Wazo: Wana jm forum nasi tufanye party ya mwaka tufahamiane

Jamani wana JM forum kumbe nasi tunaweza tukafanya party yetu ya mwaka, members tukutane tufahamiane.
Jinsi party ya 8020 fashions ilivyofanikiwa hivi karibuni, itupe changamoto
Mnaonaje wakuu kuhusu hili?
sitaki kabisa hiyo hoja,yaani mnifahamu na siku mkinifahamu tu nabadilisha ID,ebu acheni huo mchezo kabisa
 
Hilo wazo poa sana. Ila tutatumia majina yetu halisi, hakuna kutambulishana kwa id za Jf. Mfano: habari, mimi naitwa Magamba Yameliwa, ni mwana chama wa Jf. Then, makofi pwaa.! pwaa.! pwaaa.! Pendekezeni Venue.
 
Suala la kukutana ni wazo zuri sana lakini tatizo na jinsi tulivyo sambaa,wanachama wa JF wako dunia nzima,sasa tutakutanaje?,na wengine tupo kwenye harakati januari hadi disemba,huo muda nitaupata wapi na itakuwa wapi na gharama za malazi na chakula itakuwaje?,kweli ni wazo zuri lakini ni gumu kutekelezeka...
 
1. Najiuliza kulikoni na tumekosa nini hata kujipa adhabu ya kujilinganisha na mtandao huo kiasi cha kuiga mfano wake.
2. Inamaana kila kitu kianzishwacho lazima kiji evaluate kwa sherehe?
3. Nini kitafuata baada ya kukutana huko? Kuanzisha DECI? Au UPATU?
Mimi nadhani hivi tulivyo tunatosha sana, wanaofahamiana waendelee kukutana, na wengine tutazidi kufahamiana tu kulingana matukio lakini si kwa style hii ya siku fulani na deadlines(sherehe na kalenda)

Kufahamiana maana ni kukutana kwa pamoja (na sio lazima wakati huo wewe kufuchua identity yako LOL, muhimu ni wewe ununue ticket na kuhudhuria function). Na katika party hiyo kutakuwa na shughuli nyinginezo muhimu kama vile kuchangisha pesa kwa kusudio fulani (fundraising) nk na baadaye makusanyo hayo yafanyike katika kusaidia jamii.
Unaju JF ina members wengi sana (waliopo ndani na nje ya nchi) na kama tukifanya shughuli kama hii na kufanikiwa itakuwa ni jambo la kusaidia jamii yetu kwa aina fulani. Nafahamu ingawa hapa tunachangamia mada ki anonymously, si haba wengi tuna nia njema kwa jamii yetu, na hivyo basi tufanye kitu fulani positive na isiwe Jamii forums za blah blah tu miaka yote
 
Ngoja hicho kikao ahudhurie al shabab mtakiona. Hamjui kuwa jf ni adui mkubwa wa ccm?
 
Kukutana hakuna ubaya kama lengo la kukutana litawekwa wazi. Lakini nashauri members wasijuane ID zao.Ingawa kwenye attendance book yaandikwe yale ya JF.Na pia wasizuiwe watakaotaka kujuana personally. Kikubwa lengo liwe na maana kwa Jamii, isiwe kufahamiana.Ahsante.
 
Suala la kukutana ni wazo zuri sana lakini tatizo na jinsi tulivyo sambaa,wanachama wa JF wako dunia nzima,sasa tutakutanaje?,na wengine tupo kwenye harakati januari hadi disemba,huo muda nitaupata wapi na itakuwa wapi na gharama za malazi na chakula itakuwaje?,kweli ni wazo zuri lakini ni gumu kutekelezeka...

Ndio wana JM forums tumesambaa dunia nzima, ila inaweza ikapangwa na matangazo yakatoka, na tukaamua kufanya hiyo get together jiji kuu dar es salaam. Miezi ya July, August wabeba mabox ughaibuni wengi huwa likizo bongo, basi ingekuwa wakati muafaka sana wa kufanya hili.
Kwa wale watakao safari kutoka nje ya dar, nadhani gharama za chakula etc litakuwa ni jukumu lako binafsi, ni suala la member kujipanga na kuhudhuria hilo tamasha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom