Wazungu waleta fitina mradi wa gesi asili-LNG

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,740
6,429
Jiosmee wazungu wanavyoleta fitina kwenye Gasi ili wasilipe kodi na sisi Tanzania tukose Masoko..Soma gazeti la Mtanzania.Wazungu si watu

MATUMAINI ya Watanzania kupata mapema faida za mradi wa gesi iliyogunduliwa Lindi miaka 15 iliyopita yamedoda kwani juhudi za Serikali kulazimisha mradi huo utekelezwe haraka zimegonga mwamba kwa wadau wa mradi huu kuonesha hawako tayari hadi miaka mitatu ya kujadiliana iishe na kuandika sheria mpya ya kuyapendelea makampuni matano ya mradi huo.

Kampuni hizo ni kampuni za kimataifa za gesi na mafuta za Statoil (Norway) BG Group na Ophir Energy (Uingereza) Exxon Mobil (Marekani), wakishirikiana na Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) kama kampuni ya Taifa ya Mafuta Tanzania (NOC) zijadiliane kwa awamu tano ni mijadala itakayochukua miaka mitano.

Hali hiyo tata imekatisha tamaa watu wengi na kuitaka Serikali itafute wawekezaji wengine ili mambo yaende shoti kuliko kutumia magwiji hawa ambao wana vitimbi na ajenda ya siri kwani kimsingi hawana shida yoyote ya kifedha.

Kwa maana hiyo ndiyo sababu BG Group bado ipo kwenye kundi ingawa rasilimali yake alikwishamuuzia Royal Dutch Shell kwa dola bilioni 55 na inadaiwa na TRA kodi ya ‘capital gains tax’.

Haitaki kulipa ikisubiri sheria zibadilishwe na zilengwe kuwanufaisha wao au Serikali iuze gesi hiyo bei ya jumla ya kutupa na waachane nayo.

Wanoko wa masuala ya uchumi wanasema kuwa Nigeria ilipata na kuendelea kuteseka na kampuni hiyo eneo la Ogoni katika Delta ya Niger na hivyo ikiingia hapa itafanya kasheshe mpaka nchi hii tukome kwanini tulikuwa na gesi.

Ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi ya LNG ni muhimu ili kuweza kuuza gesi yetu nje ya nchi ikiwa kama kichuruzika (liquid) kwa kila hali ni mchakato mrefu na mgumu na sasa ndio kwanza umeanza kwenye hatua inayoitwa Host Government Agreement (HGA).

Yaani hayo ni mapatano kati ya Serikali na kampuni hizo za uchimbaji za nje na mahusiano yao.

“HGA ni makubaliano ya kisheria kati ya mwekezaji wa nje na Serikali ya nchi inahusu haki na wajibu wa mwekezaji kuhusu uendelezaji, ujenzi na uendeshaji wa mradi na mwekezaji wa nje. Huweka misingi ya utendaji kazi na mahusiano,” anasema Prof. Ntalikwa.

Agosti mwaka jana, Rais Dk. John Magufuli, aliagiza Wizara ya Nishati na Madini kuongeza juhudi kwenye mradi wa mtambo wa kuchakata gesi ya LNG ili mradi huo wa dola bilioni 30 au shilingi trilioni 65 haucheleweshwi na vikwazo vya urasimu na kutowajibika kwa upande wa Serikali.

Rais Magufuli alisisitiza kutaka kuona mradi unakwenda mbele, hakujua kuwa suala hilo ni kizungumkuti na lina masilahi ya wengi na hivyo litakwenda tu kwa makubaliano ya wengi (consensus) na huliwezi kulipangia ratiba mjarabu ila kwa maelewano.

Rais Magufuli alizungumzia hayo akiwa Ikulu baada ya kupata taarifa ya mradi wa gesi kutoka kwa Meneja wa Statoil nchini Tanzania, Oystein Michelsen, ambaye alisema itachukua miaka mitano kufikia uamuzi wa kuwekeza (final investment decision).

Wengi walishangaa na ucheleweshaji huo lakini mambo yanavyokwenda inaonekana itakuwa hivyo.

Tokea mwanzo ilionekana kutokubaliana na kiu na ari ya kuwekeza kwa pande hizo mbili ambapo wakati Magufuli anataka mradi uende haraka, Statoil kwa niaba ya wadau wawekezaji hawana haraka na kuonekana kusubiri hali fulani ya soko la mafuta au biashara ya gesi na hivyo ndivyo itakavyokuwa mpaka gesi tuiuze kwa bei ya kutupa kutokana na njaa ya fedha.

Rais alifikiri kuwa ni maofisa wa Serikali ni kikwazo lakini sasa iko wazi kuwa kampuni za mafuta ndio tatizo.

Profesa Justin Ntalikwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ambaye amesema kwenye vyombo vya habari kuwa timu ya wataalamu wa Serikali wako kwenye majadiliano na kampuni za mafuta hizo tano kujenga Mtambo huo wa LNG.

Katibu Mkuu huyo alisema chini ya HGA pande hizo mbili watatengeneza miundo ya kifedha ambayo itaamua namna gani bei ya gesi itakavyopangwa, masuala ya ardhi na mengine yanayohusiana nayo.

Mambo yaliyopo mezani ni pamoja na kampuni hizo kutaka sheria mahususi itakayotumika katika mradi huu kabambe na kudai HGA iwe sehemu ya hiyo sheria.

Prof. Ntalikwa anasema katika majadiliano hayo yataamua kutumia sheria zilizopo za gesi na mafuta au kutunga mpya na hasa ikizingatiwa kuwa kutaka sheria mpya kunaweza kuhitaji mwaka mmoja zaidi ili kuipata.

Anasema majadiliano ya aina hii huchukua muda mrefu na inaweza kuchukua zaidi ya miaka mitatu kuanzia mwaka jana (2016).

Baada ya hapo kampuni hizo zitaunda timu ya usanifu wa mbele wa mradi yaani Front End Engineering Design (FEED), ni usanifu wa msingi baada ya usanifu wa awali (Conceptual design) au Feasibility Study na FEED design inajizatiti juu ya usanifu wa kifundi (Technical Design) na kutolewa makisio ya gharama ya mradi kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho wa uwekezaji (Financial Investment Decision (FID).

Hayo ni majumuisho na uamuzi wa mwisho kuhusu uwekezaji wa mtaji (Capital Investment Decision) CID ikiwa ni sehemu ya matumizi ya muda mrefu wa shirika katika vianishi vya namna ya kutawala na kuendesha rasilimali za kampuni na muundo wa mtaji.

Prof. Ntalikwa anasema ana imani itakapofikia mwaka 2020 mradi utafikia michoro ya msanifu majengo na kila kitu kitakamilika ifikapo mwaka 2029.

Uko hapo? Anasema ni safari ndefu lakini hakuna jinsi ya kufanya.

Wananchi wanataka leo si kesho

Taarifa ya kuchelewa mradi imeleta sononeko kwa watu wengi kwa utafiti mdogo uliofanywa na Mtanzania, ambao walifikiri matatizo yao ya uchumi yamekwisha kwani Serikali ingepata uwezo mkubwa katika huduma za jamii ikiwa ni pamoja na elimu, afya, maendeleo ya miundombinu mbalimbali na ustawi wa maendeleo kwenye uchumi.

Kwa kifupi ni utajirisho ambao unaonekana sasa kucheleweshwa na kukubali kuzugwa na mahitaji ya wawekezaji na kutaka Serikali ifanye mazungumzo na wawekezaji wengine ili tupate maendeleo haraka kwani mwenye shibe hamjui mwenye njaa.

Wengi wanafikiri China inaweza ikaisaidia Tanzania vizuri zaidi kuliko hawa wengine kwani wana matatizo ya kisera na kimtazamo kwani wamezoea vya kunyonga na hivyo vya kuchinja hawaviwezi.

Ni kweli la kuvunda halina ubani, lakini kwa vigezo vya miradi kama hii sehemu nyingine ulimwenguni imechukua muda mfupi zaidi na hivyo ni vizuri kwa uongozi Petroleum Upstream Regulatory Authority (PURA) na Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) pamoja na wizara wakachukua hatua nyingine za ziada kuharakisha kwani suala hili linatawaliwa na siasa vile vile na hivyo linaweza kuvurugika.

Kule Ghana na Nigeria muda uliotumika toka uvumbuzi hadi kuuza gesi na mafuta ni chini ya miaka sita na hivyo kuna nafasi ya kujadiliana badala hiyo ya kwetu ya miaka 20, kuna haja ya Serikali kuchunguza kwa makini na undani zaidi.

