Wazo: Utamjua mtu kwa kundi la rafiki zake

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Mtu - Jakaya Mrisho Kikwete

Rafiki zake:

- Marehemu Ditopile Ukiwaona Mzuzuri (alijiuzulu baada ya kutuhumiwa mauaji)
- Edward Lowassa (alijiuzulu kutuhumiwa matumizi mabaya ya cheo)
- Rostam Aziz (kabanwa na Bunge kuhusu ufisadi)
- Andrew Chenge (kajiuzulu sababu ya ufisadi)
- Ibrahim Msabaha (kajiuzulu kutokana na matumizi mabaya ya cheo chake)
- Nazir Karamagi (kajiuzulu kutokana na matumizi mabaya ya cheo)
- Rashid Othman (kashindwa kuongoza Usalama wa Taifa)
- Robert Manumba (Kashindwa kuongoza idara ya upepelezi wa makosa ya jinai hadi Rais anaunda timu nyingine ya kuchunguza uhalifu)
- x,y (marafiki wengine ambao wataingia matatani miezi michache ijayo)

Conclusion:

Any.
 
That's why I said earlier that he doesn't pass the believability test when some people try to potray him as being clean....
 
Mtu - Jakaya Mrisho Kikwete

Rafiki zake:

- Marehemu Ditopile Ukiwaona Mzuzuri (alijiuzulu baada ya kutuhumiwa mauaji)
- Edward Lowassa (alijiuzulu kutuhumiwa matumizi mabaya ya cheo)
- Rostam Aziz (kabanwa na Bunge kuhusu ufisadi)
- Andrew Chenge (kajiuzulu sababu ya ufisadi)
- Ibrahim Msabaha (kajiuzulu kutokana na matumizi mabaya ya cheo chake)
- Nazir Karamagi (kajiuzulu kutokana na matumizi mabaya ya cheo)
- Rashid Othman (kashindwa kuongoza Usalama wa Taifa)
- Robert Manumba (Kashindwa kuongoza idara ya upepelezi wa makosa ya jinai hadi Rais anaunda timu nyingine ya kuchunguza uhalifu)
- x,y (marafiki wengine ambao wataingia matatani miezi michache ijayo)

Conclusion:

Any.

hii inaonyesha kuwa yeye ni one of them! Yup
 
Na zipo njia mbili kubwa za mtu kushinda uchaguzi. Moja ni kuhakikisha unakuwa mgombea wa chama chenye nguvu na mvuto, kama ilivyo CCM hivi sasa. Maana yake ni kuwa hata wewe mgombea ungekuwa hovyo kiasi gani, utabebwa na chama, na utachaguliwa kuwa diwani, mbunge au rais, kwa sababu tu ya chama. Njia nyingine na ya pili ni mgombea mwenyewe kuwa na sifa ambazo zinatosha kuvutia wananchi wampigie kura, sio chini ya kivuli cha chama chake.

Haya ni maneno mazito sana ya mheshimiwa Mkapa katika Hotuba yake , kwenye mkutano wa halmashauri kuu ya ccm, dodoma, 25 agosti 2004.Hii hotuba mpaka leo huwa siisahau.aliona mbali sana kuhusu hawa watu..tukiacha ubaya wake alioufanya.

Unaweza kuipata hapa kama watakuwa hawajaitoa. http://www.ccmtz.org/hotuba/040825nec.htm

 
Mtu - Jakaya Mrisho Kikwete

Rafiki zake:

- Marehemu Ditopile Ukiwaona Mzuzuri (alijiuzulu baada ya kutuhumiwa mauaji)
- Edward Lowassa (alijiuzulu kutuhumiwa matumizi mabaya ya cheo)
- Rostam Aziz (kabanwa na Bunge kuhusu ufisadi)
- Andrew Chenge (kajiuzulu sababu ya ufisadi)
- Ibrahim Msabaha (kajiuzulu kutokana na matumizi mabaya ya cheo chake)
- Nazir Karamagi (kajiuzulu kutokana na matumizi mabaya ya cheo)
- Rashid Othman (kashindwa kuongoza Usalama wa Taifa)
- Robert Manumba (Kashindwa kuongoza idara ya upepelezi wa makosa ya jinai hadi Rais anaunda timu nyingine ya kuchunguza uhalifu)
- x,y (marafiki wengine ambao wataingia matatani miezi michache ijayo)

Conclusion:

Any.

