Wazo la leo: Tatizo la watoto wa mitaani nchini Tanzania litaisha lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo la leo: Tatizo la watoto wa mitaani nchini Tanzania litaisha lini?

Discussion in 'Jamii Photos' started by Pape, Aug 9, 2010.

 1. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa!
   

  Attached Files:

  • AB.jpg
   AB.jpg
   File size:
   104.3 KB
   Views:
   43
 2. A

  Anold JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Tatizo la watoto wa mitaani ni tatizo sugu na baya sana hasa katika nchi zinazoendelea. Kwa Tanzania tatizo hili halionyeshi dalili za kuisha maana mamlaka zinazohusika hazioni sababu za kukabiliana na tataizo hili. Inasikitisha sana kuona watoto wengi wakiwa wanarandaranda mabarabarani huku viongozi mbalimbali wakiona ni jambao la kawaida. Mimi binafsi ninapowaona watoto hawa wanazurura moyo huniuma sana maana naona watoto hawa hawajui lolote na hawastahili kupata tabu hii wanayopata, fikiria jua, mvua, baridi pamoja na kukosa huduma zote muhimu ni mambo ya kawaida kwa watoto hawa.

  Mtu angeniambia niwapi nielekeze lawama zangu, moja kwa moja ningeelekeza kwa serikali kwani hao ndiyo wanaweza kukabiliana hata kuondoa tatizo hili moja kwa moja na kwa haraka. Mimi nilipokuwa nasikia Kitu kinachoitwa Ustawi wa jamii, nilidhani ni watu ambao wakati wote huangalia na kusimamia jamii ya Kitanzania nakujua matatizo yao na kuyachukulia hatua, inavyoelekea hilo sio jukumu lao!! Niliwahi kufikiria kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ndiyo ingebeba jukumu hili ambalo sidhani kuwa ni kubwa la kuwashinda, chakusikitisha ni kwamba sijawahi kusikia mpango wowote wa maana unaoonyesha kuwa serikali imechoshwa na tatizo hili la watoto wa mitaani, jukumu hili toka zamani linaelekea kuachiwa Taasisi za dini ambazo nyingi kwa sasa hazina uwezo kutokana na kujitoa kwa wafadhili wa Kizungu ambao waliweza miaka hiyo kulibeba kwa kiasi fulani. Tatizo hili la watoto wa mitaani kwa kiasi kikubwa limeota sugu sana katika miji mikuu hasa mijini. Tatizo hili haliwezi kwisha kutokana na ubinafsi na ukosefu wa Upendo kutoka kwa viongozi wetu pia jamii kwa ujumla kuona kuwa ni kitu cha kawaida kuona mtoto akitangatanga bila kuwa na usimamizi au walezi wa uhakika. Hii ni hatari sana kwani pamoja na kuwa hatima ya watoto hawa itakuwa mbaya lakini haya ndiyo mambo yanayochangia kuongezeka kwa uhalifu na mambo yanayoendana na hayo.Wakati umefika Serikali yetu kutafuta namna ya kukabiliana na tatizo hili ili ikiwezekana liondoke kabisa aidha manispaa pamoja na Halmashauri na jamii kwa ujumla iweke mikakati madhubuti ya namna ya kukabiliana na tatizo hili, kinachokosekana hapa ni ubunifu na kutokuwa na viongozi ambao wanaliona tatizo hili la watoto wa mitaani kama changamoto, sitaki kuamini kuwa jiji kama hili la Dar linaweza kushidwa kuamua kujenda vituo maalum vya watoto hawa na kuhakikisha kuwa kila atakayekutwa anazurura mtaani hupelekwa kwenye vituo hivyo na kuhakikisha wanapewa huduma pamoja na elimu ili watoto hawa baadae wawe manufaa kwa taifa badala ya kuwa balaa kama wataachiwa kama ilivyo sasa. Haya ni mambo yanayowezekana jamani!!!!
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Ndugu yangu, hili tatizo litaendelea kuwa kubwa kama tutaendelea kufikiria kuwa wa kulaumu ni serikali kama unavyosema hapa.Ni sawa na kutibu dalili badala ya kutibu kiini na chanzo cha ugonjwa. Hawa watoto wanaoitwa wa mitaani, hawajatokea mitaani kama ugonjwa bali tunawazaa sisi wenyewe. Wazazi mara nyingi kwa sababu moja ama nyingine hutoa msukumo wa kufanya watoto waishi mitaani badala ya ndani ya familia.Ukiachailia mbali watoto yatima wenye kufiwa na wazazi wote, wengine wanakuwa na wazazi - baba na mama. Unakuta labda baba kampa ujauzito mwanamke kisha akamkimbia au kukataa mimba/mtoto. Na mwanamke anayezalishwa ( asingepata ujauzito kama angetumia kinga ) alipaswa kujua kabisa kuwa kitendo hicho kingeweza kuleta mtoto na mzigo mkubwa wa malezi ungemwangukia. Kwa ujinga wake ( nasisitiza tena UJINGA WAKE) vyote hivyo hakuviona na anapojikuta kapigwa chenga ya mwili, basi hukimbilia njia rahisi ya kutelekeza mtoto! Wazazi wengine huweka mazingira magumu sana kwa watoto - ukatili, na hata wazazi wanapotengana na kuoa au kuolewa basi mzigo wa watoto huonekana kama kero, na kwa vile hakuna upendo unaoonyeshwa kwa watoto basi watoto hutoka majumbani na kuishia mitaani.Watoto wengine ni wakorofi tu hawapendi kuwa wasikivu na huona ni afadhali kuishia mitaani. Kiafrika hatukuwa na utaratibu wa shelters/homes kwa watoto hata yatima maana familia pana ( extended family) iliwachukua watoto na kuwalea.Siku hizi tunaona watu wakitaka serikali ichukue jukumu hili.

  Huenda tungeanza na kupunguza hizi sababu za kuzalisha watoto wa mitaani. Wazazi wawe na ufahamu kuwa vitendo vyao huzalisha watoto wa mitaani. Nitarudi tena kwenye hii mada maana nahitaji kuondoka hapa sasa.
   
 4. F

  Fanta Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi naona wa kuwalaumu kwanza kabisa ni wazazi, (mzazi ndio mtuhumiwa in the first degree). Kama tungewajibika kwa matendo yetu nadhani hawa watoto wangepungua kwa kiasi kikubwa sana.

  kila kitu tukisukumia kwa hii serikali tutakuwa tunakosea wakati mwingine. Hata yenyewe in limits. Hebu tueajibike kwanza kwa kiwango chetu kabla hatujafungua midomo kuilaumu serikali (am not waiving the responsibility of the govt here)

  hebu fikiria mnapeana mimba huko, then mmoja wa wazazi au wawili wanaamua kuyakacha majukumu yao ya kulea watoto na kuwafanya waishie kuranda mitaani, unailaumu serikali ndo ilikutuma kwenda kuijaza dunia bila mpango??

  Its high time people should take responsibilities when they crew up!!
   
Loading...