Wazungu bwana, weacha tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazungu bwana, weacha tu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lekanjobe Kubinika, May 11, 2011.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka mwaka 1997, mama mmoja wa Norway kutoka chuo kikuu fulani alikuja Tanzania kufanya utafiti wake kwa ajili ya PhD ya social anthropology. Yule mama ni pande kidogo, kaenda juu urefu na anatembea kama dume. Alipofika Arusha alikuwa anaishi umasaini kwenye nyumba zao akikaa na wanawake wa kimasai kujifunza wanavyoishi. Akajinyakulia mwanume mmoja dereva wa Taxi pale mjini Arusha akamkodi ili amzungushe kwa usafiri vijijini.

  Alipokusanya data zake alirudi kwao chuoni. Pale chuoni kulikuwa na kawaida ya presentations kwa watafiti wote. Naye siku moja alipangiwa saa yake. Akaleta power point na aliandaa presentation yake hivyo akiwa amepiga picha nyingi nyingi sana. Title yake sasa, sidhani kama ni rahisi kwa mwanamke wa kiafrika kukichagua na kukitetea. Labda kwa kuwa kiliandikwa kwa kiingereza "The Vagina Can Not Be Cursed". Alionyesha picha hizo akitafsiri moja baada ya nyingine, zikibeba maelezo muhimu juu ya umuhimu wa title yake.

  Kwa ufupi tu, alieleza mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume, mazingira ya kutunga mimba, akitolea mfano kwamba mazingira ya kimasai ni magumu lakini kama mwanamke lazima kukubali wajibu kumtunza mzee wakati wowote na mahali popote ukiwa tayari au la, kuzaa na kulea watoto na shughuli zote afanyazo mwanamke wa kimasai. Akasema alikwenda na yule taxi driver kuwaonyesha wamasai kwamba mwanmke anaweza kuamua saa na mahali pa kumliwaza mzee. Alipojaribu role za kimasai akagoma ku-conceive na kuwaambia nao wamasai wanaweza kugoma.

  Aliulizwa madhara aliyoyafanya kwa familia ya dereva huyo kufanya vitu vyao kwa maonyesho akatetea kwamba ni sehemu ya burudani na alijitahidi kuwa karibu na mke wa dereva akimtimizia mahitaji yake yote na kumhakikishia kwamba hanyang'anywi mume ila ni biashara ndogo ya kimaisha. Pia akasema, alifaidika sana na mwanaume yule lakini alitii ahadi ya kutozaa naye, akisema mwanaume huyo naye alimpenda sana mamaa huyu kwa sababu, kwa maelezo yake, The vagina can not be cursed. Alisema mahusiano yao yalikuwa baina ya appliances zao na sio wao spiritually. Aliwaacha hoi wasikilizaji.

  Kila mara likija wazo la aibu za dada zetu waliofunzwa kimila, inakuja picha ya mama yule namuona akilini mwangu akipresent kwa jazba. Wanaume walibaki kuchekea mvunguni mwa meza zao tu, akawazidi kete na hatimaye thesis yake ikapita kiulaini. Is it opportunism? Ujasiri ule sijauona hata kwa mzungu mwingine, ila kwa hadithi zenye mitazamo tofauti japo nayo ni ya ajabu. lakini ajabu, ingawa aibu ipo sana kwetu Afrika, hatujali sana na kuheshimu matakwa yetu. Mwanamke ni nadra kumkuta anatafuta mwanaume wa urafiki naye waziwazi ila magonjwa ya zinaa kibao. Wazungu wako open minded katika masuala hayo lakini magonjwa ya zinaa kwao sio sana kama kwetu.

  Kumbe bora ukweli na uwazi kuliko soni na kificho????
   
 2. mariah leos

  mariah leos Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mh!!haya bhana.:happy:
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuna raha yake kukumbuka yaliyotokea nyuma. Experience is the best teacher ever.
   
 4. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  aisee na taxi dreva alitoa ushuhuda gani?
   
Loading...