RockCarnegie
JF-Expert Member
- Jan 17, 2019
- 963
- 1,927
Habari wana JF
Ni wazi kuwa taifa na dunia nzima wako kwenye vita dhidi ya adui asiyeonekana, corona virus. Ni mhimu wote tukaungana kupambana na adui huyu anayehatarisha uhai wetu!
Tatizo langu ni dosari katika kauli za makamanda wetu wanatoa mbinu na maelekezo ya namna ya kupambana na adui corona!
RC wa Dar ndugu Makonda anesikika akihamasisha watu wasifunge kazi zao kwani watakufa kwa njaa badala ya corona! Baada ya siku moja anawatangazia tena kuwa ataanza kukamata wanaozurula ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona!
Swali la kujiuliza kama shughuli za wananchi hazijazuiliwa kuendelea, ni vigezo gani vitatumika kukamata wazurulaji? Wazurulaji wana alama?
Watanzania walio wengi hawako kwenye mifumo rasmi ya ajira, ni watafuta riziki, wanaamka hawana ramani za kazi, watazipata huko huko!
Serikali mnatakiwa kuwa 'specific', muache kubahatisha. Toeni maelekezo ya kueleweka, corona virus anashambulia kila mtu, hoja ya wazurulaji ni hoja ya kibaguzi na inalenga kunyanyasa na kuonea watu bila sababu!