Rose Mayemba
JF-Expert Member
- May 7, 2012
- 721
- 1,017
Labda nianze kwa kutoa mfano wa mwanawake hawa wawili.
Mmoja kati ya hawa wanawake alibahatika kupata mtoto mapema tu baada ya kufunga ndoa, alimpenda sana mtoto wake tangu kuzaliwa na kukua kwake.na kwasababu hii hata mtoto naye alijua anapendwa sababu iliyopelekea awe huru kufanya kila atakacho.
Majirani hawakuvutiwa sana na mwenendo wa mtoto yule hivyo kumtonya mamaye apate muda wa kukaa na kumkanya mwanae. lakini kwa sababu mama alimpenda sana mtoto wake alihofia kumkwaza hivyo kumwacha aishi vile alivyotaka.
Siku isitokuwa na jina yule mama alipata taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba mwanae amembaka mtoto wa miaka 12 hivyo ana kesi ya kujibu, yule mama alilia sana lakini haikusaidia kwani mwanae aliishia gerezani.
Huyu mwenzake naye akapata mtoto, lakini makuzi yake yalikuwa ya taabu sana mpaka alipopata akili za kujitambua, mamaye alimpenda sana, hakusita kumkanya kila alipoona anakwenda kinyume na maadili na ilipobidi alimwadhibu, hapa napo majirani hawakukaa kimya, walimwendea na kumsihi asimnyanyase sana mtoto kwani ule ulikuwa ndo wakati wake.
Kwa msimamo mkali yule mama alipuuza mafundisho ya majirani na kumlea mwanae katika misingi imara, mwanae aliendelea vema na baadae alikuwa msaada mkubwa sana katika familia na ukoo wao.
********
Kusimamia misingi ya kile unachokiamini ni jambo la muhimu sana kabda hujapiga hatua nyingine mbele.
Ni wangapi tumeona biashara zao zinakufa kwa sababu tu ya kukosa usimamizi makini?. Ni wangapi tumeona wakishindwa katika mipango yao kwa sababu ya kuyumba kwao kifikra.
BANADAMU MWENZAKO ANAWEZA KUSEMA KWA NIABA YAKO LA HAWEZI KUKUSAIDIA KUFIKIRI.
ILI UWE BORA NA IMARA NI LAZIMA USIMAMIE MISINGI NA KANUNI ULIZOJIWEKEA BILA KUSAHAU KUTAFUTA NI WAPI MWENZAKO ALIJIKWAA ILI KUIFANYA NYEPESI ZAIDI SAFARI YAKO