Wazo: Waliosomeshwa BURE enzi za mwalimu watafutwe popote walipo walipe

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,762
4,576
Jana tumeshuhudia orodha ndefu ya wadaiwa wa bodi ya mikopo.... Wengi wao ni vijana tena wapo ambao hawajaariwa lakini bodi imekomaa nao... Nadhani ili haki itendeke orodha hii iunganishwe na ile ya wale waliosomeshwa bure enzi za mwalimu kwani wengi wao wako kwenye ajira na hawakurudisha gharama walizotumia enzi hizo..... Naamini kati yao wapo wanaofanya kazi bodi sasa sijui wanajisikiaje kukomaa na madeni ya vijana wao wakati wenyewe walisoma bure______.ni wazo tuuu.
 
Kwani ukiajiriwa leo na makubaliano ya mshahara wa laki moja kwa mwezi na mwingine aliajiriwa mwaka uliopita kwa mshahara wa 80,000 kwa kazi ile ile. Yule wa mwaka jana anaweza kweli kulalamika amepunjwa 20,000.?
 
Acha Ukuda wewe.... watu tumeitumikia hii nchi kwa mishahara midogo sana mmeshakua mmekuta nch shwari sasa mnataka kuleta Machafuko nchini.... haya Kakojoe ulale...

Wapigania Uhuru wa Zimbabwe wampinga Mugabe... ni Dalili za kuchokwa ukizidisha ukuda wa kijinga... Mnajona mshaota Mapembe Sana
 
Tulia wewe.... Lipieni madeni yenu... Hakuna chabure
 
huchelewi kusema hata waliofariki ndugu zao walipe............ nani alikuambia Kulikuwa na mikopo enzi hizo..... sisi tulikuwa wachache kipindi kile UDSM ilikuwa moja tu...... sasa hivi ma UDSM kibaooo hakuna hela za kuwalipia.... halafu sisi tulikuwa na adabu hadi udsm tulikuwa tunachapwa viboko..na tunakomaaaa.... nyie tu hata ukiona mende chumbani unataka kuandamana.... acha hizo dogo imekula maharage ya wapi sijui
 
Tulilipa kwa kufanya kazi miaka miwilli na kukatwa mshahara kulipia bursary bila kubadirisha kazi. Kulikuwa na utaratibu mzuri usiokuwa na maumivu. Tatizo la sasa ni loan siyo bursary. Bursary wewe unasoma ukiwa na uhakika upo kwenye establishment ya kitaifa. Utaratibu huu ulikufa na Azimio la Zanzibar 1983/84 lililoingiza ajira holela zilizodhibitiwa na hadi sasa kudhbiitiwa na ofisi ya rais utumishi.

Zamani zetu zilidhibitiwa na Wizara ya Mipango iliyokuwa ya kitaalam zaidi kwa kupanga matumizi ya raslimali watu kulingana na mahiraji yote ya nguvu kazi ndani na nje ya serikali (Yaani mipango ya kitaifa) .

Sasa hivi ni Ikulu kudhibiti kila kitu hata mihimili mingine .
 
Bod wanajisumbua tu maelfu ya wahitimu wamegraduate no job watazilipaje hzo fedha bora wangetafta namna watumikie taifa. Hao waliosoma zamani ndo wamekula mema ya nchi na walikua wakimaliza tu ajira so ndo walikatwa huko
 
Tulilipa kwa kufanya kazi miaka miwilli na kukatwa mshahara kulipia bursary bila kubadirisha kazi. Kulikuwa na utaratibu mzuri usiokuwa na maumivu. Tatizo la sasa ni loan siyo bursary. Bursary wewe unasoma ukiwa na uhakika upo kwenye establishment ya kitaifa. Utaratibu huu ulikufa na Azimio la Zanzibar 1983/84 lililoingiza ajira holela zilizodhibitiwa na hadi sasa kudhbiitiwa na ofisi ya rais utumishi.

Zamani zetu zilidhibitiwa na Wizara ya Mipango iliyokuwa ya kitaalam zaidi kwa kupanga matumizi ya raslimali watu kulingana na mahiraji yote ya nguvu kazi ndani na nje ya serikali (Yaani mipango ya kitaifa) .

Sasa hivi ni Ikulu kudhibiti kila kitu hata mihimili mingine .
Nasisi watufanyie kama mlivyofanyiwa sio kutugeuza kuwa wahalifu na kutuaibisha.... Watupe miaka miwili ya kujitolea then yaishe vinginevyo hakuna usawa
 
Tukimaliza hili tuanze kuwalipa na wale walionyang'anywa nyumba na mashamba yao kwa neno la ujamaa na kujitegemea. Walioporwa biashara zao pia.
 
Nasisi watufanyie kama mlivyofanyiwa sio kutugeuza kuwa wahalifu na kutuaibisha.... Watupe miaka miwili ya kujitolea then yaishe vinginevyo hakuna usawa
Hili linakinufaisha chama dola kutoa rushwa na ahsante kwa watu wao . Naamini kikiingia chama mbadala hoja na uzoefu uliokuwa wa manufaa kama hili yatazingatiwa.
 
Bodi ingoje wale waliosoma zamani wastaafu kwanza kwa sababu ndio wamezishikilia ajira zote hadi sasa hivi
 
Jana tumeshuhudia orodha ndefu ya wadaiwa wa bodi ya mikopo.... Wengi wao ni vijana tena wapo ambao hawajaariwa lakini bodi imekomaa nao... Nadhani ili haki itendeke orodha hii iunganishwe na ile ya wale waliosomeshwa bure enzi za mwalimu kwani wengi wao wako kwenye ajira na hawakurudisha gharama walizotumia enzi hizo..... Naamini kati yao wapo wanaofanya kazi bodi sasa sijui wanajisikiaje kukomaa na madeni ya vijana wao wakati wenyewe walisoma bure______.ni wazo tuuu.
Tuko wengi sana na tuko tayari kulipa! kwa kweli sitamsahau mwalimu Nyerere. Utaratibu uanzishwa tutalipa!
 
Jana tumeshuhudia orodha ndefu ya wadaiwa wa bodi ya mikopo.... Wengi wao ni vijana tena wapo ambao hawajaariwa lakini bodi imekomaa nao... Nadhani ili haki itendeke orodha hii iunganishwe na ile ya wale waliosomeshwa bure enzi za mwalimu kwani wengi wao wako kwenye ajira na hawakurudisha gharama walizotumia enzi hizo..... Naamini kati yao wapo wanaofanya kazi bodi sasa sijui wanajisikiaje kukomaa na madeni ya vijana wao wakati wenyewe walisoma bure______.ni wazo tuuu.

Imekula kwako, haitakaa itokee, kila zama na kitabu chake. Nenda kalipe mkopo.
 
Hivi mnajua bodi huwa wanapiga penaiti kila mwaka kama hujalipa, nimeenda kuchukua statement yangu nimepigwa penalty 5% kila mwaka ambao sikulipa tangu nimalize chuo. But nimewambia sikuwa na kazi niwalipe nini sasa. Kama hujalipa nenda kachukue statement yako uone nchi ilivyo jamani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom