Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,794
Kuna kitu kinaniumiza na kunishangaza sana mpaka leo... MAREHEMU KUDAIWA PESA YA MATIBABU!
Hili pengine liko hapa kwetu tuu tena kwenye hospital zetu za setikali ambako ndio wanyonge wengi hukimbilia Tuna viongozi wetu waliojivika wema sana lakini katu sijawahi kuona hili walau wakilinong'ona...NEVER!
Kama majirani ndugu na jamaa wanaweza kusamehe deni lolote walilokuwa wanamdai marehemu serikali yenye ukwasi inashindwa vipi kusamehe gharama za matibabu? Hii ni laana mjue
Kama hujawahi kukumbwa na hiki kitu ni ngumu kuelewa.. Lakini chukulia mfano mmemuuguza kwa hali ngumu sana ndugu yenu ambaye wakati mwingine ndio mtegemewa wa familia. Pengine alipata maradhi mbaya au ajali, mkamuuguza kwa muda mrefu lakini hatimaye akafariki dunia
Mkiwa mko kwenye uchungu mkubws wa kumpoteza mpendwa wenu ambaye sometimes anaacha yatima mjane au mgane.. Kuna dunia mpya ngumu inayoisubiri familia ya namna hiyo kuanzia chakula, mavazi, malazi elimu, afya nk.. Mnazuiwa na uongozi wa hospital husika kwamba hamuwezi kuuchukua mwili wa mpendwa wenu hadi mlipe gharama zake za matibabu! Hili jambo linaumiza sana
Unajiuliza hii ndio serikali yangu ndani ya nchi yangu huru inavyojali raia wake!? Tulimpoteza mjomba wetu mwaka 2007 tena kwa uzembe wa madaktari pale Muhimbili lakini tukanyimwa mwili hadi tulipe deni la matibabu yake kiasi cha million saba na ushee
Huwa nazikumbuka kwa uchungu mkubwa zile siku anko wetu akiwa kalala mochwari sisi tukihangaika kupata milion 7 tuukomboe mwili wa mpendwa wetu!
Tangu hapo nimeendelea kusoma visa vya kusonenesha mno vya ndugu kuzuiliwa kuchukua miili ya ndugu zao mpaka walipe gharama za matibabu ambazo ni mamilion ya shilingi...! Sijawahi kusikia serikali ikisema chochote
Msanii Profesa J yu mgonjwa.. Tunamtakia nafuu ya haraka.. Kwenye maradhi yake fanilia imejitokeza na kuomba msaada..na wamesaidika haraka sana.. Ikiwemo serikali...!
Hospital aliyolazwa Proffesa J kuna mamia ya wagonjwa wenye uhitaji sawa ama zaidi ya J lakini hawana pa kupazia sauti zao zikasikika nao wakasaidika kama J
Tukiamua kwa utayari wetu tunaweza kutenga siku moja kila mwezi tukafanya harambee kubwa na kile kinachopatikana kikaenda kuwasaidia wenye maradhi ya gharama kubwa na wasio na uwezo wa kumudu gharama zake! Harambee hiyo ikiambatana na kuikumbusha serikali walau kubeba gharama za wale wanaokufa huku wakidaiwa mamilion ya shilingi na hawana uwezo wa kupata hata robo yake
Harambee hiyo iende sambamba na kampeni ya bima kwa wote kwa gharama himilivu, Na haya yote yafanyike kwa upendo, kwa kujitoa kwa uaminifu mkuu, hofu ya kimungu na huruma ya kweli.. Kwa kufanya hivyo tunaweza hata kuepuka laana nyingi hasa hii ya kuzuia mwili kwa ajili ya madeni ya gharama za matibabu.