#COVID19 Wazungu wangetaka kutuua wangetumaliza toka zamani kachomeni chanjo

Ameandika Malisa GJ.

Kumekuwa na mjadala mkubwa sana kuhusu chanjo ya Corona katika nchi nyingi za Afrika. Baadhi ya viongozi wa dini wamedai chanjo hiyo inalenga kupunguza idadi ya watu weusi kwa kuwazuia kuzaliana, na wengine wameihusisha na chapa ya 666 inayodaiwa kuwa ya Mpinga Kristo.

Kufuatia madai hayo mwanaharakati Tracy Zille wa Afrika Kusini ameandika maoni yafuatayo (nimefanya tafsiri isiyo rasmi);
_________
Waafrika wanapaswa kuwa watu wa mwisho kulalamika kuhusu chanjo ya Corona. Kama kweli wazungu wangetaka kuwaua wangeshafanya hivyo miaka mingi iliyopita. Vinywaji vingi vinatoka Ulaya, hadi maziwa ya watoto. Wangetaka kuwaua wasingekua na haja ya kusubiri chanjo ya Corona.

Kitu kikubwa waafrika wanachoweza kutengeneza ni watoto wasio na mpangilio baada ya kufanya ngono kienyeji. Tulieni, hakuna mtu mwenye mpango wa kuwaua. Nyie sio muhimu sana wala sio tishio kwa dunia kiasi cha kutaka kuwaua.

Kama hamtaki chanjo yetu basi tengenezeni yenu. Lakini kama hamuwezi kutengeneza kondomu wala miswaki, mtaweza kweli kutengeneza chanjo ya corona? Hadi vichokoa meno (toothpick) mnaagiza China halafu mko busy kutukana wazungu eti wanataka kuwaua?

Jifunzeni angalau kutengeneza condom kwanza kabla hamjapiga kelele zisizo na msingi kuhusu chanjo ya Corona. Dawa nyingi mnazotumia katika hospitali zenu ni kutoka Ulaya, lakini leo mnajazana ujinga eti wazungu wanataka kuwaua kupitia chanjo ya Corona.

Hata chupi mnazovaa zimetoka nje ya Afrika. Kama sio kutoka China basi ni mitumba kutoka Ulaya na Marekani. Hamuwezi kutengeneza hata chupi za kusitiri maungo yenu lakini mko "busy" kutukana wazungu wanaoumiza vichwa vyao kutengeneza chanjo ya corona.

Hamuwezi hata kutengeneza dawa rahisi ya kutuliza maumivu ya kichwa kama Panadol, lakini mnajazana ujinga eti wazungu wanataka kuwaua. Sasa uamuzi ni wenu. Kuikubali chanjo ya corona mpone, au muikatae mfe kwa ujinga wenu.

Kama sio wazungu midomo yenu ingekua inanuka kama maiti ya panya kwa sababu hamuwezi kutengeneza hata dawa ya meno. Colgate inatengenezwa Marekani, Aquafresh Uingereza, Mentadent Canada, Sensodyne Japan. Tungetaka kuwaua si tungeshawamaliza siku nyingi? Kwanini tusubiri kuja kuwaua kupitia chanjo ya corona?

Tunatengeneza wanasayansi wa kuisaidia dunia, nyie mko busy kutengeneza Mitume na Manabii matajiri. Tunatengeneza chanjo ya corona nyie mnatengeneza mafuta ya upako. Halafu mnasema tunataka kuwaua. Wajinga nyie.

Hata dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKWIMWI (ARVs) zinatoka Ulaya na Marekani. Sasa kama kweli wazungu wanataka kuwaua waafrika si wangeshawamaliza kupitia ARVs? Unakuta mwafrika amekondeana kwa UKIMWI lakini akishameza ARVs za wazungu akapata afya anasema eti wazungu wamebuni chanjo ya Corona ili kuua waafrika. Upumbavu gani huu?

Msinitukane kwa kuwaeleza ukweli. Tumetumia pesa zetu kuwajengea vyuo vikuu (Chuo kikuu UDSM kilijengwa mwaka 1961 na JF Kennedy, Chuo kikuu cha Zambia kilijengwa na Harold Wilson mwaka 1996, Chuo kikuu Nairobi kilijengwa na Anthony Eden mwaka 1956 kikiitwa Royal Technical College).

