Wazo langu: Hivi haiwezekani CHADEMA ikafanya mkutano wa hadhara kwa amani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo langu: Hivi haiwezekani CHADEMA ikafanya mkutano wa hadhara kwa amani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mndengereko, Sep 3, 2012.

 1. Mndengereko

  Mndengereko JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 7,127
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
  Ndugu zangu wan JF embu leo naomba tuongelee hii kitu kutoka moyoni. Mimi sio mnazi wala mwanachama wa chama chochote ila kila ninaposikia CHADEMA wanataka au wanafanya mkutano mkubwa wa hadhara basi watazuiliwa na polisi then wao watakaidi amri hiyo mwishowe watafukuzana kwa marungu na mabomu ya machozi mpk watu wasio na hatia kufa na wengine kujeruhiwa.

  Maoni nionavyo mimi ni kama vile CHADEMA wanfanya makusudi ili watu walichukiie jeshi la polisi baada ya kujeruhiwa.Hivi CHADEMA wakiahirisha mkutano wao mpaka siku watakokubaliana na jeshi la polisi kosa linakuwepo wapi?

  Hivi hatuoni kwamba uhai wa binadamu una thamani kuliko hizi siasa za bongo tafadhali jamanii tujirekebishe hata kama polisi wamekosea lakini kama CHADEMA wangefuata maagizo yao asingekufa mtu Iringa,Morogoro wala Arusha.

  Nawasilisha wadau
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  UMEANZA vizuri ila mwisho UKAJIFUNUA GAMBA LAKO.

  Nani kakuambia POLISI wanaruhusiwa KUZUIA au KURUHUSU Mikutano/Maandamano?

  Wao wana taarifiwa tu ili watowe ulinzi na hayo mengine hayawahusu.

  Hiyo ndiyo KATIBA YA NCHI kwa sasa. Kama mambo huyajui KAA KIMYA.

  HAKI HAIOMWBI ILA INAPIGANIWA.
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280

  Sasa mpunguze kulialia mkipigwa, maana kwenye kupigana kuna kupiga na kupigwa.
   
 4. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wewe sio mwanachama wa chama chochote ila umetumwa na wanachama wa CCM!

  Rudi kajipange upya!
   
 5. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Eti mie siyo mnazi!!!??? Kumbe ni mchongoma! ubongo uliokufa huu!
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Fujo hutokea pale tu polisi wanapokuwepo kwenye mikutano ya CHADEMA.

  Kwenye tukio la jana, haingii akilini kwa nini polisi wengi walikuwa wanamzunguka mwandishi mmoja tu wa habari?
   
 7. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hii ni dunia......hakuna binadamu wa kawaida anayeweza kushangilia mauaji hata kama ni ya adui yake......kumbuka leo ni kwa Daudi(R.I.P) .....kesho inaweza kuwa kwako au kwa ndugu yako wa karibu......hutakufa kwenye maandamano ya CDM manake wewe sio mwanachama wao ila utauliwa hata na majambazi.......narudia tena hii ni dunia!
   
 8. m

  mamajack JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wewe mwehu uliyetoroka matibabuni,wanaopigwa wala hawahusiki na cdm.ila polis wenu wanamakengeza.
   
 9. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wanatii sheria bila shuruti kutoka kwa mkubwa wao JK!
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nani analia? Umesoma popote hapa mie NINALIALIA? Hebu soma kama nimejadili chochote kuhusu hili.

  Muda wa kuendelea kujadili haya mauwaji umekwisha. Njia mbadala inabidi zianze kutafutwa.
   
 11. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,173
  Likes Received: 1,257
  Trophy Points: 280
  Wewe nafikiri una matatizo ya ubongo!! Kazi ya jeshi la polisi ni nini?
  Hivi polisi wakiua watu wasiokuwa na makosa kwa risasi ni nani wa kulaumiwa!!
  Kumbuka Arusha maandamano yaliruhusiwa na kuzuiliwa dakika za mwisho!! kwa sababu za "kiintelijensia".
  Angalia kote utauona mkono mchafu wa serikali. Unasisitiza waache kukutana na wakutane kwa matakwa ya wakubwa, huku wenzao wa CCM wakifurahia ulinzi madhubuti wa jeshi hilo hilo kipindi hicho hicho.
  Double standard ndiyo inayoudhi.
  Jeshi la polisi na CCM wamedhamiria kuzuia mageuzi kwa nguvu za risasi za moto!! hili ni wazi. Kwa sasa mawazo na mtizamo wako hauna nafasi tena.
   
 12. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Kazi ya kichwa sio kufuga nywele.........mtoa mada naona kichwa chako unatumia kufuga nywele...mikutano ya cdm yote huwa na amami tatizo ni ccm na serekali ambazo siku zao zinahesabika.....gamba huonekana kwenye mavi yaliyokauka kumbe nawewe ni gamba loooooo!
   
 13. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  unasema sio mnazi wa chama chochote lakini utakuwa unajua fika kuwa baada ya polisi kusababisha vifo pale Arusha na kusumbua sana cdm walifanya maandamano na mkutano bila hata chembe ya ulinzi wa polisi na kilichotokea kila kitu kiliisha bila hata chembe ya vurugu.
  Tokea hapo wenye akilki zao wakajua na kama wewe hujajua hilo muulize mwenzio lakini utakuwa umechelewa sana kujua chanzo cha vurugu!
   
