We Dada mzuri Wa Simba uliyeniwezesha kuingia CCM Kirumba tarehe 28.05.2022 Mungu akupe uombacho na uishi miaka mingi sana!

kidunula1

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
6,299
6,321
Shukurani zangu kwake!
Nikiwa nimefika nje ya CCM Kirumba Stadium Kwa ajili ya kushuhudia timu kubwa kuliko zote hapa nchini, timu pendwa kuliko zote nchini, YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB "The Citizens Team", Mabingwa kihistoria wakikata mdomo na mkia Wa mtu saa 5 asubuhi na kukuta tiketi zote zimeisha Kuna Dada mmoja mhindi aliyevalia jezi ya Simba iliyompendeza sana akarudisha matumaini yangu ya yaliyokuwa yametoweka!

Huyu Dada Naamini anasali sana, anamuamini sana Mungu na mpenda haki. Na katika maisha ya kidunia Kwa lugha nyepesi niseme hana njaa!.

Nilifika nje ya uwanja saa 5 asubuhi nikiwa na jamaa yangu na kukuta tiketi zote zimeisha. Kuna muda tukatafuta hata tiketi ya elfu 10 Kwa elfu 30 ikashindikana. Ilipofika saa 7 na nusu tukawa tumekata shauri na kuamua kwenda kutafuta sehemu nzuri ya kuangalia hiyo mechi kwenye TV. Tukiwa tupo njiani katikati ya umati Wa watu akatokea Dada akiwa na bro mmoja wote wakiwa wamevalia jezi za Makolowizard zilizowapendeza sana huku wakiwa na haraka sana. Katika ule mpishano wetu Wa haraka sana ghafla nikasikia Yule Dada aiksema nina tiketi 3 hapa anayehitaji na nitamuuzia Kwa shilingi elfu 11 tu kiasi cha watu kuona kama ni masihara mana wengi walikuwa wakirudi majumbani na mtaani kwa kushindwa kuingia uwanjani. Nami nikajitosa kama utani nikamuita Kwa nguvu huku nikionyesha nia ya kuhitaji miongoni mwa hizo tiketi. Dada akasimama ghafla na yule bro nikamsogelea nikamwambia Mimi nahitaji tiketi mbili akazama kwenye pochi yake alokuwa ameivaa na kuibuka na tiketi, nikampa hela kama masihara. Pale pale akaja bro mmoja naye akaungana na Mimi akampa hela na hivyo kufanya zile tiketi 3 kuwa zimeisha.

Kilichofanya niandike huu Uzi ni namna yule Dada alivyonistaajabisha Kwa moyo alionao ambao Kwa Yale mazingira yalivyikuwa nilimtafsiri kama mcha Mungu,Mpenda haki,mpenda mpira Wa miguu, mwenye upendo Kwa binadamu wenzake bila kujali itikadi,rangi na asiye na njaa Kwa sababu zifuatazo:-
1. Alikuwa amevaa jezi na kits za Simba lakini akatupa tiketi Mimi na jamaa yangu tuliokuwa na kits za Yanga ilihali kulikuwa na wanasimba wengi walokuwa na jezi kama yeye walokuwa wana tatizo kama langu.
2. Wakati anatoa zile tiketi kwenye pochi yake ndipo watu wakaamini kwamba Dada ana hizo tiketi na ghafla wakaja watu walokuwa na kits za Simba Na Yanga wakapandilia Kwa juu. Wapo walomwambia watampa elfu 15, na wengine 20 ila yule Dada akanishangaza Kwa kuwaambia "No! Huku akiweka ishara ya mkono, Nitawapa hawa watatu waliowahi na nitawauzia Kwa elfu 11 tu!" Na hiyo ndio ilikuwa ni bei halisi ya majukwa ya mzunguko mana ilikuwa ni elfu 10 ukiweka na gharama ya kadi ya N card ndio inakuwa elfu 11 ( Hapa ndipo palipofanya nimuone dadangu ni mcha Mungu, mpenda haki na asiye na njaa). Baada ya kunishangaza hivi niliomba japo nimpige kiss la upendo akaishia kutabasamu yeye na yule bro aliyekuwa naye kisha wakaondoka fasta bila kusema chochote!

Je ungekuwa wewe ungefanya kama huyu Dada kwenye kiwingu cha watu takribani elfu 5+??, usingeuza hizo tiketi Kwa elfu 20,30,40 n.k?, Usingezingatia itikadi Kwa kujali walovaa kama wewe? Dada ulinifunza sana na uliiwakilisha vema timu yako!
 
Hapa ndpo mtu unaona kabisa JF haina huruma na ina ubaguzi!🤣🤣uzi tangu jana saa 8:56 pm no comment mpaka mimu nilipokuja kuuokoa saa 12:14 am
 
Back
Top Bottom