Wazoefu wa kuuguza mgonjwa wa HIV+ naombeni ABC..

Prince Of Darkness

Senior Member
Feb 28, 2018
102
81
Salam wanajamvi, moja moja kwenye hoja. Nina bwana mdogo ni HIV+ kwa sasa ana miezi 3 tangu aanze kutumia dawa za arv, kwa upande wa afya anaendelea poa sana, coz kabla hajaanza dawa alidrop uzito mpaka kilo 38, lkn alivoanza dawa alianza ku-gain pole pole mpaka sasa ana kilo 62. Inshu sasa imekuja imekuja kichwani dishi limeyumba yaani anaropoka visivyoeleweka, mara anatoloka wakati mwingine anasusa kula na kuongea. Mwanzo niliambiwa hali hiyo ni kawaida itaisha baada ya wiki 3 au mwezi, cha ajabu mpaka sasa unaelekea mwezi wa nne dishi halijakaa sawa. Wadau nifanyeje Hali ya akili ya huyu dogo ikae sawa au haiwezekani ndo atakuwa wa hivi hivi jumla?
 
Mrudishe hospital apate tena ushauri na saha kutojikubali ndio tatizo kuu ndio kawaida mtu anapo kuwa kwenye gridi ya taifa ujiona maisha yake yana isha wakati wowote
😂😂😂 kumbe mkuu huwa unatoaga ushauri wa maana sometimes,kwahiyo sasa nimegundua yale mambo unayoandika humu kuwa wewe fundi huwa unazuga watu...
 
Mkuu wanakuwaga na semina semina kwenye clinic zao huko ambapo wanakutana wengi.

Pia wana michezo mbali mbali netball football nk..hiyo inasaidia kukutana na wenzake wenye hali kama yake.

Atakutana na shughuda za watu walioishi miaka mingi wakiwa wanatumia dawa, itamfanya ajione kwamba kuugua huo ugonjwa sio mwisho wa maisha Bali ni mwanzo wa maisha mapya ya kujipenda na kujikubali na kujali afya kwa kula vizuri nk.
Sijajua hili kama bado linaendelea ila jaribu kufuatilia mkuu.
 
Salam wanajamvi, moja moja kwenye hoja. Nina bwana mdogo ni HIV+ kwa sasa ana miezi 3 tangu aanze kutumia dawa za arv, kwa upande wa afya anaendelea poa sana, coz kabla hajaanza dawa alidrop uzito mpaka kilo 38, lkn alivoanza dawa alianza ku-gain pole pole mpaka sasa ana kilo 62. Inshu sasa imekuja imekuja kichwani dishi limeyumba yaani anaropoka visivyoeleweka, mara anatoloka wakati mwingine anasusa kula na kuongea. Mwanzo niliambiwa hali hiyo ni kawaida itaisha baada ya wiki 3 au mwezi, cha ajabu mpaka sasa unaelekea mwezi wa nne dishi halijakaa sawa. Wadau nifanyeje Hali ya akili ya huyu dogo ikae sawa au haiwezekani ndo atakuwa wa hivi hivi jumla?
Ukisema ni wewe kuna tatizo!?, hadi umsingizie ndugu yako!funguka tukushauri vizuri
 
Duh pole sana ndugu, jitahidi kumsisitiza kuhusu lishe na dawa azingatie baada ya muda atakuwa sawa tu.
Asante Sana, kuhusu lishe na dawa si tatizo kabisa kwa sababu namsimamia vizuri we fikiria uzito ulishuka hadi kilo 38 lkn kwa usamamizi mzuri wa lishe na dawa uzito umepanda hadi kilo 62
 
Pole sana kwa hali unayopitia mkuu. Nafikiri jaribu kwenda kwenye zile clinic zao wanaweza kutoa mwanga zaidi wa nini kifanyike. Hongera pia kwa kutomnyanyapaa.
CC
Sky Eclat
Pole sana kwa hali unayopitia mkuu. Nafikiri jaribu kwenda kwenye zile clinic zao wanaweza kutoa mwanga zaidi wa nini kifanyike. Hongera pia kwa kutomnyanyapaa.

CC
Sky Eclat
Asante clinic zao walisema hiyo hali ni kawaida itakoma baada ya wiki 3 lkn sasa zishapita inakimbilia mwezi wa nne sasa
 
Back
Top Bottom