FAJES
JF-Expert Member
- Oct 29, 2017
- 714
- 627
Amani kwenu Wadau,
Kama tuonavyo kuwa idadi ya Wahitimu wa Vyuo katika fani mbalimbali ni kubwa kuliko uwezo wa Upatikanaji wa Ajira hasa Serikalini.
Na ni dhahiri kuwa, si rahisi kwa vijana wahitimu kuwa na mitaji ya kujiajiri. Hivyo basi, Serikali inaonaje kama ikifupisha umri wa mtu kustaafu kazi kutoka miaka 55-60 na kuweka utaratibu wa mtu kusitisha mkataba wake wa kazi anapofikisha miaka kumi kazini.
Faida za kufanya hivyo ni kama ifuatavyo:
1) Vijana wengi wanaomaliza vyuo mbalimbali na kutegemea ajira na wao watapata haki ya kufanya kazi kwa wingi wao maana fursa za ajira zitakuwa nyingi.
2) Waajiriwa wengi watapambana usiku na mchana kufanya kazi kwa bidii ili kuwekeza zaidi maana watakuwa na fursa ya kufanya kazi muda mfupi wa miaka 10 kuliko ilivyo sasa kuwa mtu akishapata kazi anabweteka kwakujua ana ajira ya kudumu hadi uzeeni.
3) Usemi wa asiye na ajira ajiajiri utafanikiwa kivitendo maana hawa watakaomaliza mkataba wao wa miaka 10 watakuwa na mtaji ambao watautumia kujiajiri.
Karibu kwa mawazo mbadala wakuu.!
Yangu ni hayo...