Wazo Mbadala; Wafugaji tufuge FARU badala ya Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo etc

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,451
29,128
Heri ya Mwaka Mpya wadau,

Leo asubuhi hii ya siku hii ya kwanza kabisa ya Mwaka huu 2017 nimeamka na mawazo mapya ya kujikwamua kiuchumi. Hii ni sababu mwaka uliopita maisha yalinitesa (kuisoma namba) hivyo wakati wenzangu jana wanauaga mwaka kwa sherehe, mie nilikua kitandani nakuna kichwa huu mwaka mpya nitoke vipi. Katika njia nilizofikiria za kujikwamua mojawapo ni ya ufugaji.

Nimesikia kua bei ya Faru mmoja ni Tshs 200million. Nimewaza kua kumbe Faru ana value kubwa namna hii. Nimewaza kua kama wafugaji tunaofuga Ng'ombe ambao mwisho wa siku tunakuja kuwauza kwa Tshs 800,000/= hadi Tshs 1,500,000/= kama tukiamua kuwekeza kwenye ufugaji wa FARU tutatoka sana kimaisha.

Manake kama Faru moja analeta kipato mara 200 zaidi ya Ng'ombe, hii ni ratio ya maana sana kufikiria. Shamba ninalofugia Ng'ombe ndio hilohilo nitakalofugia hao FARU. Labda tu nikaribishe ushauri na mawazo yenu wadau mnaonaje hii idea niliyoamka nayo asubuhi hii?? 200mil against 1.5mil si mradi zuri sana huu wakuu??

NB;
Topic hii haihusiani hata kidogo na Faru John, bali ni maswala ya Ujasiriamali na Kujikwamua kiuchumi
 
Miaka imeobgezeka kijana....kuendelea tandikia watu janvi acha....amka piga mishe utafanikiwa tu....kama g'ombe kakushinda huyo faru utaanzia wapi?
 
Miaka imeobgezeka kijana....kuendelea tandikia watu janvi acha....amka piga mishe utafanikiwa tu....kama g'ombe kakushinda huyo faru utaanzia wapi?
Ng'ombe hajanishinda Mkuu,
Nataka tu nijiongeze
 
Wazo bora kabisa la kuanzia mwaka...... mbegu tunatoa wapi ss?
 
Faru wanafugika. Sio kwa kuwauza wakizaliana bali kwa kuvuna pembe zake na kuuziuza, pembe za faru zinakatwa kwa juu na kuota kama kucha za binadamu.
Afika Kusini kuna sanctuary za aina hiyo.
 
Back
Top Bottom