Wazo la leo: Vikundi vya mazoezi ya viungo virasimishwe

pererge

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
571
201
Kumekuwa na tabia ya vijana maeneo mengi, kwa jiji la Dar Es Salaam, kufanya mazoezi ya viungo asubuhi.

Pita manzese darajani asubuhi utakuta vijana wanajifua kwa pushap, kuruka, kurushiana ngumi na aina nyingine za mazoezi.
mazoezi hayo hufanyika juu ya daraja na wengine huwa chini yaani kwenye barabara (ya BRT)

Kwa mpita njia anayewahi kazini asubuhi na mapema atakuwa na uhakika gani kuwa hao wanamazoezi ni salama kwake?

Nadhani kutokana na kukua na kuongezeka kwa hao wanamazoezi wa asubuhi ipo haja kwa serikali kuweka utaratibu wa kuvisajili vikundi hivi ili vijulikane rasmi.
Vikisajiliwa itajulikana Jina la kikundi, Viongozi wao, Ofisi au Kituo chao, Pahali rasmi pa kufanyia mazoezi n.k.

kwakweli kwa sasa pale Manzese darajani kundi linalofanya mazoezi limekua kubwa hadi linatisha.

Nawakilisha hoja.
 
Inabidi polisi waweke doria maeneo kama hayo kuhakikisha kuwa usalama unakuwepo. Kuvirasimisha sidhani kama itazuia uhalifu. Wakikataa kujisajili utawanyima haki yao ya kufanya mazoezi?

Kuna wengine wanakuwepo maeneo ya beach karibu na aga khan hospital wakitokea maeneo mbalimbali ya dar. Si rahisi kuwasajili wale, wengine wala hawajuani!
 
Hilo la wafanya mazoezi mmojammoja sijajua nini kifanyike. Pia kama ni mtu anafanya zoezi lake kukimbia huko ufukweni hiyo si tatizo sana ila wakishakuwa kundi kubwa ni heri wakawa na utaratibu maalum wa kufanya mazoezi.

sasahivi yanajengwa madaraja mengine pale ubungo, nayo yatakuwa ni viwanja vya mazoezi.
 
Labda sijakuelewa vizuri. Hapo darajani wanakuja kundi au mmoja mmoja. Kama ni kundi ka wanaokimbia jogging weekend ni vizuri kuwa na utaratibu maalum wa kujulikana. Lakini kama kila mtu anakuja kivyake kisha wanakutana pale, urahisi ni kuongeza usalama tu
 
sijafahamu wanakuja kwa utaratibu gani ila ukipita hapo muda wa asubuhi saa moja moja utakuta watu zaidi ya ishirini wakirushiana makonde wengine wanapiga poshap n.k ni kikundi kipo poamoja
 
sijafahamu wanakuja kwa utaratibu gani ila ukipita hapo muda wa asubuhi saa moja moja utakuta watu zaidi ya ishirini wakirushiana makonde wengine wanapiga poshap n.k ni kikundi kipo poamoja
Kamata wote hao peleka JKT wakajenge taifa maana wana nguvu za kuchezea
 
Back
Top Bottom