Wazo la Jumapili: Ninatamani Prof Kabudi angekuwa na uthubutu na ujasiri kama wa Prof Assad dayosisi yetu ingepona!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,901
141,838
Mimi ni muumini wa Imani ya Kristo ninayeabudu katika Kanisa la Anglikana dayosisi ya Dsm kama mshirika wa kawaida.
Dayosisi yetu imepitia katika kipindi kigumu sana cha kufisadiwa mali za Kanisa tena na viongozi wetu wa kiroho huku wale wa kimwili wakikaa kimya. Hali hiyo ilisababisha vijana wachache walioishika Imani sawasawa waendeshe mapambano ya kukomboa mali za Kanisa kabla hazijamalizwa zote. Hatimaye walifanikiwa kumuondoa askofu Dr Mokiwa kitini lakini mali nyingi za Kanisa zikiwa zimeshauzwa kwa wapagani.

Miongoni mwa ufisadi mkubwa ukiwa ni mkataba wa Pango kati ya Kanisa na benki ya DCB pale magomeni, nyumba ya Kanisa iliyoko oysterbay, shamba la Kanisa kule buza na ardhi ya Kanisa pale Kurasini.

Kilichoniuma zaidi ni kutokea kwa ufisadi huu wakati Prof Kabudi akiwa kiongozi na mshauri mkuu wa askofu Dr Mokiwa. Alikuwa na nadhani mpaka sasa anayo nguvu ya kisheria na kikatiba kwa mujibu wa katiba ya Kanisa Anglikana jimbo la Tanzania, lakini hakufanya chochote mpaka leo kijiji cha anglikana pale buguruni kimemezwa chote na kanisa kubakiwa na eneo dogo sana.

Ninamkumbuka mzee Malecela jinsi alivyofanikishwa kurejeshwa eneo la Kanisa lililouzwa kifisadi na mchungaji pale Iringa mjini eneo ambalo sasa limejengwa Kanisa kuu na makao ya askofu wa dayosisi ya Ruaha.

Ndiposa nasema kama Prof Palamagamba Kabudi angekuwa jasiri kama Prof alhaj Assad basi ardhi ya Kanisa isingeuzwa kwa wapagani hata sm 1.

Jumapili njema
Maendeleo hayana Imani!
 
Hizo taarifa hata mie ninazo,nenda mbele hatua ingine usimsubiri Palamagamba
Ndio nikashauri na vijana wale wakafanya kama Prof alhaj Assad kutangaza " udhaifu " wa askofu kwa Kanisa zima. Hatimaye Dr Mokiwa akafyekelewa mbali na sasa tuna askofu mpya ambaye kuapishwa kwake kulihudhuriwa na mkuu wa nchi Rais Magufuli.

Ila Prof Kabudi angetimiza wajibu wake tusingefikia huko!
 
Sasa waviziaji na wambeya huwa wanatumia jitihada gani kupata habari zaidi ya kujipendekeza na kutega masikio yao marefu kama mbawa za bombadia?
........kama kukosa taarifa za kujiheshimu ukiwa kwenye dhamana ya mahakama...... Lazima kidebe kitakuhusu!
 
Back
Top Bottom