RORYAKWETU
Member
- Nov 18, 2011
- 83
- 13
Mimi ni mhitimu wa elimu ya juu mwaka huu na katika tathmini yangu swala la kusubiria ajira inaweza kusababisha ndoto zangu zisitimie kwani napoteza muda kwani wakati mwingine najikuta nikitamani hata kufanya kazi ilimradi niweze kujikimu kitu ambacho kwa maisha ya sasa ni hatari sana.
Mimi nina uwezo wa kupata mtaji wa milioni tano tu fedha za kitanzania hivyo kwa sababu naamini kuwa hili ni jukwaa la biashara na ujasiriamali naomba michango yenu ya kimawazo kuhusiana na wazo la kuwa wakala wa kuuza vocha za jumla, luku na startimes. Napendelea biashara hii kwani si hatari kwangu mimi ambaye ndiyo naanza ukizingatia nina mtaji mdogo.
Lengo langu ni kuwa kupata kazi niipendayo mimi na si ya kuchaguliwa na ndugu au wazazi ndiyo maana nahitaji kujishughulisha ili kukuza kipato changu ili nijitegemea kwa kiasi kikubwa na kuwa katika nafasi nzuri ya kutimiza hili lengo langu.
Mimi naamini kuwa maisha bora yanawezekana kama vijana wengi watajengewa uwezo wa kujitegemea
Asanteni sana na mungu awabariki