Wazo: Ujinga wa watumwa wa kiafrika na siasa ya Tz ya leo, safari bado ndefu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo: Ujinga wa watumwa wa kiafrika na siasa ya Tz ya leo, safari bado ndefu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jasho la Damu, Apr 29, 2011.

 1. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wakuu JF
  Siku moja nilikuwa nasoma makala moja kwenye Internet iliyoandikwa FOOLISHNESS OF AFRICAN SLAVES. naomba niwashirikishe kwenye kisa hicho ili hapa GREAT THINKERS muweze kulinganisha na maisha ya siasa za Africa na Tanzania kwa ujumla.
  Makala inaanza hv: Kulikuwa na watumwa 100 wa kiafrika walikuwa wakilima huku wakisimamiwa na Askari wa kizungu
  1 akiwa na bunduki. wakati wakiendelea kulima watumwa 2 walipata wazo la kutoroka wao na wenzao 98.
  Watumwa wale 2 walimpiga yule Askari
   
 2. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  inaendelea

  kisha wakampora bunduki yule Askari wa kizungu na kukimbia nayo, wale watumwa 98 waliobaki nao walitupa majembe chini kuanza kuwakimbiza watumwa wale 2 na walipowafikia waliwapiga na kuwanyanganya ile bunduki na kumrudishia yule mzungu ili aendelee kuwalinda.

  Leo hii tunashuhudia matukio kadhaa yakitokea Africa na Tz katika medani za kisiasa za kuwaabudu na kuwalinda wanaotutumikisha kwa faida zao. Napenda nianze kuangazia pande za Africa nikianzia nchi ya Zimbabwe ambapo tumeshuhudia
   
 3. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  inaendelea
  Africa ikimkataa shujaa wa Africa R.mugabe ambaye siku zote amekuwa akipinga utawala wa kizungu hali kadhalika hali hiyo imejionyesha ktk nchi za kaskazin mwa Africa ambapo AU imeendelea kuwakandamiza waafrica wenzao.

  Tukirudi hapa kwetu Tz tunashuhudia dhahiri ile dhana ya ujinga wa watumwa wa kiafrica ikizidi kutuangamiza. watumwa 2 (CDM na Wanaharakati) wanajaribu kumpora bunduki(madaraka) aSkari wa kizungu (CCM) ili watumwa/watz wapate kuwa huru na maisha bora.
   
 4. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kweli mwafrika ana laana, kwa hiyo tusisubiri maendeleo ya haraka wakati sote wajinga, wavivu, waoga, wajuaji, chuki na fitna baina yetu, hatukubali kujifunza.
   
 5. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  lkn watumwa 98(CUF,UDP,NCCR etc) wanaendeleza tamaduni za kuwaabudu, kuwasujudia na kuwatii mabwana zao CCM kwa kuamua kuwakandamiza wenzao CDM na wanaharakat ili washindwe kutimiza lengo la ukomboz wa nchi ya Tanzania.
   
 6. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Hadithi ni nzuri sana ila kuhusu ulinganifu sidhani kama wewe ni mchambuzi mzuri.
  Kwa kesi yetu ni kama hao wawili wanataka kumuua askari na kumpokonya silaha ili wao ndiyo wawatumikishe wenzao 98. Kwa bahati nzuri hao 98 wamegundua hila.
  Kwa mazingira yetu hao 98 ndiyo wenye busara zaidi maana wangekosa hata chakula wanachokipata kwa taabu.
  Unafahamu hakuna mtu anapenda shida, kama suala la kumpokonya silaha askari na kutoroka katika mazingira yale lingekuwa na tija kwa angalau 80 kati yao na bila kutia shaka basi kama ni kupingwa suala hilo lingepingwa na watu wawili na hivyo kuwaita hao wajinga ingekuwa sawa.
  Nilichokipenda zaidi kutoka kwako ni kwamba unajua kuwa uwiano wa wanachadema na watanzania wengine ni mdogo kiasi hicho na kwamba ni kwa utashi wa kisiasa tu unaweza kuuita "nguvu ya umma"
  Chadema wanaweza kuongeza ushawishi kwa umma na hivyo kuweza kuaminika kwa watu wengi zaidi (wakiwemo wajinga) na kuchukua dola. Ni kama tu watachagua kuswitch kwa right politics kwa Tanzania. Waache siasa wanazozifuta tangu baada ya uchaguzi watajua ni kwa kiasi gani Ccm ni wepesi 2015! Au vinginevyo watu wataendelea kunung'unika lakini kwenye kura bado watawapa Ccm, wewe utaendelea kuwaita wajinga.
  Lakini watanzania wa sasa ni werevu sana...
   
 7. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kweli JF mnaitendea haki kama uwanja wa Great Thinkers
   
 8. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama wewe si mmoja wa wale 98 basi lazima ni fisadi au uzao wa mafisadi kama Rizwan, January, Nape etc
   
 9. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  BEPARI nina wasiwasi na uelewa wako. Refer hiyo story then think critical may be ur head has been stuckin.
  Roy masters aliwai kusema hv. Cruel people have power, they get their energy frm u through the way u respond(with negative emotions).
  We may be legally free but morally n emotional we are still in the dark ages.we all live under feudal system of slave n tyrants.its devilish military chain of command where every 1 who responds (with negative emotions) becomes a slave also loads it over a slave.
   
Loading...