Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Wale watalii ambao ni wakunga kutoka Marekani, walikuwa wamechelewa safari yao kwa muda wa saa moja. Kumbe Mwenyezi Mungu alikuwa na sababu zake maalum za kuwakutanisha na tukio la ajali ili waweze kufanya jambo la upendo mkubwa.
Wakashuka kutoka kwenye gari la watalii na kuingia kazini katika kusaidia kuokoa miili ya watoto na waalimu wao. Picha zinaonyesha sura za huzuni kubwa walizokuwa nazo wakunga wale wakati wakiwa kwenye mchakato wa uokoaji.
La kutokea limetokea, wamezikwa watoto na waalimu wawili na dereva mmoja. Huzuni ikatawala shughuli zote za maziko. Maisha ni ya kuendelea kama kawaida kwani vitabu vya dini vinatuambia kuwa kila nafsi itaonja mauti.
Kuna somo la wema ambalo sisi watanzania tunapaswa kulichukua na kulifanya sehemu ya maisha yetu. Wazungu wale wangeweza kuambiana au kumwambia dereva aahh hebu tuendelee na safari haya hayatuhusu. Lakini ni moyo wa upendo ndio uliokuwa chanzo cha wao kuwa sehemu ya waokoaji siku ile ya ajali ya Rhotia Karatu.
Vitabu vya dini vinasema amebarikiwa yule atoaye kuliko yule apokeaye. Ndege ikaja Tanzania tena maalum kwa malaika watatu na Mama zao wazazi. Ili mradi tu watoto wale waweze kupata matibabu ya kiwango cha juu ili siku zijazo waweze kutoa mchango katika maisha haya.
Utayari wa wazungu na binadamu wengine katika kutoa msaada wa hali na mali, siku zote huwa ni chanzo cha Baraka za Mungu. Haiwezekani Muumba akamuacha mja wake hivi hivi tu pale anapokuwa tayari katika utoaji wa aina yoyote ile.
Watanzania mara nyingi tunapenda kujiona kama vile tunachopewa na mtu fulani au taasisi ni haki yetu, tunapindisha midomo na kuwa na sura zenye kiburi pasipo kufahamu kwamba Baraka za kweli zinakwenda kwa mtoaji na sio sisi wapokeaji.
Ajali ya kule Karatu itufundishe kwamba ipo siri ya mtoaji kupata mema mengi maishani, kuliko yule anayekimbia kuhusianisha matukio mbalimbali na masuala ya kishirikina na kishetani.
Wazungu pamoja na dhambi zao nyingi tu lakini wanao ule moyo wa utoaji. Tujiulize kwa undani, kwani Mungu asiwabariki wale wakunga watatu na serikali ya Marekani kwa kutoa ushirikiano katika kuwatibu majeruhi watatu?
Kwanini watoto na wajukuu wa wakunga wale wasijekuwa watu muhimu katika kipindi cha uhai wao?. Baraka zipo zaidi kwa mtoaji kuliko mpokeaji, na hili liwe ni jambo lenye kuhitaji tafakuri ya kina.