 14. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tunajua kati yetu lipo kundi linalofaidika na huu mfumo uliopo na pengine na wewe pia ni miongoni mwao!! kwa hiyo ni lazima mtu kama wewe kufurahia kwa kila kinachotokea hivi sasa hapa nchini! Sikushangai!
  Lakini kinachotokea leo ni mbegu tu mbaya inapandikizwa ipo siku kama utakuwa hai utajuta kwa kinachokuja kutokea mbele!
  Kama hutokuwa hai basi itamhusu, mwanao au mjukuu wako ama vyovyote vile lakini itakuwa mbaya sana.

   
 15. Mndengereko

  Mndengereko JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 7,127
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
  haingi akilini kuamini kwamba mara zote polisi hawawatendei haki chadema na pia ni ngumu kwa mimi kuamini kwamba chadema wapo sahihi mara zote yaani hawakosei kuna kitu wankipandikiza jamnai tufunguke nilijua mtaniita mimi gamba lakinii huu ndio ukweliambao mimi naudhania
   
 16. P

  Paul S.S Verified User

  #16
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Haki inaambatana na wajibu mkuu na hakuna uhuru usio na mipaka

  Kazi ya polisi haiishii kupokea taarifa tu na kuleta ulinzi, ni lazima pia waangalie hali halisi ya kiusalama inaruhusu hicho kinachotakiwa kufanyika kifanyike
  Sasa kama polisi wataona kunasababu za msingi hicho kilichotaarifiwa kufanyka kitasababisha kukosekana kwa usalama ambao wao kama chombo cha kazi hiyo wanaona iwapo kikitokea na wakijaribu kizima inaweza kuleta mdhara basi wanawajibu wa kusitisha au kubadili utaratibu

  Ingawa maranyingi Polisi wanakuwa wanatoa maamuzi ya kionevu na kibabe dhidi ya CDM lakini pia CDM nao wakati mwingine wawe wanaangalia pia, maana kuwashawishi tu watu kufanya kitu ambacho kinapelekea vifo na pengine kupeleke kukipa umaarufu zaidi chama tu sio busara nzuri pia

  Na most of time ni maandamano/matembezi ndio yanaleta tabu na si mikutano
  Naamini wanaweza kabisa kufanya mikutano yao vizuri na wananchi wakawasikia na kuwaelewa bila kuanza kuandamana mabarabarani
   
 17. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  mndengereko kwa taarifa yako polisi wamekuwa wakivamia mikutano ya chadema na kuanzisha vurugu kulikuwa na haja gani kutumia polisi kwa mkutano wa kufungua tawi kijijini??chaguzi za chama zinazofanyika kwenye matawi mpaka watu kutishiana bastola mbona polisi hawafanyi uvamizi kama ule wanaofanya kwenye mikutano ya chadema??kwa hakika nchi inakwenda autopilot daudi mwangosi anapigwa bomu la tumbo rpc anaangalia polisi wamemshikilia ilijamaa washoot tumbo bado unaongea ujinga mndengereko???polisi watakanusha sana lakini awamu hii na huko tunakokwenda hali yao itakuwa mbaya sana.wameamua kutekeleza mikakati ya ccm kuvuruga vyama vya upinzani kwa bahati mbaya muda ndio unatoa hukumu.
   
 18. Mndengereko

  Mndengereko JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 7,127
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
  kwa arusha ninajua kwamba kabisa polisi walichemka lakini vipi seemu nyingine ambapo chadema waliambiwa kuna sensa na wenyewe wakanagania kufanya mkutano
   
 19. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ndiyo matatizo ya kula kabla hujapiga mswaki.

  Pitia habari hizi na angalia kama kulikuwa na MKUTANO WA NJE au maandamano.

  Safari hii POLISI wamedai lazima kuwe na mikutano ya NDANI TU na si ya nje.

  Ila hapohapo, Mwanza wameruhusiwa kufanya FIESTA (TAMASHA).

  Na hata hivyo, sababu ya KUPIGA waandishi wa habari ni nini?

  Kumbuka aliyeuawa alikwenda kuuliza kwa nini wanampiga Mwandishi mwingine.

  Anyway, sikujua kuwa Waandishi wa habari walikuwa wanaandamana jana huko Iringa.
   
 20. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama sikosei wewe ni aidha ni punguani.Maana swali la kwanza ulipaswa kujiuliza wewe mwenyewe ni kwamba nini kazi ya jeshi la polisi na nini kazi ya chama cha siasa na chama cha siasa ni kitu gani..Ujiulize kwanini jeshi la polisi liombwe na kwanini kila likiombwa na CDM lazima likatae!!!Kisha ungejiuliza kwani jeshi la polisi haliwezi kuwalinda chadema kwa amani?Ukishapata hayo majibu ndo uje hapa jamvini soi unaanza ooh mimi sio mnazi wa siasa alafu unaleta pumba zako za kitoto hapa!Watu kama ninyi ndo mnadhani mtanzania sana ni yule aliye CCM na Chadema sio watanzania na hawana haki ya kuishi...Sasa ujue tu kwamba CDM sio mbowe wala wilbroad slaa wala kabwe chadema ni watanzania wote wenye haki ya kukutanika kusikiliza sera za kila chama na neno chama ni jina tu ila ni watanzania haohao sio kama unavyotaka kutufikirisha ujinga wako kwamba labda chama ni jitu fulani lililotoka maporini au mbinguni au baharini!Emu muulize hata mtoto wako wa chekechea kwanini polisi wauwe watu ambao hawana uhusiano na wanasiasa wanauwa mara muuza magazeti mara mwandishi wa habari tena wako rundo yeye mmoja tu na hana silaha!!!Sasa kwa upunguani utakuta mke wako siku katolewa utumbo na polisi na wala hajui hata siasa kama ulivowewe huijui Kilaza wewe!!!
   
Loading...