Wazurulaji wanaolengwa kukamatwa na RC Makonda ni akina nani?

RockCarnegie

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
890
1,000
Habari wana JF

Ni wazi kuwa taifa na dunia nzima wako kwenye vita dhidi ya adui asiyeonekana, corona virus. Ni mhimu wote tukaungana kupambana na adui huyu anayehatarisha uhai wetu!

Tatizo langu ni dosari katika kauli za makamanda wetu wanatoa mbinu na maelekezo ya namna ya kupambana na adui corona!

RC wa Dar ndugu Makonda anesikika akihamasisha watu wasifunge kazi zao kwani watakufa kwa njaa badala ya corona! Baada ya siku moja anawatangazia tena kuwa ataanza kukamata wanaozurula ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona!

Swali la kujiuliza kama shughuli za wananchi hazijazuiliwa kuendelea, ni vigezo gani vitatumika kukamata wazurulaji? Wazurulaji wana alama?

Watanzania walio wengi hawako kwenye mifumo rasmi ya ajira, ni watafuta riziki, wanaamka hawana ramani za kazi, watazipata huko huko!

Serikali mnatakiwa kuwa 'specific', muache kubahatisha. Toeni maelekezo ya kueleweka, corona virus anashambulia kila mtu, hoja ya wazurulaji ni hoja ya kibaguzi na inalenga kunyanyasa na kuonea watu bila sababu!
 

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
23,543
2,000
Huyu naye anatuchanganya kila siku anaongea tofauti,jana kasema tupige kazi,leo anasema kesho wanaozurura watakamatwa. Mmekuwa futuhi mara mnasema wafungwa waachiwe kwa ajili ya corona halafu wazururaji wakamatwe kwa ajili ya corona

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
3,900
2,000
Huyu naye anatuchanganya kila siku anaongea tofauti,jana kasema tupige kazi,leo anasema kesho wanaozurura watakamatwa.Mmekuwa futuhi mara mnasema wafungwa waachiwe kwa ajili ya corona halafu wazururaji wakamatwe kwa ajili ya corona

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
Kwa akili yako kupiga kazi ni sawa na kuzurula?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,087
2,000
Vibarua, na wamachinga pia maana sidhani kama wana angukia kwenye kundi muhimu mfano wanaouza mahitaji ya nyumbani ie sokoni nk.

Lakini kwa upande mwingine, chinga wanaweza kuachiwa kwasababu ya vile vitambulisho vyao, jambo ambalo bado linaifanya amri hii kuwa tata na pengine imesababishwa na ukosefu wa mkakati maalum wa kupambana na covid-19.
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
5,756
2,000
Kuanzia asubuhi alfajiri mpaka usiku kuna maelfu ya watu wanaingia na kutoka katikati ya jiji la Dar (hususani Kariakoo na Posta), zaidi ya 99% ya wote hao utawakuta wanatembea kwa miguu katika hiyo mitaa.

Kiujumla watu wote hao wanafuata huduma au bidhaa kati kati ya jiji, iwe kuuza au kununua. Kamwe huwezi kumtofautisha mwenye shughuli rasmi na asiye na shughuli rasmi, wote wanafanana.

Wote ni wazururaji. Nadhani Makonda aliwalenga wote hao, ama basi hakuwalenga hao!
 

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
756
1,000
Kwa akili yako kupiga kazi ni sawa na kuzurula?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi wewe ni jambo gani amelifanya Makonda ukaacha kuunga mkono? Kuzulula anakosema huyo ziro brain ni kupi hasa? Maana hata kazi za machinga kwa maana halisi ni uzululaji unao leta kipato kwa mzululaji!

Katika mistakes kubwa zilizofanywa na awamu ya tano moja wapo ni kumpa cheo Makonda

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom