WAZO LA JUMAPILI: Consultant wa kutafutia mchumba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WAZO LA JUMAPILI: Consultant wa kutafutia mchumba!

Discussion in 'Love Connect' started by WomanOfSubstance, Jun 6, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kwenu mnaotafuta mke wa kuoa!

  Miaka ya nyuma, kijana hakuwa na kazi kubwa saaana kutafuta mchumba tena kwa vigezo avitakavyo mwenyewe.

  Kigezo cha uchapa kazi, usomi, hata mwonekano/wajihi ilikuwa rahisi sana kupata. Kama ni uchapa kazi basi jamii au hata familia ya karibu iliweza kuvalidate. Kuhusu ulimbwende ndio kabisaaa ilikuwa rahisi kuona. Mdada alikuwa na nywele za asili akisuka au kunyodwa kwa staili mbalimbali za kiasili na kupaka mafuta ya asili haswa ya nazi.

  Ngozi ilikuwa asili kabisa.Kama ni mweusi basi alikuwa mweusi. Mweupe alikuwa mweupe kweli.

  Siku hizi, tabia ni kitendawili kujua... sijui atakuambia nani.. labda kama ni jirani yako au mnasoma wote.... na mnakaa mji mmoja! Kama ni urembo, basi wa dukani ndio asilimia zaidi ya 70 mradi uchache uwepo tu.Ndio maana wanasema siku hizi kila mwanamke ni mrembo. Kuanzia nywele, mboni za macho, kope, kucha,matiti, makalio hadi kule nyetini ni artificial! Akina kaka mna kazi kubwa.

  Inabidi muweke ma consultants wa kuwasaidia kung'amua vigezo vipi ni vya kweli au asili na vipi vya kuungaunga!

  Lakini hata akina kaka nao hawajambo siku hizi. Mkorogo wanawazidi kina dada, wananyoa nyusi, wanafanyiwa waxing, wanajikwatua kuliko akina dada wakati mwingine. Mwanamke usipoangalia, mumeo atakuzidi kwa "urembo"....

  Dunia twenda wapi?
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Duh!
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mke bora hutoka kwa Mungu! sara na kuomba kukiambatana na kufunga ni suluhisho tosha, kuepuka hizi made in Republic of China!
   
 4. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Yalah! Hadi nyetini ati artificial! How is that possible?
   
 5. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,831
  Likes Received: 20,845
  Trophy Points: 280
  WOS,ningependa sana kuchangia topic yako,ila kuna maneno mawili yananichanganya,naomba unisaidie nini maana na/au tofauti ya MLIMBWENDE na MREMBO.
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  si hamtaki "used"..basi inakuwa re-packaged!
  Its all about kuwawekea wanawake standards which are way too high, mnataka warembo kupitiliza, mnataka asiye used wakati kila mumuonaye mnataka mumjaribu hata kama hamna nia naye, ilhali nyie vya kwenu ni vichache tena wakati mwingine hafifu sana au hakuna kabisa maana mdada akitaka kuweka standards hamkawii kusema kuwa ni changu......!
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kimsingi hayana tofauti kubwa sana - yote yana maana uzuri - beauty..si unajua hata kizungu kuna Beautiful, pretty, glamorous, gorgeous etc....
   
 8. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  ni kweli kabisa W.O.S.lakini mimi nimekupenda wewe naturaly,no consultancy needed hapo hao wengine nawaachia masanilo na fidel
   
 9. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  vipi mke wetu wa kuli-mbwani,nae ulipewa na mungu mkuu.
   
 10. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mada nzuri WoS..

  mie naona hata huyo consultant naye tutamtembezea pochi/tutamuhonga awadanganye!LOL:painkiller::target:
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sara na kazi ndugu yangu! Namtumainia bwana kwa kila jambo
   
 12. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Mkuu naomba nitofautiane na wewe kidogo

  HATA UFUNGE, UOMBE, BILA JUHUDI BINAFSI HUWEZI FANIKIWA KUMPATA MKE MWEMA, so ukijifungia kanisani au nyumbani ukiwa unaomba huyo mke atakufuata kanisani au nyumbani? pamoja na kuomba you need to go out jichangane from there ndo unaweza fanikiwa
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Jun 6, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  I'm sorry but this is gay as hell. Mwanaume gani huyo anayefanyiwa waxing na kunyoa nyusi? Hiyo waxing anafanyiwa sehemu gani ya mwilini? Kwapa? Kwenye makalio? Kifuani? WTF? Gay is as gay does....
   
 14. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #14
  Jun 6, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Unampataje sasa toka huko kwa MUNGU?hii ndio hoja yenyewe.Nitajuaje kwamba ametoka kwa MUNGU...
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Jun 6, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ooh yeah...fanya utafiti kuhusu vaginoplasty au vaginal rejuvenation na penile enlargement....

  Huko majuu siku hizi ukitaka kutoka na demu organic (kama wewe ni mwanaume) basi huna budi kuchagua ambaye siyo mzuri sana. Ukitoka na wale wanaowaita drop dead gorgeous basi kuna uwezekano mkubwa sana wa huyo dada kuwa feki.
   
 16. P

  PELE JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe kabisa, Mwanaume yeyote anayenyolewa nyusi na kufanyiwa waxing basi ni lazima ana kasoro fulani katika uanaume wake. Unyolewe nyusi na kufanyiwa waxing ili iweje? uwe na macho ya kurembuka na mwili laini kama mwanamke? si ajabu mwanaume kama huyu anaweza kula hata kungu manga ili macho yake yarembuke zaidi.
   
 17. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Labda ndio sababu siku hizi kabla ya kuoa wanaume huwaweka 'kinyumba' kwanza ili angalau waweze kubainisha organic out of artificials na baadae wafanye maamuzi ya kuoa au 'kutumia na kutupa'. Najua bado njia hii haisaidii sana kufanya maamuzi sahihi.
   
 18. P

  PELE JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wanaume wengi wameshaerevuka na hivyo kuweza kupambanua uzuri wa kuzaliwa na uzuri wa kununua, na wala hawahitaji consultants kuweza kutofautisha. Ni wachache mno ambao wanaweza kuuingia mkenge wa uzuri wa kununua.
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Umenichekesha sana..hapo kwenye bold....
   
 20. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hili nalo nenooo!!!
   
Loading...