Wazo la Kuanzisha Tawi la Chadema hapa Uingereza...for a start | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo la Kuanzisha Tawi la Chadema hapa Uingereza...for a start

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mlalahoi, May 23, 2011.

 1. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Nimekuwa na wazo la kuanzisha tawi la Chadema hapa Uingereza,sio kwa vile CCM wana matawi yao nje ya nchi bali imani yangu kwamba Chadema as a formidable opposition party na ambacho kimeweka mbele maslahi ya nchi badala ya kisiasa kinapaswa kuungwa mkono ndani na nje ya Tanzania yetu.

  Kama unaafikiana na wazo hili basi naomba tuwasiliane kwa PM,tukusanye mawazo mbalimbali kwa minajili ya kuunda tawi lenye ufanisi as opposed to matawi ya CCM yanayofahamika zaidi kwa picha kwenye blogs kuliko ku-promote maslahi ya Watanzania (well,they can't kwa vile mtoto wa mchawi is likely to inherit characteristics za kichawi pia).

  Ni matarajio yangu kwamba tawi la UK litafungua njia ya uanzishwaji wa matawi mengine kwingineko.Dokta Slaa,Regia,Mnyika,Zitto na viongozi wengine wa Chadema ambao ni wana-JF mnaombwa kuchangia mawazo yenu kuhusu suala hili

  Mods,naomba usihamishe post hii,tafadhali.
   
 2. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Asanteni sana tuungeni mkono watu wa huku nyumbani. Mawazo ya kuisapoti Magamba ni ya Kijima
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Siungi mkono hoja, labda ungetueleza kwanza je vyama vya siasa hapo uingereza umeshawahi kuona matawi yao? jibu kama ni hapana ndio ujifunze wao wanawezaje kuendesha siasa zao bila porojo za matawi? hao wanaccm wanaofunguwa matawi huko hawafungui kwa sababu ya itikadi bali ni NGO zao za kuwatapeli kina JK.
   
 4. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naona ni vyema tu aanzishe! Ni wazo zuri tu!
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Watanzania achennei na mambo ya siasa huko nje anzisheni NGO za elimu, afya. na kijamii. Siasa ni chanzo cha matatizo mengi nchini mwetu lakini sulisiho la matatizo tuliyonayo si siasa......

  Msiige chama cha Magamba. We all need changes not matawi ya siasa. tena huko nje. Hata kama we ni nazi wa CDM anzisha smething italenga kwenye key problem ya Tanzania .

  Eg trough NGO ya elimu kwa watanzania mnaweza kukusanya computer/laptop used kwa ajili ya shule za sekondary. Through NGO mtapata ha asuprt kubwa zaidi na sio trough wing ya siasa.
   
 6. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mambo ya ngoswe mwachieni ngoswe, jamani mnapokuwa nje ya Tanzania muwe Watanzania sio wana CDM wala wana CCM tuondokane na huu utitiri wa umburukenge.
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Tupo pamoja Mkuu, tafadhalini Chadema kuna mambo yanayoweza kufanywa na Chama Cha Mafisadi tu kama CCM na myaogope kama ukoma ! Onyesheni utofauti wenu na vyama vya maslahi ya tumboni.
   
 8. Tankthinker

  Tankthinker Member

  #8
  May 24, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi nakuunga mkono kabisa, jambo la maana wewe binafsi jielimishe juu ya CDM na sera zake ili unapo anza kuwasiliana na wakazi wengine mlio nao huko uwe na uwezo wa kuwaelimisha. Ukisha fanikiwa kuwaelimisha na kupata watu walio tayari kuwa wana chama ndipo uushirikishe uongozi wa CDM uje kuhamasisha zaidi na kufungua tawi rasimi. Swala la kuanzisha tawi sio swala la kuuiga CCM, bali ni swala la kupanua ugo wa wan CDM kwani inapotokea kuwa kuna wana CDM wako nje ya nchi kuna ubaya gani kwa nia ya kuji mobilize wasianzishe tawi ili shughuli na mimkakati iwe rasimi?. Songa mbele mkuu.
   
