Wazuia ununuzi wa 'shangingi' la Mkurungenzi Mtendaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazuia ununuzi wa 'shangingi' la Mkurungenzi Mtendaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Jan 15, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  BARAZA la Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro limzuia ununuzi wa gari la Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo ili fedha zilizotakiwa kutumika zifanye kazi ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari za kata.


  Awali zidi ya Sh.105 milioni zilitengwa ili kununua gari la Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo.


  Lakini kuzuia ununuzi wa gari hilo kunafuatia upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo inasemekana asilimia 58.8 ya wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka jana watakosa nafasi za kuanza kidato cha kwanza kutokana na upungufu wa madarasa.


  Akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika juzi mjini Ifakara, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Hassan Goagoa, alisema ni aibu kwa wilaya hiyo kufaulisha wanafunzi 7,462 na kati yao wanafunzi 3064 tu ndiyo waliopata nafasi wakati wanafunzi 4,398 wanakosa nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.


  Kutokana na hali hiyo halmashauri ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro imeweka mikakati mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka jana wanajiunga kidato cha kwanza.


  Mwenyekiti huyo alitaja mikakati mingine ya kupata fedha za dharura kuwa ni kusimamisha ujenzi wa awamu ya pili ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri,kuchukua fedha za faini za mifugo wanazotozwa wafugaji walioingiza mifugo wilayani humo, fedha kutoka mfuko wa elimu na kukusanya michango ya elimu kutoka kwa wananchi ambao hawakutoa.


  Alisema kama mikakati hiyo ikitimia halmashauri hiyo inauwezo wa kukusanya kiasi kikubwa cha fedha kutokana na upungufu uliopo hivi sasa wa madarasa 98 yenye thamani

  ya shilingi milioni 362,088,000.


  Awali mkuu wa wilaya ya Kilombero Evarist Ndikilo alisema wilaya inabidi iandae mkakati maalum ili wanafunzi wote 7,462 ambao ni sawa na asilimia 72.24 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani wanaingia kidato cha kwanza mwaka huu ambapo ufaulu huo ni

  ongezeko la asilimia 11.14 ikilinganisha na kiwango cha ufaulu cha mwaka jana.


  Goagoa alisema mikakati hiyo itaenda sawa na agizo la Rais la kutaka wanafunzi wote waliofaulu kuingia madarasani hivyo wilaya inahitaji kufanya juhudi binafsi ili wanafunzi wote waingie kidato cha kwanza.


  Sambamba na hali hiyo, Baraza hilo lilimtaka Ofisa elimu wa mkoa kuruhusu watendaji wa idara ya elimu katika wilaya hiyo kuweka hadharani majina ya wanafunzi wote waliofaulu ili wanafunzi hao wapate muda wa kujiandaa tofauti na hivi sasa ambapo wengine wamekwisha kata tamaa.


  Walisema kufichwa kwa majina ya wanafunzi hao, ni sawa na kuwanyima haki na kwamba lazima yatangazwe ili kuwapa hamasa wazazi wao kujiandaa na pia kuchangia michango mbalimbali ya maendeleo.


  Tatizo hilo, limekuja baada ya Ofisa elimu mkoa kuzuia majina ya baadhi ya wanafunzi waliofaulu hakitaka baadhi ya kata zisizomalizia majengo ya shule za sekondari kukamilisha ili majina hayo yatangazwe jambo ambalo wananchi wanamlalamikia.
  Source: Mwananchi  Kumbe madiwani wakati mwingine wanaweza kutoa maamuzi ya busara.
  Hivi kama madiwani wote wa halmashauri zote Tanzania bara wakiamua kufanyakazi kwa kuweka mbele maslahi ya wananchi kama hawa wa Kilombero Mkoani Morogoro tungejengewa shule na mtoto wa miaka 17 ?.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,600
  Trophy Points: 280
  Nawapongeza sana hao madiwani najua kuwa hy kigogo wa halmashauri anachukua tu gari lolote hapo ofisini si kwamba atakuwa anakosa kabsa usafiri....wakajenge hayo madarasa na wakomae sana kupaata walimu kufundisha hao wanaliofaulu la sivyo itakuwa mbuzi kula mkeka......
   
Loading...