Hatari za kisiasa (political risks) ni kubwa na zinaweza kuukwamisha mradi na kufanya ndoto ya Watanzania ikaishia kuwa ndoto. Ni lawama tupu!

Mengineyo

Gesi ya Tanzania kiwango chake kimefikia ujazo wa futi mraba trilioni 57.27 na wawekezaji ni hao watano ambao wameainishwa hapo awali.

Timu hiyo ya majadiliano itajadili faida kwa Tanzania katika kile kinachoitwa maudhui ya nyumbani (local content) masoko ya gesi na maamuzi kwa kiasi gani kitauzwa nyumbani na kiasi kipi kitauzwa nje na nani ili kulipia madeni ya utafutaji na uendelezaji.

Wazo la jumla ni kujenga Mtambo wa LNG wa nchi kavu karibuni kilomita 120 kutoka baharini na makisio ya awali ni gharama ya dola bilioni 30 sawa na shilingi trilioni 65 katika ardhi ya hekta 20,000 ambapo 18,000 zitakuwa kwa viwanda na hekta 2,000 kwa Mtambo wa LNG pale Likong’o Lindi.

Mtaalamu alonga

Neema Lugangira ni mtaalamu wa Kujitegemea wa Masuala ya Maudhui (Local Content) anayeishauri Serikali katika Ofisi ya Waziri Mkuu nini cha kufanya kuhusu suala la gesi na ujenzi wa Mtambo wa LNG na anasema kuna haja ya kuyaelewa baadhi ya mambo ambayo kwasasa ni nyeti lakini ni muhimu watu kuwa nayo kichwani ili yasije yakapotoshwa na wajanja na kuleta purukushani katika jamii. Ni rahisi kutoeleweka katika masuala hayo ambayo yana mahitaji tata na yanayokinzana toka sehemu nyingi za uchumi.

Anasema Serikali imechagua kuwa na mtambo nchi kavu wa LNG badala ya baharini ili kuhakikisha kuwa Tanzania inafaidika vilivyo kwa kuona inashiriki katika shughuli za mwenendo wa mtambo kwa urahisi zaidi. Nchi ya Msumbiji kwa kufananisha, imeamua kuwa na mitambo yote miwili ya kuelea (floating plant) na ule wa nchi kavu (onshore plant) kuvuna rasilimali yake inayokadiriwa kufikia futi za mraba trilioni 185 mara tatu ya hazina ya Tanzania.

Anasisitiza kuwa ni muhimu kwa Tanzania na wananchi wake kushiriki kikamilifu na kuvuna faida ya shughuli hizo za uchumi wa gesi na zinazoendana nazo.

Mtaalamu huyo ambaye ndio mwasisi wa kitengo cha maudhui ya nchi (local content) ofisi ya Waziri Mkuu anasema Mtambo wa Baharini hautoi fursa nzuri ya kushiriki kwa ukamilifu kwa kampuni zetu za nyumbani.

Kutokana na Msumbiji kuwa na mpango wa mtambo wa kiboya (floating plant), wao watatutangulia kuwa na LNG plant na hivyo watakamata mwanzo masoko.

Neema anaupongeza msimamo thabiti wa Tanzania lakini wawekezaji hawautaki kwani unapunguza kula yao na kuchelewesha kulipa deni la ujenzi wa mtambo na hivyo ni shubiri kwao.

“Tanzania inakusudia kulinda masilahi ya nchi na hivyo kusisitiza kuwa asilimia 10 ya gesi iwe ni kwa matumizi ya soko la nyumbani pekee bila kujali inatumika au hapana,” alidokeza Neema.

Anasema nchi lazima iweke kikomo cha chini cha kutumika na kubaki nyumbani vinginenvyo wawekezaji watapenda kuondoka na kila kitu na kusafirisha nje na kuwaacha mtupu ndani ya nchi. Hata tukiagiza gesi nje tutahitaji LNG Plant kwani gesi ni chanzo rahisi cha kuzalisha umeme kwa matumizi ya viwanda, uzalishaji viwandani na kwa usafiri wa magari. Ni mradi wa kudumu kwa miaka 40 ijayo.

