Wazo la Kufungia Mwaka: Ukweli Tusioupenda Kutoka 2014

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Mwaka 2014 ndio unaelekea kututupa mkono na kubaki katika historia. Kuna mambo mengi kama taifa na kama Mtanzania mmoja mmoja tumeyaona katika mwaka huu; mambo ambayo mengine yameacha ladha chungu katika ndimi za fikra zetu. Ni mambo ambayo tumegundua au tumetambua kuwa yameendelea kuwa kweli na kwa namna fulani hatuoni ni vipi mambo hayo yatabadilika hasa katika mwaka huu mpya wa Uchaguzi Mkuu.

Mambo hayo ni ya kweli kwa kutokea kwake, falsafa yake au hata kujirudia kwake. Ni mambo ya ukweli ambayo hatuwezi kuupenda (unwanted truth). Kwa mfano:

1. Kuna watu - na kwa kuangalia kura za Serikali za Mitaa ni wengi - bado wana mapenzi ya dhati na chama tawala na wako tayari kusema, kufanya na kutenda lolote ili kiendelee kuwa madarakani. HILI NI KWELI.

2. Ufisadi umepewa kiti cha enzi; una watumishi wake na una watu ambao wanatoa sadaka zao kwenye madhabahu yake kwa mbinde na upinde. Bado hatujapata dawa ya ufisadi. HILI NI KWELI.

3. Siasa zetu bado ni za mambo ya watu (person-oriented) kulikuwa kuwa siasa za masuala (issue oriented). Bado tofauti zetu zimejikita katika watu zaidi kiasi kwamba unaweza ukaamini kubadilisha watu kunaweza kubadilisha mwelekeo wa taifa. Tumesahau kwa miaka zaidi ya hamsini tumekuwa tukibadili watu kwenye nafasi mbalimbali lakini bado tupo tupo tu. HILI NALO NI KWELI.

Sijui mwenzangu katika mwaka huu unaweza kusema ni mambo gani umeyaona kuwa ni ya kweli na kwa kweli kuyakubai kuwa ni kweli hupendi lakini inabidi uite kikombe kikombe na gudulia gudulia.

Heri ya Mwaka Mpya

Tujiandae kumkoma nyani giledi tena..... mchana kweupe...

MMM
 
Watanzania hawajali tena maovu wanayoyasikia maana wanaamini haiwasaidii.....mfano mtu na akili zake timamu anauliza "hivi hizo hela za escrow hata zikirudishwa mimi nitafaidikaje? si zitaishia kwenye seminar,kununua V8 na safari za mafunzo kwa wakubwa tu?
 
Mhimu mwakaa huu unaoanza tuanze na kubadili mfumo wa kiutawala badala ya kubadili watu.
 
Kila Mtu Mwenye uchungu wa Nchi achukue jukumu la kuelimisha ndugu zake kijiji ili waamke Na waache kuipigia kura CCM. Kura za vijijini ndio zinawaweka madarakani hawa wezi
 
Wazo na ukweli huu unatisha!
 
I agree tujikite kwenye issues oriented politics and not partisan then we can write CCM's political orbituary
 
Ni kweli usio pingika, wanao irudisha CCM madarakani ni watanzania wenzetu wa vijijini na si kosa lao ni la uelewa. CCM wanajua hilo fikana mtaji wao wote ni kuhakikisha hawaelewi, ili waendelee kuwa mtaji wao. Uchaguzi wa mitaa ulio isha umeijaruhi CCM na tusipo kuwa makini watakuwa kama mbogo aliye jaruhiwa, chochote mbele yake ni halali yake. Ni vema sisi tulio elemeika tutumie muda mfupi ulio salia kuwaelemisha hawa ndugu zetu wa vijijini ambao tayari wana "hints" lakini wanahitaji msisitizo. Tunaweza tumia wakati huu wa "CIVIC EDUCATION" kwa katiba mpya kufikisha ujumbe na ama kweli we neet to get organised na kuwafikia kila mwenye upeo kukabidhiwa kijiji ama kata.

NAWAHAKIKISHIA, TUKISHINDA KUIKATAA KATIBA, BASI TUTASHINDA UCHAGUZI UJAO KUWATOA CCM NA KINYUME CHAKE PIA NI SAHIHI KABISA
 
Mkuu, hapo kwenye bold hapo; Unayafahamu vizuri matokeo ya serikali za mitaa ya jiji la Dar Es salaam!?
 
Mhimu mwakaa huu unaoanza tuanze na kubadili mfumo wa kiutawala badala ya kubadili watu.

Kwenye mfumo tungefanikiwa sana kupitia katiba mpya, lakini kwa ule uchakachuaji uliofanywa na BMK....
Tunahitaji mapinduzi kama yale ya Burkina Faso
 
Kila Mtu Mwenye uchungu wa Nchi achukue jukumu la kuelimisha ndugu zake kijiji ili waamke Na waache kuipigia kura CCM. Kura za vijijini ndio zinawaweka madarakani hawa wezi

Tatizo siyo VIJIJINI kaka,tatizo tulioko mjini,tunadhani kwa kutoenda kupiga KURA ndiyo umesoma,vijijini akina mama wengi wanapiga KURA na kwenye upinzani wanawapigia upinzani,mfano halisi ni jimbo la Mbeya mjini.Kuna mpaka wa bibi wazee waliompigia Sugu kura.
 
Tumeendelea kubaki taifa ombaomba...bajeti yetu bado ni tegemezi...hakuna nia ya dhati ya kujitoa huko....HILI NI KWELI
 
Mimi ombi langu kwa serikali kwa mwaka ujao...waangalie uwezekano wa...kuundwa tume maalumu itakayo simamia mahari za mabinti ili na sisi walalahoi tupate wenza......ni hayo tu.........
 
Vyama vya upinzani vinatarajia kushiriki uchaguzi usio na tume huru ya uchaguzi. Tena unaoweza kulihusisha jeshi hili ni kweli
 
Back
Top Bottom