Hiyo ni mifano tu lakini tumetumia pesa zetu kuwajengea vyuo vingi na vituo vingi vya utafiti. Nyie mnatumia pesa zenu kujenga makanisa makubwa na kuwanunulia Mitume na Manabii magari ya kifahari.

Vituo vyetu vya utafiti vimebuni chanjo za magonjwa makubwa kama surua, polio, tetekuwanga, ndui, homa ya ini etc. Vituo vyenu vya mitume na manabii vimebuni mafuta ya upako. Mnanunua mafuta ya upako kwa gharama kubwa bila kupiga kelele, lakini chanjo ya corona mnayopewa bure mnapanua midomo kuitukana. Mna mdudu kichwani, si bure.

Halafu hii sio chanjo ya kwanza kuwaletea huko Afrika. Tumeleta chanjo nyingi na mmezitumia bila kelele. Chanjo za polio, surua, homa ya ini, tetekuwanga etc. Tungetaka kuwaua si tungetumia chanjo hizo? Kwanini tusubirie ya corona?

Baadhi ya nchi za Afrika mmeanza kuharibu miundombinu ya teknolojia ya 5G kwa kuihusisha na Corona. Hili si jambo la kushangaza kwa sababu mnaua hadi mama zenu wa kuwazaa kwa kuwahusisha na uchawi. Kwa sababu tu ya ngozi zao kusinyaa kwa uzee na macho yao kuwa mekundu kwa kutumia nishati ya kuni, kwenu huo ni ushahidi wa uchawi. Mnawaua bila huruma.

Muda si mrefu mtaanza kuwaua wagonjwa wa Corona kwa kuhisi wamelogwa au wametupiwa mkosi. Haya ndio mawazo ya watu wapumbavu, wasioelimika na washamba kama nyie. Watu ambao mnaamini eti kila nyumba ya tajiri ina chumba maalumu cha kufuga majoka yanayomletea hela.

Sikikizeni nyie wapumbavu. Kama chanjo ya Corona ingegunduliwa Afrika, viongozi wenu wasingeitumia. Wangesafiri kwenda India au nchi za Ulaya kutafuta chanjo nyingine.

Viongozi wa Afrika hawaamini katika huduma za afya za nchi zao. Hawaamini hospitali zao, hawaamini madaktari wao, hawaamini hata dawa zao. Ndio maana wakiugua hata malaria tu wanapanda ndege kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kwahiyo wakati mkiwaza eti wazungu wanataka kuwaua kwa chanjo ya corona, viongozi wenu nao wanawaza mnataka kuwaua kwa huduma mbovu za afya. Ndio maana wanajenga hospitali lakini hawatibiwi humo, wanasomesha madaktari lakini hawawaamini. Wanakimbilia kutibiwa nje. Wanajenga shule lakini watoto wao hawasomi humo.

Chanjo ya Corona ni kengele ya kuwakumbusha waafrika kuchagua viongozi wenye maono na uwezo wa kupambana na matatizo yao. Afrika ingekuwa na uongozi thabiti ingekua bara tajiri zaidi duniani. Lakini kwa sababu ya ujinga wenu wa kuchagua viongozi wasio na maono, wameuza rasilimali zenu kwa wazungu na Wachina, kwa faida yao na familia zao, huku wananchi mkiteseka kwa umaskini.

Badilikeni. Kabla hamjalaumu wazungu,

Nini maoni yako?
"WAMESHINDWA!"

Ropoka hii... Wameshindwa Mashetani hawa wakubwa! MUNGU atawaangamiza viumbe wabaya sana hawa....

Yaani hawa viumbe yapo meengi ya kuwaambia meengii....

Kiufupi wanaumwa kupitiliza! Ila MUNGU msikie tu hivyo hivyo makusudio yao yameshindikana "WAMESHINDWA" MUNGU awashinde awaangamize Amina!

Mtihani mkubwa MWENYENZI MUNGU aliotuletea katika hii dunia ni hawa viumbe wanaitwa " WAZUNGU" Mabalaa yoote, Shida zote, Chokochoko, Ufisadi, Uhasidi, Fitina, Magonjwa Mabalaa ya kila aina! n.k.... ni hawa viumbe wanaoitwa "WAZUNGU"

Huu ni mtihani mkubwa MWENYE ENZI MUNGU katuletea!

Halafu wanaanzaje anzaje kufungua vinywa vyao kuropoka uozo kama huu....
Wanaanzaje?

Yaani yapo meengi mengi ya kuwaeleza viumbe hawa hapatoshi!!!!
 
Back
Top Bottom