Uchaguzi 2020 WCB yamwaga mamilioni kwa kigogo CCM

Hiyo hadithi yako tungeiamini Kama usingemuhusisha diamond na ubunge, diamond amejikita kwenye mziki zaidi na mziki wake unamlipa kuliko hata huo ubunge.
 
Ndefu pumba tupu,umepoteza muda wako bure,wewe ni bure kabisa!
*Lengo awasaidie ubunge Diamond, Babu Tale

Na MWANDISHI WETU

WAKATI homa ya Uchaguzi Mkuu wa Udiwani, Ubunge na Rais likipanda Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB) linaloongozwa na msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeanza kujipanga kwa viongozi wake kutaka kuwania ubunge na udiwani.

Katika kile kinachoonekana kujipanga Diamond na kundi la lake sasa wanamwaga mamilioni ya fedha kupitia Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM ambayo inaongozwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole ambapo inadaiwa kundi hadi sasa imeshahongwa Shilingi milioni 100 ili kuwasaidia viongozi wanaounda kundi la WCB.

Fedha hizo pia zinatajwa kama sehemu ya kishawishi kwa Idara ya Uenezi ambayo imekuwa ikiratibu shughuli za hamasa hasa katika kampeni huku mameneja wa Diamond wakitajwa kuwania ubunge akiwamo Hamis Taletale maarufu kama Babu Tale ambaye kwa sasa anataka ubunge katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, linaloongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba.

Mbali na Tale pia meneja mwingine wa Diamond ambaye amekuwa akifanya ushawishi wa kutaka ateuliwe kuwania ubunge katika Jimbo la Mbagala ni Said Fela maarufu kama ‘Mkubwa Fela’ ambaye kwa sasa ni Diwani wa Kata Kilungule Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

“Kwa sasa Diamond anatumia nguvu kubwa ya kufanya ushawishi wa chama ikiwamo kugawa fedha kupitia Idara ya Uenezi kwanza ili atengeneze upepo ili chama kimteuwe awanie ubunge Kigoma Mjini, lakini si hilo tu hata mameneja wake, Babu Tale ambaye sasa kila wiki amekuwa na ziara katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki hasa kijijini kwao Mkuyuni naye anataka ubunge.

“Si huyo tu pia yupo Said Fela ambaye naye ameanza kampeni za chinichini kutaka ubunge katika Jimbo la Mbagala, hili si jambo la kufumbiwa macho. Na hili ndilo linalowafanya wajione wao wanawezo wa kukitia mfukoni chama Babu Tale amemwambia kaka yake Idd Taletale naye agombee udiwani Kata ya Makurumla Manispaa ya Ubungo kwa lengo la kutaka kuwang'oa viongozi wa CCM wa Kata ambao wamekuwa kikwazo kwao kutokana na kuonekana kumbeba aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilimahewa Idd Towatowa ambaye naye anakabiliwa na kesi ya ufisadi katika Saccos ya Urafiki.

“Tena ninachotaka kukwambia wapo baadhi ya watu ambao hujitambulisha kuwa ni wasaidizi wa Polepole ambao kila baada ya siku mbili huenda katika maskani ya kila Tale pale Mwembechai na hupewa fedha tena huitwa kwenye gari maalumu na kisha hupewa bahasha.

“…chama inabidi kifuatilie kwa makini maana pia wapo baadhi ya viongozi wa chama wa wilaya za Ubunge na Temeke nao hutumia mwanya huo kwenda kujichotea fedha, hadi sasa ninachotaka kukwambia zaidi ya milioni 100 wale watu wa Polelepole wameshachukua,” kilisema chanzo chetu ambazo hakikutaka kutajwa jina gazetini.

Katika ziara ya Diamond aliifanya mwishoni mwa mwaka jana mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 10 ya tangu alipoanza na sanaa ya muziki, alikodi mabehewa ya treni sambamba na kukabidhi msikiti alioujenga mjini Kigoma.

Hata hivyo hatua hiyo ilitajwa kama sehemu ya mkakati ya kutafuta ushawishi wa chama, ambapo alifanikiwa kumvuta Katibu wa Itikati na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ambaye alifanya ushawishi wa kisiasa ikiwamo kumpigia simu Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli pasi na kujua kilichojificha nyuma ya mkakati huo.

Licha ya mkakati huo ambao sasa unaonekana kukwama hasa baada ya viongozi wa CCM katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Kigoma ambao wameanza kufuatilia nyendo za wasanii hao kwa kila hatua ikiwamo kufungua majalada ya maadili.

Katika kile kinachoonekana jotyo kuanza kupanda CCM kimetoa ratoba ya awali ya mchakato wa kuwapata wabunge na madiwani ambapo fomu zitaanza kutolewa kuanzia Julai 16 hadi 20, 2020 na Julai 23 vikao vya kamati za siasa kukaa na kuanza kuwajadili wagombesa kwa kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za mikoa.

Julai 25, vikao vya Kamati za Siasa za mkoa kuwajadili wagombea na kutoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar kutoa mapendekezo kwa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanziabar.

Julai 27, 2020 Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar kuwajadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu na Julai 30, kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuwajadili wagombea na kufanya uteuzi wa mwisho.

“Agosti 2 hadi 4, 2020 kupiga kura za maoni Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya/ Jimbo kwa upande wa ubunge. Agosti 5, 2020 Vikao vya Kamati za Siasa za Wilaya kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Mikoa huku Agosti 6 ikiwa ni vikao vya Kamati za Siasa za Mkoa kuwajadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar.

“Agosti 7, Halmashauri Kuu za Mikoa kufanua uteuzi wa mwisho kwa wagombea udiwani. Na Agosti 9, 2020 Kikao cha Kamati Maalumuya Halmashauri Kuu kuwajadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu ya CCM Taifa,” ilieleza ratiba hiyo ya awali ya CCM

Pamona na hali hiyo Agosti 12 hadi 13 Kamati Kuu ya Taifa itawajadili wagombea ubunge na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu.

Agosti 8, 2020 Halmashauri Kuu itawajadili na kufanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea ubunge.

DK. BASHIRU NA RUSHWA

Kutokana na kile kinachoonekana kuiva kwa mchakato wa kuwapata wagombea ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, kila wakati amekuwa akitoa onyo kwa wanachama wa chama hicho waliogeuza uchaguzi ni sawa na soko la kununua au kuza kura huku akisema sasa hawana nafasi.

Katika ziara yake katika mikoa ya Tanga na Kigoma, alivitaka vikao vya uteuzi kutenda haki kwa wagombea wote ikiwamo viongozi kuacha chuki.

Pamoja na hilo alisema chama hicho hakitamwacha yeyote atakayehuska katika rushwa, wakati ikielekea kwenye uchaguzi Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Alisema matokeo ya rushwa katika kutafuta nafasi za uongozi yamekuwa na maumivu kwa wagombea na kusababisha kupata vipongozi wasiostahili, ambao mwisho wake hawawezi kuwa watumishi wa wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom