso namna anavyonitesa mie ila haonekani.

Naomba mnisaidie kumfikishia huu ujumbe popote pale mtakapomuona.

We jamaa acha kunitesa, nishakupenda ujue.

Wewe mwenyewe mzuri..??? Unalipa...??? Usije ukamfanya mtu ajione amedharauliwa...
 
Humu ndani kuna kitu kinanichanganya. Ina maana watu wanajuana phyisicaly au. Kwa sababu unapompenda mtu si inabidi uwe umemuona. Au unampenda mtu kwa comments zake. Kama ni kwa comments sidhani kama kuna love hapo. Muda si mrefu zitakuja mada mpya za Majuto hapa na habari za X kama tulivyoona kwa wengine humu ndani.
 
Umevurugwa wewe!! Avatar tu umezimika je akiwa mjomba(mlugaluga) au wewe ni morijo(polygon)?
 
Back
Top Bottom