Wazoefu wa Aliexpress mpitie hapa mtoe msaada wa haraka tafadhali

Hawa "cannaiao economy global" Wanachelewesha saanyingine mpaka miezi Miwili.

Na "cannaiao global for special goods" Hawa Wako Faster Kidogo tofauti na hao Economy, Hawa unaweza pata mpaka siku 14
Na "AliExpress Standard Shipping" Pia hawatofautiani sana na "cannaiao global for special goods"

Muhimu kuangalia Kampuni unayoitumia Kusafirisha, Nakushauri unaponunua kitu cha zaidi ya $10 usitumie Free Shipping, labda ikiwa ni ya Aliexpress Wenyewe, Ni bora ukachagua Shipping hata ya kulipia ambapo unaweza kulipia hata 2000 au 3000 au zaidi.
Boss tusaidie haya makampuni ya hizo bei ili sisi wajasiliamal wadogo tuweze watumia
 
Wakuu Habari ya nyie, nahitaji kuagiza simu aliexpress ila sio mzoefu sana, make nilipoagiza mara ya kwanza kwa ajili ya kupata uzoefu ndo nilibaki njia panda, niliagiza kitu cha dollar 1.5 tar 01/06 mpaka leo tar 20/07 inasoma departed country of origin shipping method cannaiao economy global, tar 05/06/ nliagiza saa ya dollar 3.5 shipping method cannaiao global for special goods ilichukua wiki 2 tu kunifikia.

Simu ninayohitaji kuagiza ni xiaomi redmi 8A 4GB RAM, 64GB internal, shipping method itakua aliexpress yenyewe ya bei nafuu, hivo wakuu mlowai agiza mnipe experience make naogopa kupigwa kama nlivopigwa na kikuu.

Kwa kikuu niliagiza simu ikaja na tatizo nkaomba refund wakanambia nirudishe simu, nikapeleka hela mpaka wa leo chenga tangu mwezi wa 5.

Link ya simu yenyewe hii hapa, 104.99US $ 26% OFF|Global ROM Xiaomi Redmi 8A 8 A 64GB ROM 4GB RAM Mobile Phone Snapdragon 439 Octa Core 6.22
Mimi nimeagiza toka July 1 Hadi Leo hakuna updates yeyote ya maana zaidi ya mzigo parcel left country of origin.

Kuna cargo company zinazingua saana.
 
Mimi nimeagiza toka July 1 Hadi Leo hakuna updates yeyote ya maana zaidi ya mzigo parcel left country of origin.

Kuna cargo company zinazingua saana.
Utafika, kuna kipindi parcel yangu ilikaa miezi mi3 lakini ilifika.
 
Wako Faster zaidi ya "cannaiao economy global" ndo mana unakuta wakati mwingine wana charge ada kidogo.
Kuna kampuni ambazo nasikitika sana siku hizi sizioni na hii ni kutokana na covid-30, yaani mizigo yangu ilikuwa lazima ifike tu.

(1) China Post Registered Air Mail
(2) China Post Ordinary Small Packet plus
(3) 4PX Singapore Post OM Pro

Pamoja na kwamba kuna wakati ilitokea mzigo kuchelewa ila delivery ilikuwa hakika labda tu seller awe mhuni. Yaani hata gharama za shipping zilikuwaga mayai sana.

Shenzi sana Covid-30

Sent from my cupboard using mug
 
kwanini mkuu usichukue redmi 9? utofauti mdogo wa bei ila redmi 9 ni simu kali sana kila idara.

kuhusu 8A na band inayo B3, B7 naq B40 ila haina B20 hivyo hutapata 4g tigo nje ya mji na smile.
Naunga mkono hoja redimi 9 nisimu bomba Kwa wenye vipato vya Kati
 
Kama una haraka na bidhaa husika, EPUKA kununua bidhaa ambayo ni Free Shipping!!!

Now, let's say umeona Saa X inauzwa $10 Free shipping, na umeona similar watch inayouzwa hiyo $10 but $2 Shipping, bora ununue hiyo ambayo utalipia shipping!!!
 
Back
Top Bottom