Mzee Mkjj,
Enzi zile niki/tukiangalia sinema za Bluce Lee na waigizaji wengine,antagonist anakuwa na kundi lake kubwa tu la maadui, mmoja baada ya mwingine wanapigana na protagonist na kushindwa mwishowe inakuwa ni zamu ya antagonist mwenyewe kupigana/kujilinda/kujinusuru. Mara zote protagonist anashinda.
Nadhani kinachoendelea sasa protagonistic power iliyomo katika umma ikiambatana na kufichuliwa kwa siri za mafisadi, inazidi kumwangusha adui mmoja baada ya mwingine na tunazidi kumkaribia huyo antagonist mwenyewe. JF haina budi kufacilitate hii advancing move ya protagonist.Tunapo pa kuanzia,kabla hajakalia kiti cha enzi,I quote...
Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.

Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.
 
Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika. [/I]

umekumbusha jambo moja ambalo nililisahau wiki iliyopita (na uzee huu naanza kusahau vingi)... mmojawapo wa wajumbe walioongozana na Kikwete kwenye ziara nchini Chini wiki ile iliyopita si mwingine bali mmoja wa watendaji wa Barrick Gold, Bw. Kahama ambaye kama JK na yeye ni swahiba mkubwa wa James Sinclair.
 
Does know one knows where the ownner of SAMAX Limited is,ni mtanzania..yupo hai kweli??

Connection the dot...
 
umekumbusha jambo moja ambalo nililisahau wiki iliyopita (na uzee huu naanza kusahau vingi)... mmojawapo wa wajumbe walioongozana na Kikwete kwenye ziara nchini Chini wiki ile iliyopita si mwingine bali mmoja wa watendaji wa Barrick Gold, Bw. Kahama ambaye kama JK na yeye ni swahiba mkubwa wa James Sinclair.

See now which direction to turn 'kumkoma nyani' missiles?
 
MKJJ,

like the olden saying,"Tell me your friends and tell you who you are" katika sheria wana principle ya kilatini kwenye statutory interpretation inaitwa "Nosctitur asssocii".
 
Mwkjj ongeza na hawa

GRAY S. MGONJA

Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited ambayo maelezo yake tumeyatoa kuhusiana na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake kama Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa mabilioni ya fedha za umma katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.

NIMROD ELIREHEMA MKONO

Mheshimiwa Nimrod E. Mkono ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijiji na Mshiriki Mkuu wa kampuni ya mawakili ya Mkono & Company Advocates ya Dar es Salaam. Barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali inaainisha kuwa Benki Kuu imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia ambapo Benki Kuu inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 60. Kwa mujibu wa barua ya wakaguzi tayari Mkono & Co. Advocates wamekwishalipwa shilingi 8,128,375,237 kwa fedha taslimu kwa kesi hiyo ambayo bado iko mahakamani. Malipo haya ni sawa na asilimia 13.5 ya deni lote inalodaiwa Benki Kuu. Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa kumalizika na hivyo inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.
Lakini hoja nyingine ya kimsingi ni kama malipo haya kwa mawakili yanaruhusiwa chini ya Kanuni za Malipo ya Mawakili na Uamuzi ya Gharama za Kesi za mwaka 1991, Tangazo la Serikali Na. 515 la mwaka 1991 (Advocates' Remuneration and Taxation of Costs Rules, 1991). Kanuni hizi zimeweka kiwango cha malipo ya mawakili katika kesi ambazo fedha inayodaiwa ni zaidi ya Shilingi milioni 10 kuwa ni asilimia tatu. Kwa kufuata masharti ya sheria hii ya malipo ya mawakili, kampuni ya Mkono & Co. Advocates ilipaswa kulipwa Shilingi bilioni 1.8.
Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au ubadhirifu wa fedha za umma kwa muda mrefu. Kwa mfano, ‘Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G. Chavda Kuhusiana na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme' iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi Novemba 1994 ilisema yafuatayo kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: "Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako tukufu na hotuba ndefu lakini ni vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba yake na Subash Patel mwenye makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De Change na Nimrod Mkono, Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD., AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)
Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: "Mheshimiwa Spika, ni vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza hapa haukuwa wa hila. Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli za Kamati (permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art (reassignment) kwa Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu kinafichwa. Nimrod Mkono alikuwa Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Oxford Services Ltd. na pia anamiliki Kampuni ya Marcus Ltd., makampuni ambayo kwa pamoja yamefaidika kwa kuupata jumla ya Shs. 4,477,870,279.61 chini ya utaratibu wa DCP."

Bila kumsahau huyu

. BENJAMIN WILLIAM MKAPA


Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 alipomaliza kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au washirika wa karibu wa familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira Mkoani Mbeya. Hisa zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa mkataba
 
jema haliwezi kutoka kwa ovu hata siku moja.
madhali kaingia madarakani kwa pesa za kifisadi, huyu mtu mpaka atatoka watanzania sisi tutalia na ufisadi tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom