Wazo: Serikali ijenge fukwe za kutengeneza (man-made beaches) kama njia za kuongeza mapato kwa baadhi ya Halmashauri

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Serikali yetu ikiwa inaangalia namna ya kuongeza vyanzo vipya vya mapato kwa ajili ya kukuza Uchumi na kuboresha huduma za kijamii kama maji, umeme, afya na elimu, hivyo kama wananchi hatuna budi kutoa ushauri na maoni yetu kila tunapoona kuna fursa mpya serikali inaweza kutumia kuongeza mapato.

Uwepo wa fukwe za kutengeneza, naona ni kitega uchumi kwa serikali ikizingatiwa fukwe za asili ni chanzo kikubwa cha mapato kwa serikali. Fukwe zinachangia mapato kwa kiwango kikubwa kwa sababu wanaochangia ni watu wa rika zote. Ukiachana na faida za kiuchumi ambazo serikali itafaidika, ajira zitazalishwa na ujasiriamali kufanyika pia zitasaidia jamii kukusanyika pamoja.

Katika mkoa kama Dodoma ambao ni makao makuu ya nchi yetu, serikali haina budi kuwekeza kwenye miradi yenye matokeo ya muda mrefu. Kwa mtazamo wangu, kuwepo kwa Fukwe za kutengeneza katika jiji la Dodoma kutasaidia kukuza uchumi wa jiji na kuhamasisha utalii wa ndani. Pia, uwepo wa fukwe hizi zitabadilisha mandhari na muonekano wa jiji letu.
 
Dodoma inatajwa kuwa ni kame lakini water table yake iko juu, unapendekza maji yapatikane kwa nja gani
 
Back
Top Bottom