Wazo la Rais Magufuli kuanzisha kambi za vijana wasio na kazi ni zuri ila..

RingaRinga

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
1,041
510
Mh Rais aliwataka wakuu wa mikoa kuanzisha kambi za kazi kwa vijana ambao hawana kazi ili kuondoa wimbi la vijana wanaokaa mitaani bila kazi zenye tija.

Ila sina hakika kuwa serikali imejipangaje katika kuhakikisha kambi hizi zinakuwa nafaida kwa walengwa na taifa kwa ujumla

Wakuu karibuni kwa mchango wa mawazo au ushauri wa jinsi ambavyo serikali inaweza kufanya ili kambi hizi zivutie vijana wengi kujiunga nazo kwa hiari bila hata kulazimishwa na mwisho wa siku ziwe na faida kwao na pia kambi hizi zisiwe mzigo kwa taifa, karibuni!
 
Sina Mawazo Yoyote,Kwa Kuwa Wenye Kulitaka Liwepo Hawajuhi Hata Ni Kwanini Vijana Wanakaa Pasipo Kuwa na Ajira
 
Hilo wazo ni zuri sana kama mikoa itajipanga kikamilifu. Mkoa wa Kigoma uliwahi kufanya kitu kama hicho kwa kuwakusanya vijana katika wilaya ya Kigoma na kuwaweka katika kambi. Vijana hao walipewa shamba eneo la Lugufu kipindi cha mkuu wa wilaya Mongela. Vijana hao walipewa pembejeo, mbegu na vitu vingine muhimu kwa ajili ya kilimo. Ilifikia hadi Mikoa mingine ilituma wataalamu wao kuja kujifunza namna Mkoa ulivyohamasisha vijana kujiunga pamoja.

Hata hivyo,sina uhakika kama kikundi hicho kipo hai hadi sasa. Kikundi kingine cha vijana kilianzishwa katika wilaya ya Kibondo(Power Group). Kikundi hiki kilijishughulisha na kilimo cha mihogo. Viongozi wengi waliokuwa wanatembelea mkoa wa Kigoma walikuwa wanapelekwa Kibondo kwenda kukagua kikundi hiki kwani kilikuwa na mafanikio makubwa. kikundi hiki nacho sina uhakika kama kinaendelea. Kwa ujumla, kama viongozi wa mikoa wana utashi wa kisiasa, vikundi vya vijana vinaweza kuanzishwa mikoani na kuwa na tija kama vikiwezeshwa!
 
Mimi nadhani kulikuwa na tatizo la kukosa dhamira ya kweli ya kuhakikisha kambi hizo zinakuwa suluhisho la vijana kujikwamua na tatizo la ajira hasa katika sekta binafsi,
Hapakuwa na utashi wa kisiasa.

Maoni yangu juu ya swala hili ni haya:-
i) Serikali inaweza kuandaa sera itakayopelekea kuanzishwa kwa kambi hizi lakini ziwe na mfumo tofauti kimuundo tofauti na vile haa mym alivopendekeza, zisiwe kama JKT.
Kama sikosei nadhani kambi zilizokuwa Kigoma na ambayo ipo Mara kwa sasa zimeanzishwa chini ya ubunifu wa mikoa husika, na hapo ndipo inapofika mahala kambi hizi zinakuwa hazina mluzi wa kutosha kuzifanya ziwe kimbilio la mtu yeyote anayetafuta ramani ya kuanzia maisha ya ujasiriamali. Kambi hizi ziundwe chini ya sera ya taifa na si ubunifu wa serikali ya mkoa.
ii) Kwa kuwa ajira kubwa ipo ktk sekta ya kilimo na ufugaji serikali iwajengee uwezo wa kiujuzi na kimkakati ili vijana waweze kufanya shughuli hizo kwa ufanisi pindi watakapotoka katika makambi hayo.
iii) Serikali ni vyema ikaandaa masoko ya kuaminika kwa bidhaa zitakazokuwa zinazalishwa hapo kambini kwa muda wote lengo likiwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana hawa kuondoka kambini na mitaji yao itakayowasaidia kuanza ujasiriamali binafsi bila kuwa na vikwazo vya mitaji.
iv) Serikali pia inaweza ikawaandalia maeneo ya kufanyia shuhuli za uzalishaji mali vijana wenye mahitaji ya kuendelea kukaa sehemu moja ili waweze kuendelea kufanya shughuli zao pamoja kama walivyozoea lakini pia iwaelimishe mbinu za kutafuta masoko, AU
v)Serikali iwawezeshe vijana hawa kuunda vyombo vya kikanda kama ushirika ambavyo pia vitawasaidia kupata masoko ya uhakika ya bidhaa zao.

Naamini mawazo haya yanaeeza kuboreshwa kadri inavyofaa na kufanyiwa kazi ili twende mbele kwa kasi.
Vijana ndio taifa la leo wakiachwa nyuma ni bomu lenye kulipuka wakati wowote.
 
Back
Top Bottom