Wazungu matapeli wa M-Pesa!

lolyz

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
339
199
Kuna wazungu wameonekana siku ya jana mitaani wakitembelea maduka yanayotoa huduma za M-Pesa wanadai wao wametoka makao makuu.Wakifika wanauliza una float kiasi gani kwenye akaunti yako,majina ,na namba za simu kitu ambacho ikiwa yeye ametoka makao makuu ni lazima akicheck namba yako anaweza kuona salio.Wanatumia simu za Blackberry kama data input yao -Tahadhari kwa walioachwa kwenye maduka wasibabaike kisa ni wazungu - wamevaa t-shirt za Vodacom ila hawaji na gari la kiofisi,naskia kuna namna wakijua salio lako ni rahisi kukuibia??????
 
Dah!! Maisha magumu kwa kweli, kila siku watu wanaibuka na mbinu za ajabu za wizi.
 
Mimi nawalaumu Uhamiaji kwa kuruhusu Wageni kuj a kwa wingi kwa kutumia Jina la Uuwekezaji

Idadi kubwa ya wazungu wanao kuja bongo ni vichaa,ila wabongo tulivyokiuwa washamba na waoga,mtu akimuona mzungu anashangaa shana kumbe wengine ni vichaa huko kwao wanaletwa bongo.
 
Mimi nawalaumu Uhamiaji kwa kuruhusu Wageni kuj a kwa wingi kwa kutumia Jina la Uuwekezaji
Ni kweli kabisa.Mfano kuna wazungu fulani wapo Ifakara eti wanachimba visima vya maji nao wanjiita MSABI mpaka TBL imewapa mil 80 kwa ajili ya visima Ifakara .Wanachofanya ni wizi mtupu hipo pump wanatoa TANIRA wanamodify kidogo then unapigwa mil 1 mpaka 3 inatehema ni wapi.Kazi wanafanyishwa na WASWAHILI KWA UJILA KIDOGO SANA .MSABI water and sanitation NGO Tanzania
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom