Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,887
- 143,983
Moja ya vitu vinavyokera sana nchi hii ni urasimu ulioko katika maofisi, idara, vitengo na taasisi mbalimbali za serikali.,urasimu unaopaswa kuwekewa mkakati maalumu kudhibiti.
Urasimu huu sio kero tu watanzania, bali hata kwa wageni wakiwemo wawekezaji wanaotafuta vibali au huduma nyingine serikalini na hivyo kuchangia kufukuza wawekezaji.
Unakwenda katika wizara au taasisi fulani ya serikali kutafuta kibali, leseni , n.k au hata kugongewa muhuri lakini utasumbuliwa mpaka unaweza kujuta kuzaliwa nchi hii.
Yote hii ni kwasababu katika baadhi ya idara na taasisi za serikali, kumejaa miungu watu waliolewa madaraka na bahati mbaya hakuna utaratibu uliowekwa kudhibiti urasimu serikalini na ndio maana wanatesa na kusumbua watu.
Urasimu mwingine unachangiwa na taratibu na sheria mbovu zinazopelekea mchakato mirefu kabla ya mtu kupata kile anachohitaji na wakati mwingine taratibu ndefu ndio huchangia rushwa pale mtu anapochoka na kuuamua kutafuta shortcut.
Binafsi nafikiri wakati umefika wananchi wapige kura ya maoni ya wazi au vinginevyo kufichua idara na taasisi za serikali zilizokithiri kwa urasimu hapa nchini na matokeo yawekwe wazi kwa umma
Idara na taasisi zitazoonekana kupigiwa jura nyingi, zichunguzwe na hatua stahiki zichukuliwe.
Sometimes kuna urasimu hata wa kupitisha mambo ya kiserikali pale taasisi au idara fulani inapotakwa kutoa kibali kwa taasisi nyingine au kupitisha maombi ya idara au taasisi nyingine ndani ya serikali.
Urasimu na rushwa ni vitu viwili tofauti vinavyofaa kushughulikiwa kila kimoja kwa uzito wake ingawa vinaonekana kwenda pamoja.
Nakerwa sana na urasimu uliopo katika nchi yetu kuliko hata rushwa.