Wazungu Mgodi wa Tulawaka na vibali FEKI, worth mamilion kwa serikali

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,537
6,458
kuna jamaa kanipigia simu leo hii kutoka Biharamuro huko kagera, anasema kuna wafanyakazi wanne wa immigration hapo mjini kwao, wamekamatwa kufunguliwa kesi mahakamani kwa kosa la kuwapatia vibali feki wawekezaji wa kizungu mgodi wa Tulawaka wa Barick, vibali ambavyo selikali ingepata milion zaidi ya hamsini, lakini watu hawa waliziweka pesa hizo mifukoni mwao na kutoa vibali visivyo tambulika na uhamiaji. issue hiyo nasikia ilikuwa kubwa sana kwasababu hapo mjini hao jamaa walikuwa maarufu sana, hasa kwa kuchukua mademu na kutembelea magari mazuri. kama kuna waandishi wa habari kutoka huko, tunaomba updates na kesi imeendeleaje. idara ya uhamiaji imeoza. wazungu hao wamekaa hapa kwa muda, walikuwa wakiingia na kutoka kupitia boda zetu bila shaka, vipi hawakukamatika hadi leo hii? au kuna mtandao wa ufisadi uhamiaji?
 
na mvunja mwananchi ni nani? hili ni shamba la bibi hata hivyo....wanyonge watabaki kuwa wanyonge, wajanja watabaki kuwa wajanja, wenye nafasi wataendelea kuvuna shamba la bibi, wasio na nafasi/ajira wataendelea kutoa macho tu. kweli hii ni bongo, dili za kifisadi kama nigeria.
 
sasa nategemea na wazungu wenyewe watapelekwa mahakamani.
 
kuna jamaa kanipigia simu leo hii kutoka Biharamuro huko kagera, anasema kuna wafanyakazi wanne wa immigration hapo mjini kwao, wamekamatwa kufunguliwa kesi mahakamani kwa kosa la kuwapatia vibali feki wawekezaji wa kizungu mgodi wa Tulawaka wa Barick, vibali ambavyo selikali ingepata milion zaidi ya hamsini, lakini watu hawa waliziweka pesa hizo mifukoni mwao na kutoa vibali visivyo tambulika na uhamiaji. issue hiyo nasikia ilikuwa kubwa sana kwasababu hapo mjini hao jamaa walikuwa maarufu sana, hasa kwa kuchukua mademu na kutembelea magari mazuri. kama kuna waandishi wa habari kutoka huko, tunaomba updates na kesi imeendeleaje. idara ya uhamiaji imeoza. wazungu hao wamekaa hapa kwa muda, walikuwa wakiingia na kutoka kupitia boda zetu bila shaka, vipi hawakukamatika hadi leo hii? au kuna mtandao wa ufisadi uhamiaji?

Na vipi hao wazungu waliofaidi hivyo vibali feki, watazidi kutusumbua migodini au nao wamepandishwa, nadhani ni kosa kutoa na kupokea rushwa kwa maana hiyo sioni sababu ya kuwaacha hao wenye ngozi nyeupe sababu wanajulikana
 
nimecomfirm kabisa, ni kweli jamaa wamepandishwa kizimbani, walitoa vibali feki, na badala ya zile hela kuingia kwenye ofisi ya uhamiaji, zimeingia zote kwenye mifuko yao. immigration nao kumeoza.
 
Hongera zao bse 50mil kwa Tz ya sasa sio kitu as watu wanakwiba kuanzia Billion.
Ila kosa walilofanya ni kula wake na vidosho vya wenzao apo tuu ndo walipoharibu.
 
kwahiyo, 50mln iliyotakakiwa kuingizwa kwenye serikali, unafurahia kuwa ilihujumiwa? wewe pia yawezekana ni fisadi.
 
Naomba pia wachunguzwe wale wanaokuja kama wako field zisizo na ukomo.
 
watachunguzwa wapi ndugu yangu. watu tunaabudu wazungu kiasi hiki? au huwajui watz?
 
Yani bongo ishakua dampo la kila kitu yani vitu fake vmetuathiri mpaka basa mikataba fake,bidhaa fake, vibali fake, vyeti fake, ushhhh
 
Back
Top Bottom