Wazo langu: Sababu za makelele ya Wabunge kuhusu ubadhirifu unaofanywa na Serikali

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,247
342
Jana tulishuhudia makelele mengi kutoka kwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma unaofanywa na serikali ya CCM. Kwa wabunge wa upinzani sina neno la kusema kwa sababu wao ndio wanaojua kutekeleza wajibu wa kuiwajibisha serikali kuliko wenzao wa CCM. Wabunge wa CCM jana walionekana kama vile ndiyo wanakumbuka kwa mara ya kwanza wajibu wao pale bungeni. Wana dhamira ya kweli katika hilo?

Kelele zile nimehisi kama vile zina sababu zake nje ya tunachokiona sisi, yaani ubadhirifu wenyewe. Kwanza kabisa ubadhirifu uliofichuliwa na ripoti ya kamati za bunge siyo wa mara ya kwanza wala hautofautiani na wa nyakati zilizopita kwa maana ya viwango vya ubadhirifu. Je, makelele yale ya wabunge yalichochewa na nini? Mimi ninadhani sababu ni moja tu:rais anataka kubadilisha baraza la mawaziri, hivyo wabunge wamedokezwa kufanya vile ili ionekane sababu ya rais kubadilisha baraza la mawaziri ndiyo hizo kelele zao. Ninasema hivyo kwa sababu wabunge wa CCM siyo wa aina ile ya jana.

Tukirudi nyuma kidogo, tulisikia huko nyuma kuwa rais alikuwa na mpango wa kubadilisha baraza la mawaziri mwezi Machi, 2012, lakini hadi leo hilo halijafanyika. Tuliona vile vile habari humu jamvini na kwenye magazeti kuwa rais alikuwa anamsubiri Asha-Rose Migiro ndipo abadili baraza. Pengine sababu za kubadilisha baraza la mawaziri hazikutosha ndiyo maana mwezi Machi hakufanya hivyo na wala hata Asho-Rose Migiro aliporejea nchini baraza bado halikubadilishwa.

Leo tumesikia vyombo vya habari vikisema kuwa Rais Jk anausifu msuguano uliopo kati ya bunge na serikali kuwa ni mzuri kwa ajili ya kuleta ufanisi katika utendaji wa serikali. Wakati yeye akisema hivyo, baadhi ya wabunge jana walikuwa wanasema kuwa mjadala wao wanataka rais ausikie pamoja na waziri mkuu. Je, rais JK alikuwa akiyatazamia kuyasikia yale aliyoyasikia? Je, ni kweli rais hakuwa anajua taarifa za ripoti hizo na huo mpango wa wabunge wa CCM kuonesha ukali kwa serikali ya chama chao?

Rais kama unataka kuvunja baraza la mawaziri siyo lazima mpaka uwatume wabunge wa CCM kukusemea bungeni jambo la kufanya; mara "rais aache upole" nk. Rais alishindwa kuelewa ubovu wa mawaziri wake hadi wasemwe bungeni? Wabunge wa CCM waache unafiki, janja yenu tunaijua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom