Siyane
Member
- Dec 26, 2010
- 46
- 9
NATO, UN, na mambo yote ya umarekanimarekani wanawapenda sana watu wa Libya kuliko Wasyria, Wapalestina na Wasomalia. Hili linadhibitishwa na namna mamia ya watu wanavyouliwa katika nchi hizi sasa hasa huko Syria ambako kuna mwendelezo wa mazingira kama ya Libya. Cha ajabu ndani ya Syria ni vita kali baina ya serikali na raia ambapo serikali inatumia mabomu hasa katika mji wa Homs. Watoto, akina mama, n.k wanapoteza maisha kila uchapo. Haikuwa hivi kwa upande wa Libya lakini mwitikio wa umarekanimarekani ulikuwa wa kishindo. Huenda kwa kuwapenda sana Walibya kuliko binadamu mwingine, NATO, na umarekanimarekani wooote wana mpango wa kuigeuza Libya kuwa Switzerland of Africa.