 9. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hoja nyingi hapo juu hazijibu lengo la thread, kwa mfano kusema siasa ni chanzo cha matatizo ni sio suluhisho , hivi hizi tafiti zimefanyika lini?
  tawi la chama cha siasa ni tawi tu liwe nje ya nchi au ndani? kalengo
  ni yale yale mshikamano wa wanachama na kushauriana na
  hata kujuana sijaona tatizo lolote la hayo matawi
  hata kama kuna watu wanayatumia vibaya
  lakini sio lazima iwe hivyo , hata kuna
  upweke furani kwa wanaoishi/ kusoma
  nje ya nchi bila kujua au kuwa na maoni
  kujuu ya kinachoendela nchi mwao
  hii itakuwa furusa pekee lakini kama
  kuna tatizo jingine la haya matawi sawa ila
  kwa sasa naunga mkono
  as naongea kutoka ground zero
  hakuna raha kama kushiriki kujenga nchi yako bana
   
 10. e

  ebrah JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pamoja ndugu yangu!
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu ina maana mambo yote unayosema aukuandika hapa yamefanyiwa utafiti ? Ni elimu yangu na uelewa wangu tuunanifanya niandike na kusema ninanachona ni sahihii. So usipangue hoja yangu just because haina utafiti . Ninachosema ni observation na experince ya matatizo mengi tuliyonayo yamesababishw ana wanasiasa na siasa. Suluisho la matatizo yetu mengi linahitaji utashi wa wanasiasa kuwasikiliza naufanyia kazi mapendekz ya watendaji.......... Hapo unasemaje?????????

  Kama mm ningekuwa nje ya Tanzania japo nataka mabadiliko ya kisiasa siwezi kwenda au kujinga na jumuya yenye mtazamo wa kisiasa. Iwe ni CDM NCCR CUF. Ninachweza kuunga mkono na kushiriki kushirikiana na watanzania kuadvocate specific poblem fulani nchini. Ndo nimesema ELIMU, AFYA MIUNDOMBINU.

  Maendeleo ya kisiasa tuliyonayo Tanzania tunawazidi hata Kenya, Rwanda na Uganda lakini maendeleo ya Kielimu ,Afya, inaweza sisi ndo wa mwisho.... Sababu wewe unapenda tafit sina uweo wa kukutihibitishia lakini hali ndo hiyo...........

  BInafsi naona kwa watanzaia kufungua matawi ya siasa nje ni kukosa PRIORITISATON. Wataka mabadiliko walio nje wanaweza kufanya kitu nje ya siasa amabacho hata CCM hawawezi kufurahia. Kwa kufungua matawi ya siasa nje ya nchi Chama cha magamba watakuwa wanachekelea tu.

  Any way Goodluck . wakuu
   
 12. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu,mbona hata sioni tatizo na either side ya huu mjadala.
  Kwa upande mmoja naona wana-siasa, wanaotamani kuchangia ukombozi wa Taifa hili kupitia mlango wa siasa. Wanaamini kwamba pamoja na wanaharakati wengine walio nchini,wao nao wanaweza kuongeza chachu kutokana na position yao kwa kuwa nje ya nchi na hivyo kuwa na edge fulani. Which I find absolutely fine,given the potential I see merely on the virtue of mahali walipo.
  Kwa upande mwingine naona wanaharakati wengine wasio wanasiasa, ila wenye lengo lile lile la ukombozi na maendeleo ya Taifa. Hawa wanaamini katika asasi za afya,elimu n.k kama mlango wa kupitia. Again absolutely right!
  Ambacho sikubaliani nacho ni kule kuona kwamba kundi moja "limekosa prioritization" kuliko jingine. Hapo labda ufafanue mkuu. nadhani haya yote yanaweza kwenda pamoja,na yote yanapaswa kufanywa kama mtu yupo kwenye nafasi ya kufanya. Na lile wazo la kwamba ufumbuzi wa matatizo ya nchi yetu hii "si siasa", nina mashaka nalo sana!
   