Kuzingatia mambo yake yaende kama ilivyopangwa Tanzania ina Mpango Kabambe wa Matumizi ya Gesi yaani National Gas Use Master Plan (NGUMP) ambao kazi zake ni pamoja na kutoa mwongozo na dira ya matumizi ya gesi asilia nchini.

Matokeo chanya ya shughuli ya gesi itawezekana kupatikana kwa mapana tu kama nchi itajizatiti kwenye maudhui ya nyumbani ambayo italeta uwezo wa kupata ziada ya kuwekeza na kushiriki kwenye shughuli za gesi na hivyo kuongeza uwezo wa uchumi kufanya mengine yanayostahili.

Suala la ajira lipo tu wakati wa ujenzi wa LNG plant, lakini ajira itanywea wakati ujenzi ukikamilika na uendeshaji wa kiwanda kuwa wa kitaalamu zaidi ambapo watu wachache wenye ujuzi stahiki nchini wataajiriwa na wageni ndio watatawala kiajira kutokana na ujuzi wao maalumu.
 
Ungeweka kwenye PDF file
 
Kumbe kila "mbabe" ana "mbabe" wake. Mi nilidhani ukishakuwa na majeshi, mapolisi na uwezo wa kutoa matamko na kamandi, basi hakuna kitakachokupa shida. Kumbe mbabe wa kweli ni mwenye Trioni 65! Mungu tuonee huruma. Dunia siyo rafiki kabisa wa binaadam, tunalazimisha tu.
 
Sasa hapa naanza kuona baadhi ya wana siasa kuwa walikaa kimya wakijuwa.kuna sehemu tutakwama
 
Hawata fanikiwa na hawawezi kufanikiwa. Tatizo Tanzania inataka kutumia gas kama njia moja tu ya kujikwamua na umasikini. Ukiangalia bei ya gas ya Tanzania kwa sasa na bei ya dunia ni tofauti kabisa na wala haiakisi uwezekano wa kiwa na hayo maviwanda. Tuna hitaji investment plan. Inasemekana mpaka sasa bei ya gas Tanzania ni around 5.2us $/mmbtu akati average world natural gas price ni 3.5US $/MMBTU.

Nimejaribu ata ku google tanzania natural gas price kwenye website ya EWURA na TPDC haipo. Hivi kumbe haya mambo ni siri?????. Kwanini hawaweki wazi ili kila mtanzania aweze kuona. NaKwanini hayo makampuni yasiwekeze kwenye bei rahisi. Na unaweza kuta hiyo bei ni bila ya kodi. Ukijumlisha na kodi ndo kabisaaa.

Tanzania sasa hivi inatakiwa kuendeshwa kama kampuni ni sio kisiasa. Mfano, gharama za umeme ziko juu. Kwanini wasitafute mbadala wa kuzalisha umeme. Kitendo cha gharama ya umeme kuwa juu kinafanya uwekezaji kuwa magumu kwasababubu mtu unahitaji gharama kubwa kuendesha biashara yako na mwisho wasiku unaishia kupata hasara.

TANZANIA InatakIWA KUJIPANGA KWANZA KABLA YA KUFIKILIA MIRADI MIKUBWA KWANI ILIYOPO MPAKA SASA INAYUMBA YUMBA NA HiI NI KUTOKANA NA KUCHANGANYA MAMBO YA SIASA NA KIUTENDAJI
Bei ya natural gas

5 Year Natural Gas Prices and Price Charts

Au angalia hapa
Quandl
 
Kutokana na Msumbiji kuwa na mpango wa mtambo wa kiboya (floating plant), wao watatutangulia kuwa na LNG plant na hivyo watakamata mwanzo masoko.
Nimeipenda sana hii sehemu! Nimeipenda sana hii sehemu kwa sababu, sekta ya gas ni moja ya sekta ambayo nimekuwa nikiifuatilia sana tena tangia mwanzo!!!

Hayo yaliyosemwa mimi binafsi hayanishangazi hata kidogo kwa sababu, hata ile Sheria ya Mafuta na Gesi pamoja na Sheria ya Mapato ya Mafuta na Gesi ambayo ilipitishwa kwa haraka haraka bungeni mwaka 2015 niliifuatilia vizuri sana tena sana!!!

