We demand to be told the truth Uchaguzi umeisha -Polisi na Usalama wa Taifa

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,874
2,000
Ndugu watanzania .Natumia neno hili maana jambo ninalotaka kulisema linamuhusu kila Mtanzania .Uchaguzi umeisha Igunga mambo mengi yametokea lakini mimi kuna mambo makuu machache ambayo sikuyapenda na yna hatari mno kwa usalama wa Nchi na ustawi wa demokrasia ya Nchi yetu .Wanasiasa aliendesha siasa chafu sana kwa kudai mambo mazito achilia mbali kwaa Rage kusimama na silaha mkutanoni .

Mukama n Mchemba walitoa matamko kadhaa kwenye jukwaa la siasa wakituhumu Chadema kamba wamelet watu toka Afghanstan wakiwa tayari kuhujumu uchaguzi kwa kujilipua naamini ndiyo ilikuwa maana yao .Baadaye wakasema kuna Mungiki wa Chadema , Baadaye wakasema kuna waatu wamekamatwa wakiwa ni wapiga kura ambao si wa Igunga lakini ni wapenzi na wanachama wa Chadema .Mwisho tukasikia kuna Intarahamwe wa Chadema zaidi ya 800 wako Igunga na vijana wa Chadema toka Arusha .

Matamshi yale yaliidhalilisha sana Nchi , Jeshi la polisi , Jeshi la wananchi na Usalama wa Taifa .Niliingiwa na hofu kubwa maana sikuwa najua kesho kutakucha vipi .

Chadema walisema kuna watu wamekwa kambini Singinda na ni watu wa CCM , matukio ya tindikali yakajitokeza na mwisho jana Nape amedai kwamba watu waliogopa tindikali kujitokeza kupig kura .
Ndugu wana JF haya yalikuwa madai makuba na hatari .Ni bora sasa Mukama na kila aliyetoa tamko la ain hiyo hapo juu wahojiwe watoe taarif za ushahihi na ushahidi juu .Watueleze waliingiaje Tanzania na wamekamatwa wangapi na kama kesi ziko mahakamani tayari au kun kuhojiwa na lini watafikishwa mahakamani pamoja na sponsors wao ambao walidaiwa kuwa ni Chadema.

Nimeshangaa sana IGP amesifu kampeni zile na jeshi lake wakati kuna tuhuma nzito zimetolewa na watawal lakini amekaa kimya.Nchi hii ni yetu ila tuna viongozi ambao ni wachache wanao tuongoza na si kututawala .We demand to be told the truth vinginevyo aina hii ya kampeni si njema hata kidogo kwaTanzania .Leo wanasema watu hawakujitokeza kupika kura kumbe hawajui kwamba pamoja na kuto hakiki daftari lakini pia vita ambayo Mukama na genge alikuwa anahubiri jukwaani is one of the factor watu walikaa mbali .Tuambiwe ukweli sasa zimeisha na baada ya hapo tuelezane kama aina hii ya siasa zinatakwa Tanzania .
 

Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
0
Kukosekana kwa post za majibu kwa masaa yote 12 ni dalili tosha kuwa thread haina mashiko
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,519
2,000
Hata yule Mbunge Dokta Mwakyembe aliyeliingiza Taifa kwenye deni la Dowans kwa baraka za Sitta, aliwahi kusema katumiwa Al Shabab wamuuwe!

Hayo ndio wewe umeyasikia, ungekuwa jikoni na kusikia kila wanachokisikia wanausalama usingeishi hapa duniani, ungetafuta sayari ya kwenda kuishi.
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,179
2,000
Kukosekana kwa post za majibu kwa masaa yote 12 ni dalili tosha kuwa thread haina mashiko
Ungekuwa ule uzushi wa kuingiza makomandoo ungesupport vibaya mno lakini kwa sababu ni hoja inayohitaji utafiti na kuumiza akili ndiyo maana umetoa majibu mepesi. Mbona HB thread zake zinakwenda mbali mpaka page ya 6-10 unataka kuniambia kuna la maan lolote kule zaidi ya blah blah!
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,179
2,000
Hata yule Mbunge Dokta Mwakyembe aliyeliingiza Taifa kwenye deni la Dowans kwa baraka za Sitta, aliwahi kusema katumiwa Al Shabab wamuuwe!

Hayo ndio wewe umeyasikia, ungekuwa jikoni na kusikia kila wanachokisikia wanausalama usingeishi hapa duniani, ungetafuta sayari ya kwenda kuishi.
Nakubaliana nawe na ndiyo maana kuna uchujaji wa habari lakini madai mengine yanayotolewa na viongozi wetu hayapaswi kupuuzwa na kinachofanya habari iwe kweli ni ushahidi, kama mtu ana ushahidi kwa nini asihojiwe na kuona ushahidi wake una ukweli kiasi gani? Kushindwa kuwahoji viongozi ni uthibitisho wa ukweli wa madai hayo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom