Wazo la kuanzisha Tanzania Mechanical Engineers association (TME)

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Kila nikitazama mwenendo wa fani mbalimbali katika nchi yetu ninaona upo umuhimu mkubwa wa wataalamu kuanzisha umoja kwa wana taaluma mbalimbali kuweza kukaa pamoja kujadili changamoto na fursa zilizoko katika taaluma yao ili kwa umoja wao waungane kuleta maendeleo katika taaluma yao na Taifa kwa aujumla.

Kwa muktadha huo ninapenda kuwakaribisha MECHANICAL ENGINEERS WOTE WA TANZANIA tukae tuunde umoja wetu ambao tutakuwa tukikaa kujadili changamoto na fursa zinazoikabili taaluma yetu ya mechanical na kutoa mapendekezo kwa wahusika ili watutengenezee mazingira bora.

karibu ujiunge na TANZANIA MECHNICAL ENGINEERS (TME) face book group ili tuweze kuungana na kuunda umoja wenye kutetea fursa na kuondoa changamoto kwa mechanical engineers

inia facebook search hilo group na jiunge kwa bure kabisa hakuna kiingilio chochote
 
Ni bora ukasema changamoto zenu ili erb iwasaid

Ni bora ukasema changamoto zenu ili erb iwasaidie
ERB ni taasisi ya serikali ambayo kazi yake ni ku regulate conducts za wahandisi wote Tanzania, wahandisi tunahitaji chombo chetu wenyewe kinachotazama changamoto na fursa kutokea upande wa wahandisi wenyewe na kuwaambia serikali hapa mngetufanyia hivi au pale hivi taifa letu tungelifikisha mbali.
 
Nakubaliana na wewe 100%
 
Mechanical Engineering - hii kozi ukimaliza labda ukafanye kazi nje ya nchi - application yake kwetu hapa bado mno, wengi vijana wamekuwa ma-bankers huku ma - integration na differentiation equations kama haya yakipotelea kichwani.

1629367960818.png
 
Mkuu mimi wa kwanza nitakuunga mkono, maana tunapata changamoto nyingi sana, hasa sisi tuliojiajili
 
wazo jema sana......hii fani ni muhimu sana hasa huko ytunakoelekea.....tukutane facebook
 
Ni bora ukasema changamoto zenu ili erb iwasaidie.
Erb ni Kama taasisi ya CIVIL engineers. Haigusi changamoto za Mech. Uholela katika fani ya mech engineering ni wa kutisha. Yeyote anaweza kufanya chochote katika fani hii bila kuulizwa
 
na kibaya zaidi unakuta kazi zinazohitaji mechanical engineers zinaweza kufanywa na fani nyingine kwa kuwasimamia mafundi. Tunahitaji kulinda fani yetu kwa kazi za mechanical zisimamiwe na mechanical engineers
 
Kila nikitazama mwenendo wa fani mbalimbali katika nchi yetu ninaona upo umuhimu mkubwa wa wataalamu kuanzisha umoja kwa wana taaluma mbalimbali kuweza kukaa pamoja kujadili changamoto na fursa zilizoko katika taaluma yao ili kwa umoja wao waungane kuleta maendeleo katika taaluma yao na Taifa kwa aujumla.

Kwa muktadha huo ninapenda kuwakaribisha MECHANICAL ENGINEERS WOTE WA TANZANIA tukae tuunde umoja wetu ambao tutakuwa tukikaa kujadili changamoto na fursa zinazoikabili taaluma yetu ya mechanical na kutoa mapendekezo kwa wahusika ili watutengenezee mazingira bora.

karibu ujiunge na TANZANIA MECHNICAL ENGINEERS (TME) face book group ili tuweze kuungana na kuunda umoja wenye kutetea fursa na kuondoa changamoto kwa mechanical engineers

inia facebook search hilo group na jiunge kwa bure kabisa hakuna kiingilio chochote
Nawakaribisha face book kujiunga.

wataalamu tukae pamoja kujadili changamoto zetu na kuzitafutia ufumbuzi pamoja
 
Back
Top Bottom