Wazo lako ni la thamani sana, natanguliza shukrani zangu

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Habari wana jamvi, poleni kwa mihangaiko ya kila siku ya kutafuta riziki.

Mimi ni kijana niliehitimu elimu yangu ya degree mwaka jana kutoka chuo kimoja hapa nchini. Kama ilivyo kwa watu wote wenye malengo na kesho zao, nimekuwa nikitumia muda mwingi kuwaza, kupanga na kuweka mikakati kwa ajili ya kesho yangu. Ndoto yangu imekuwa ni kufanikiwa kimaisha ili niweze kutimiza yale yote niliyoyapanga kadri Mungu atakavyonijalia afya na mafanikio.

Kiukweli, mpaka sasa namshukuru sana Mungu kwa yote aliyonijaalia kwani nina afya, nguvu, uwezo na kubwa zaidi amenijaalia uwezo (Personal skills) ambao naamini siku nikibahatika kupata nafasi kwenye taasisi au mashirika nitautumia kwa ufanisi wa hali ya juu katika kufanikisha malengo ya mwajiri na malengo yangu binafsi. Naamini katika uwezo wangu na bado sijakata tamaa ya kutafuta ajira, imani yangu ni kuwa siku moja Mungu atafungua milango yake na nitafanikiwa kupata connection ambayo itabadili zaidi maisha yangu na kuweza kuishi maisha ya ndoto yangu. Only God knows!!!!!

Wakati nikiendelea kupambana kusaka nafasi kwenye taasisi tofauti tofauti, nimekuwa pia nikijitahidi kuweka akiba kidogo ya fedha ninazozipata katika harakati zangu za kila siku, lengo likiwa ni kuweza kuapata mtaji wa kufungua biashara yangu mwenyewe. Hata siku nikibarikiwa kupata ajira, bado nitatumia kipato changu kuzidi kuikuza biashara yangu. Mimi ni muumini mkubwa wa vyanzo tofauti tofauti vya mapato.

Nikiwa kama mkazi wa DSM, nimekuwa nikifanya utafiti wa biashara gani ninaweza kuifanya kwa kuzingatia eneo nililopo. Na baada ya kutafiti kwa muda mrefu, nimedhamiria kuwa siku nitakapofikisha akiba ya sh. 1,000,000/= basi nitaitumia kama mtaji wa kuanzisha biashara. Na biashara nilizozidhamiria ni hizi zifuatazo:-
1. Kufungua saloon ya kiume (Hiyo hela imejumuisha mahitaji yote kuanzia kodi ya flemu na vifaa vyote vya saloon.

2. Kununua pikipiki kwa mtu (Iliyo katika hali nzuri) na kumpa dreva kwa mkataba ili awe ananilipa kwa wiki. Kwa utafiti mdogo nilioufanya nimegudua kuwa pikpiki used inaanzia 800,000 hadi 1.2m.

Moja kati ya biashara hizo nimepanga kuzifanya endapo tu nikifanikiwa kufikisha akiba ya sh. 1m kwenye hii hela ndogo ambayo najibana ili kuitunza. Pamoja ni hii biashara, bado nitaendelea na harakati zangu za kusaka ajira au kipato kwa njia zingine halali.

Ningependa kupata maoni na ushauri kutoka kwenu wakuu hasa kwa wazoefu wa biashara hizi ili niweze kuzielewa kiundani kupata details nyingi na kufanya maamuzi ambayo yatanisaidia kupunguza risk japo kwenye biashara risk haiepukiki. Kwa wengine pia wenye mawazo mbadala ya kibiashara ambayo yanaweza kunisaidia kwa kuzingatia location ya DSM kwa mtaji usiozidi 1m ninaomba kuasikia pia ili kwa pamoja tujikomboe. Na kwa yeyote anaeweza na angependa kunishika mkono (connection ya kazi) nitashukuru sana.

Ni matumaini yangu kuwa siku moja nitapata mtaji na nitaifanya hii biashara na panapo majaliwa nitaleta mrejesho chanya hapa hapa kwenye jukwaa. KARIBUNI SANA kwa maoni na ushauri.

FOHADI: Focus Hardwork Discpline
 
Kuhusu pikipiki kwanini usiendeshe mwenyewe?
IMG_20201006_185000.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom