Wazo la Makonda siyo baya ila lianze na Serikali kuonesha mfano

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,304
12,965
Wazo la RC wa Dar kuwasihi wenye nyumba kupunguza kodi hasa wakati huu wa janga la Korona siyo baya kutokana na hali mbaya ya uchumi kwa wengi kwa kuwa biashara nyingi zimesimama au kufa, ofisi na taasisi nyingi zinashindwa kulipa wafanyakazi wao. Kwa sasa wenye uhakika wa kipato ni watumishi wa serikali na mashirika yake tu lakini sekta binafsi ni shida shida tupu.

Mimi naona Makonda ameota ombi zuri lakini angeanza na kuisihi serkali ipunguze bei za mafuta, umeme, maji na kodi ili kuwapa nafuu watu wengi kwa wakati mmoja kuliko kuangalia kundi dogo sana la wapangaji. Serikali inapaswa ianze kuonesha mfano kwa kuona madhira yanayo wapata wananchi wake wengi kwa sasa. Hii hali ya sasa ni kama msiba ambao haujulikani tanga lake litavunjwa lini.

Cha mwisho na yeye Makonda ajitahidi kujikarantini kwa kuepuka kufanya mikusanyiko ya watu kwakuwa licha ya kuwa ni kinyume na maelekezo ya watalaamu lakini ni hatari zaidi kwake na anaowahutubia. Rais mwenyewe kaenda kujifungia Chato sasa na yeye atulie ndani na ikibidi atumie vyombo vya habari kama radio na TV atasikika tu sio lazima azunguke na Mike kama MC (Master of Confusion).
 
Huyu hupenda kujidai mbunifu lakini anachofanyaga ni ujinga mtupu. Kwanini asiseme yeye mf. anakata 50% ya mshahara wake kununua vifaa vya wauguzi wa korona? Yeye kutoa hapana ila anataka kuwakandamiza wengine!!! Mjinga sana huyu jamaa
 
... kutokana na hali mbaya ya usafiri iliyopo ikichagizwa na mfumo wa ovyo wa usafiri wa umma uliopo hususan mijini zaidi Dar-es-Salaam; serikali itoe maelekezo kuhusu wafanyakazi kuchelewa makazini. Mikusanyiko ya kutisha ya abiria kwenye vituo vya daladala na mwendokasi kutokana na level seat haitazamiki!

Magari ni machache, miundombinu ya hovyo, abiria ni wengi kuliko uwezo wa vyombo vya usafiri vilivyopo lakini serikali ni kama vile haioni chochote! Ni jambo la kawaida kufika kituoni saa kumi na moja lakini hadi saa mbili hujapata usafiri; wananchi wafanyeje? Katika kipindi hiki cha janga la korona muda wa kuingia kazini usogezwe hadi saa tano asubuhi. Hiyo ndio hali halisi!
 
Back
Top Bottom