JF kuna wasomi wengi sana lakini majority sio wafuatiliaji wa mambo bali wanapenda kuongea lugha za wanasiasa! Kama mwana-JF ni CHADEMA basi ataongea kile ambacho Mnyika au Tundu Lissu ameongea badala ya kutafuta ukweli mwenyewe! Na kama mwana-JF atakuwa CCM basi ataongea lugha za akina Nape na JPM! Very shame!!!!

Moja ya mambo ambayo nilimpongeza sana JK ni kulazimisha ile sheria kupitishwa kabla hajaondoka! Kwavile watu sio wafuatiliaji wa mambo; wakadanganyika na maneno ya wanasiasa kwamba kwanini JK analazimisha kupitishwa hii sheria... lazima atakuwa na maslahi binafsi!!!!

Nilisoma miswada yote 3 na nikasema wazi kwamba, endapo hizi sheria zitapitishwa na bunge na hatimae tukawa na uongozi wenye uadilifu; basi gas itakuwa ndio msingi wa uchumi wetu! Ilikuwa ukiangalia sheria zote; zilikuwa zimeangalia sana maslahi ya taifa kuliko watu walivyokuwa wanaaminishwa na wanasiasa!

Na ndio maana leo hii sishangai hata kidogo nikisikia wawekezaji wanailetea figisufigisu ile sheria! Sheria imeiangalia sana Tanzania badala ya wawekezaji... ambacho kilibaki ni tu kuwa na viongozi wenye uadilifu kuitekeleza!!

Kwanini nilimpongeza sanaa JK?

JK hakuwa na uhakika nani angeingia madarakani 2015...! Kwa maoni yangu; aliamini hata Lowassa alikuwa na nafasi ya kushika Ikulu!!!

Inawezekana Lowassa sio fisadi kiasi hicho lakini watu waliomzunguka Lowassa ni monsters! Binafsi sikumuunga mkono Lowassa kutokana na tuhuma zake za ufisadi! Lakini ufisadi ambao niliuogopa zaidi sio wa Lowassa mwenyewe bali wa watu waliomzunguka Lowassa!

Ufisadi wa Lowassa ni ufisadi wa karibu kila kiongozi wa Tanzania! Hatuna kiongozi msafi wa kisiasa... labda kama hawa walioingia kwenye siasa hivi karibuni! Lakini hawa walio kwenye siasa for takribani 20 years now; MAJORITY KAMA SIO WOTE NI MAFISADI sawa na huyo Lowassa mwenye hiyo Brand Name!

Lakini ilikuwa kila nikimfirikia mtu kama Rostam Aziz mwenye ukaribu sana na Lowassa; nikawa namuogopa zaidi Lowassa kuliko mtu mwingine yeyote! Nikawa namuogopa sana Lowassa kwa sababu nafahamu Rostam Aziz ana interest kwenye uwekezaji wa gas!

Ilikuwa kila nikimwangalia mtu kama Kalamagi na Chenge... hawa watu wakawa wananifanya nizidi kumuogopa Lowassa kuliko Lowassa mwenyewe!!!!

JK aliamini endapo sheria isingepitishwa mwaka 2015 basi huenda isingepita tena!!!!! And trust me, it's a matter of time; msishangae mkisikia inabadilishwa!!!! Na mkija kuambiwa inabadilishwa kwa ajili ya maslahi ya taifa, fahamuni mtakuwa mmedanganywa na kwavile watu sio wafuatiliaji; WATAAMINI! Mkisikia imebadilishwa basi ni kuwa-favor wawekezaji
Kutokana na Msumbiji kuwa na mpango wa mtambo wa kiboya (floating plant), wao watatutangulia kuwa na LNG plant na hivyo watakamata mwanzo masoko.
Moja ya vipengle ambavyo nilivijadili sana wakati ule ni hicho hapo juu! Wana-JF wengi bado wana fikra za kijamaa!!!

Wengi ilikuwa utawasikia "...haraka yote ya nini; kwani gas inaoza!" Eti wakijifanya Mwalimu Nyerere aliyekuwa anasema madini hayaozi; haraka yote ya nini!!! Karne ya 21 bado watu wanaongea kaulimbiu za karne ya 20!!!!!

