Wazungu wamtembelea mtengenezaji helikopta Tunduma

Aug 23, 2015
89
43
Kwa ufupi Kijana Kinyekile ambaye pia ni fundi magari alitumia ubunifu wake kuunda helikopta, kitu ambacho kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, George Mbijima akiwa mjini Tunduma alimtembelea kisha kuweka jiwe la msingi kwenye helikopta hiyo.

Mkazi wa Tunduma, mkoani Songwe, Adam Kinyekile (34) ambaye alikuwa akitengeneza helikopta amepata mwaliko maalumu na wazungu kutoka Afrika Kusini kutembelea kiwanda chao cha kutengeneza chopa.

Kijana Kinyekile ambaye pia ni fundi magari alitumia ubunifu wake kuunda helikopta, kitu ambacho kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, George Mbijima akiwa mjini Tunduma alimtembelea kisha kuweka jiwe la msingi kwenye helikopta hiyo.

Hata hivyo baada ya taarifa za kijana huyo kurushwa kwenye vyombo vya habari , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilipiga marufuku kwa mtu yoyote kutojihusisha na utengenezaji au ubunifu wa ndege bila kufuata taratibu.

Onyo hilo lilionekana kumlenga Kinyekile kwa kazi yake aliyokuwa akiifanya jambo ambalo lilimfanya asiweze kuendelea na maboresho ya helikopta yake licha ya kudai ilikuwa imebaki kuruka.

Akizungumza jana, Kinyekile alisema Alhamisi ya wiki hii alitembelewa na wazungu waliodai ni Raia wa Afrika Kusini kutoka kiwanda cha kutengeneza helikopta na kutaka kuonana naye ili wajionee kazi yake waliyoiona kwenye mitandao.
 
Kiwanda cha kutengeneza helikopta Afrika kusini??? ?? Hakina jina!!!! Nadhan watakua wameipenda teknolojia yake, helicopter inayozunguka kama feni ya darini
 
hii nchi bwana inashangaza sana, yani mtu kagundua kitu halafu badala ya kumsaidia mnatangaza kua hairuhusiwi kujihusisha na utengenezaji bila kufuata utaratibu? utaratibu ni upi? ukifuata huo utaratibu urasimu kibao, TAA walitakiwa wamshike mkono, haya mambo ya ubunifu yanawezekana hata Tanzania ila shida ya viongozi wetu hawaamini ndoto za watanzania, mimi namuombea huyu kijana mafanikio, hata kama ni nje ya Tanzania ili tujifunze kutoka kwake.
 
Nchi ya watengeneza ******. Imagine kijana wa malawi aliyesupply umeme kwenye kijiji chake kwa kutumia windmill aliyoibuni aliweza kupewa tuzo na UN lakini sisi wakwetu hata wakivuma wananyamazishwa sababu ya watu wachache wanaodhani ni miungu mtu.
Huyu safi sana. Cyo wa helicopter. Huyo ndo mbunifu sasa.
 
Wazungu wanaakili sana hapo wamekuja kuchunguza teknlojia ilitumika na huyo mtz km inatofauti na yao.
Wazungu lazima wamchukue.
Ss ngoz nyeusi sijui tumelaaniwa. Ngoja tuendelee kuagiza bidhaa feki na kukopa hela.
 
Ufike wakati hata sisi waafrika tuanze kujiamini mambo mengine huanza kama hayaeleweki lakini mkitia nia na juhudi za pamoja kitaeleweka tu hebu wasomi wetu wasiache elimu ya kwenye madaftari wailete kwa vitendo sasa Afria Arise
 
Nimeamin kuwa cc watu weusi maji ya Baraka yaliishia viganjani na kwenye nyayo....Hata ukigundua dawa ya UKIMWI utasikia mauza uza ya kukuangusha.
 
Wakati serikali ya bongo imepiga marufuku wabunifu kutengeneza chopa, wazungu wanathamini kazi yao. Tutaendelea kuwa watumwa mpaka fikra mbovu zitutoke.
 
Back
Top Bottom