 13. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Ninakuwa na maswali mengi yasiyo na majibu. WAKATI WA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI, WANANCHI HUWACHANGIA PESA WAGOMBEA WA CHADEMA ILI IWASAIDIE KUSONGA MBELE, LAKINI WANAO GOMBEA KWA TIKETI YA CCM, HUTOA PESA KWA WAPIGA KURA KAMA RUSHWA.

  Kwa kuanzisha tawi nje ya nchi, litasaidia kuwapa moyo viongozi wetu wa CDM kuwa wanaungwa mkono nje na ndani ya nchi na hivyo kurahisisha ukombozi. Naamini wale wanao unga mkono ccm ni wanafiki kwa kuwa hiki chama na viongozi wake wanaonekana kutokujua wanacho paswa kufanya ili kuinua maisha ya wakazi, matokeo yake wanatumia muda mwingi kuua wale wenye mawazo safi ya kusaidia jamii.

  TUKO BEGA KWA BEGA MKUU!
   
 14. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2011
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakuu mimi sioni mnachopingana hapa, wazo la watanzania wa nje wanaounga mkono mabadiliko either kwa kuanzisha matawi ya CDM au Kuanzisha NGOs za kussuport elimu, afya, mazingira etc etc. yote ni mazuri kwani yanaelenga kuleta unafuu wa maisha ya mtanzania masikini, tukubaliane kwamba tunahitaji kuonyesha kwa vitendo ni namna gani tutaleta mabadiliko, kwahiyo wazo la NGO linakuwa lina nguvu ya kiutendaji zaidi kuliko la tawi la chama, NGO inalazimika kufanya kitu kinachonekana kwa kwa jamii kuliko tawi la chama ambalo haliwajibiki kufanya kitu concrete.

  Lakni kwa upande wa pili wanachama wa chadema nje wanaweza kujimobilize na kufanya jambo linaloonekana pia, kwa mfano washabiki wa CDM wa UK walishawahi kumchangia mbunge wa Arusha Tractor kwa ajili ya maendeleo they can also do the same!

  Kwahiyo mimi naunga mkono hoja zote mbili hapa!

  Aluta continua!
   
 15. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema as a formidable opposition party na ambacho kimeweka mbele maslahi ya nchi badala ya kisiasa kinapaswa kuungwa mkono ndani na nje ya Tanzania yetu.

  Mtoa hoja naomba mchanganuo wa Aya hiyo hapo juu (tafadhali).
   
 16. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hili wazo sio uwongo nakupa assigment moja.
  Assuume tuko mwaka 2015 CDM Imechukua nchi. Wewe kama mtaalam unaulizwa upewe nafasi gani ya uongozi kwenye shirika au Wizara kutokana na utaalama wako .

  A:Je ni nafasi au cheo gani ungependa kupewa?
  B:muhimu ungefanya nini au maamui gani hasa kwenye nafasi yako tofauti amabcho kingeleta mabadiliko ???

  Nimeshawai kuuliza hili swali la kipendegele B kwenye mada hapa hapa wenye jukwaa la siasa ndo nikagundua kuwa watu wengi tunadhani siasa zitaondoa matatizo yetu.

  Mwanasiasa akisema atawezesha treni kutoka dar kwenda mwanza i tumie 12 hrs haina maana anajua HOW? Wht politician know ni WHAT we need but thye dont know HOW to achieve it . sasa kama hakuna watendaji naprofesional wa kukuna kuwezesha aukufaniisha hilo ndo inabaki siasa tu. nayo inakuwa part of the problem.

  Tumabiane na watu wajue ukweli la sivyo hata wakija CDM au CUF wananchi watashangaa kwa kuwa na unrealistic expectations.


  But kama nilivyosema Tuwatakie mafanikio wenye nia njema hii japo tunatofautina mtizamo lengo letu ni mabadiliko magamba yatoke

  Mkuu Nakubaliana na wewe na huundo ndo ulikuwa mtazamo wangu.Wing za chadema nje zingekuwa za KI -NGO ingependeza zaidi. Do something diff to CCM Magamba .
   
Loading...