Watu tukajaribu kueleza hapa don't act as if hiyo gas mnayo peke yenu! Msumbiji nao wana gas na mataifa mengi hivi sasa yanagundua gas! Kwahiyo ikiwa hakuna sababu ya msingi ya kutuchelewesha basi hatutakiwi kuchelewa kwa sababu the sooner we enter the market, ndipo tunakuwa na chance kubwa ya kushika soko or else, tutalazimika kutumia nguvu kubwa kuiba soko!
 
Duuu kumbe kuna mengi nyuma ya pazia haya leta bisi niendelee na muhongo na hii gas yake kila hotuba lazima ataje gas miaka 5 ijayo mpka tuanze kuuza lazima soko litakuwa chini majirani zetu watakuwa washatupiga gap nao gas wanayo na ni mpambano wa soko na faida
 
Tumeshikwa pabaya,inatubidi tuziangalie upya sheria zetu za uwekezaji.ili wachina ambao hawana longo longo wanununue miradi hii.
 
Kwani tuakiachana na hayo makampuni na tukaangalia mengine itakuwaje?
 
TRILLIONI 65 KITU BWANA, magu achana na Dreamliner... TRA kamueni watu ndani ya Mwaka 2017 zipatikane haraka trilioni 65. halafu mnamfuata mchina au Mrusi tuna trilioni 65 tunataka utujengee LNG plant.. very simpleeee kabisa..

TAIFA LIACHE MAWAZO YA KIMASIKINI, MAGU TAFUTA 65 TRILLIONI HARAKA ITUPE PALE TUPIGE HELA...
 
Labda aanzishe kodi ya kichwa. Full stop!
 
TRILLIONI 65 KITU BWANA, magu achana na Dreamliner... TRA kamueni watu ndani ya Mwaka 2017 zipatikane haraka trilioni 65. halafu mnamfuata mchina au Mrusi tuna trilioni 65 tunataka utujengee LNG plant.. very simpleeee kabisa..

TAIFA LIACHE MAWAZO YA KIMASIKINI, MAGU TAFUTA 65 TRILLIONI HARAKA ITUPE PALE TUPIGE HELA...
kwa hsya makusanyo ya sasa si itachukua miaka zaidi ya mitano...
 
Watu waache kujadili kitu wasichokijua. Cha kwanza mchopasa kukijua uliki wa hivyo visima vya gesi ukoje, je mchina anayo nafasi ya kupewa na serikali hivyo visima? Ukweli uko hivi, mkataba wa umiliki wa ges iliyogunduliwa na inayoyoendelea kugunduliwa ni mkataba wa kugawana mavuno na anayemiliki asilimia nyingi ndiye anasimamia uendeshaji.
Mkataba huu kwa kimombo unaitwa Production Sharing Agreement (PSA) kwa visima vya Msimbati ushiriki upo hivi; kampuni ya M&P wanamiliki 49.5%, kampuni ya Wentworth 30.5% na TPDC kwa niaba ya serikali ya 20%. Umeliki wa kampuni hizo unatokana na uwekezaji katika kitalu husika.

Kumbuka wanachogawana hapa ni mavuno. Kwa upande wa serikali mapato makuwa yangekuwa kwenye mrahaba iwapo kama mkataba ungekuwa kama ilivyo mikataba mingine duniani kunakochimbwa rasilmali hizi za asili. Mkataba wetu na makampuni haya mrahaba (loyalty) inatakiwa ulipwe na TPDS hivi ndivyo mkataba unavyosema. Kwa mujibu wa mkataba huu mrahaba in 12.5% ambayo pia ndiyo inatumika sana duniani kote. Ukokotoaji wa mrahaba ni: Uzalishaji kwa mwezi x Bei x 12.5%. Mrabaha hutozwa kabla kampuni iliyowekeza haijaondoa gharama zake zote za uwekezaji. Baada ya hapo ndiyo kampuni ina ondoa gharama zake kisha faida hutozwa kodi na serikali.

Bei ya gas ya Msimbati: inayofua umeme wa Mtwara Tanesco wanauziwa kwa USD 5.35/mmBTU na kwa inayokuja kinyerezi serikali wanainunua kwa USD 3.00/mmBTU kwa mujibu wa mkataba wa mauziano kati ya TPDC na M&P na Wentworth. Naomba kuwasilisha wadau.
 
Back
Top Bottom