WCB wamebet vibaya kwa Lavalava na Maromboso

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,792
15,693
Nianze kwa kuwapongeza WCB kwa hatua waliyofikia kuisimamisha lebo na kuwa lebo bora zaidi Afrika Mashariki, na moja ya lebo bora Afrika.

Niwapongeze kwa kuweza kuviinua vipaji ambavyo vilikuwa havitambuliki kabisa kwenye ulimwengu wa muziki na kuweza kupokelewa vyema, vipaji hivyo ni Harmonize na Rayvanny.

Niwapongeze tena kwa kufanikiwa kumuibua tena msanii mwenye kipaji cha hali ya juu Rich Mavoko ambaye alikuwa anaelekea 'shimoni' na anaendelea kufanya vizuri na kupata riziki kupitia muziki, pengine bila WCB tungekuwa tunamsikia kwenye stori za ngada kama ilivyokuwa kwa Ray C alipokuwa Kenya, Queen Darlin nisimzungumzie maana nahisi kaingia pale kama dada wa bosi, si kipaji.

Baada ya pongezi nije kwenye hizi new signings ambazo ni Lavalava na Maromboso, nikianza na Lavalava nilijaribu kuwa mvumilivu nisimjaji mapema niendelee kumsikiliza ila pamoja na kumpa muda na kusikiliza nyimbo zake zaidi ya 4 sijaona kama ana impact kubwa, nyimbo zake ni nzuri ila ni za kawaida sana, hazistui yaani.

Unajua msanii anapokuwa kwenye lebo kubwa tunatarajia makubwa sana sasa unapotoa nyimbo za kawaida lazima tushangae umeaminikaje kuwa pale, pia nikija upande wa Maromboso huyu mtu alikuwa anasubiriwa sana kuona atafanya nini baada ya wenzake kina Aslay na Beka kuwa wameshasikika sana, na kuna baadhi ya watu walikuwa wanaamini Maromboso ni mkali kuzidi wote pale walipokuwa Yamoto Band, nadhani na Fella amewaingiza chaka WCB wakaamini hivyo, ila kwa hizi nyimbo 2 alizotoa sijaona hata mmoja unaostua, ni nyimbo za kawaida sana 'beyond expectations', sidhani kama anaweza toboa kwa nyimbo za namna hii, unajua nyimbo nzuri ni kama pembe la ng'ombe (halifichiki), Aslay kipindi ameanza kutoa nyimbo zake alikuwa hata hapeleki Clouds, anaweka U-Tube tu then mitaa inaongea, hili promo wanalompa sahivi wamedandia tu baada ya kuona dogo ana impact kubwa.

So kama Mbosso angekuwa anatoa vitu vikali hata bila ya promo la Clouds angetoboa tu.

Kwa upande wangu hapa kwa Lavalava na Mbosso WCB na 'Mendes' wao wamefanya usajili mbovu, wangemsajili Aslay wangepiga hela mno
 
Maromboso ni level zingine amekamilika kila idara kuanzia uimbaji, utungaji hadi live performance ukitaka kuona ubora wke acha kumfananisha na hao wakina Asley na Beka

Lavalava anaimba bongo fleva ya zamani izi nyimbo zke ukifatilia ni km za Diamond wa kipindi kile cha kamuambia na mbagala nyimbo zina mashahiri ya kuchomwa na kuumizwa huu mziki cku izi ni wachache wana sikiliza
 
WCB HAWACHUKUI MTU KWA AJILI TU YA KUWA NA WATU WENGI.WCB WALIMISS AINA YA MUZIKI WANAOUFANYA MBOSSO NA LAVALAVA.NADHANI NI MZIKI FULANI AMBAO UMEKAA KATIKA MAHADHI YA KITANZANIA 100%.
Kuhusu Aslay yuko poa ila ANAIMBA STYLE moja na huko alipoamua kujiweka mwisho siku watamtumia na kumtupa.
 
Ashley sahiv kashakuwa mlevi....anabwiga pombe sana ...mziki wenyewe ushamshinda ...labda uje point nyingine tukuelewe.
 
Huo uandishi hakuna hata paragraghs, nukta wewe unatiririka tu na mapovu yako, hebu rekebisha kidogo basi huo uandishi
 
Hawa jamaa wametoka kwenye kipindi kidumu (Beef zinazo endelea), so watakuja kuwa wasani wazuri waki survive kwenye hili sakata (Kubaniwa) then wakitoboa watakuwa wamejifuza mengi. Ongopa sana yule mtu anaanza kupambana anakutana na changamoto nyingi kwani zina mjenga sana akija kutomboa uto amini
 
WCB HAWACHUKUI MTU KWA AJILI TU YA KUWA NA WATU WENGI.WCB WALIMISS AINA YA MUZIKI WANAOUFANYA MBOSSO NA LAVALAVA.NADHANI NI MZIKI FULANI AMBAO UMEKAA KATIKA MAHADHI YA KITANZANIA 100%.
Kuhusu Aslay yuko poa ila ANAIMBA STYLE moja na huko alipoamua kujiweka mwisho siku watamtumia na kumtupa.
Kwenye mahadhi ndio nnapopapenda mkuu...
ukisikiliza Bora tuachane ,na somo ya kassim mganga... yani unapata ladha ya afrika mashariki kabisa
 
Yaaan kwa upande wangu sijamuelew kabsa lavalava na sjui hata majina ya nyimbo zake basi majuz nmeweka attention nmskilize mboso yule wa ya moto anayejua lkn anaimba kawaida saaan....basi ntazidi kumkubal vanny na mavoko ndan ya WCBs nzima
 
Back
Top Bottom