Wazo la Biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza Juice | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo la Biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza Juice

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kingdom_man, Oct 12, 2012.

 1. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 560
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 60
  Habari Wadau.
  Nimekuwa nikifikiria hili wazo la kununua mashine ulaya za kutengeza Juice za pakti kama zile za Azam. Plan yangu ni kununua mashine za kutengeza na kuifazi Juice. Ingredients na Logo ya pakti za Juice zipo tayari wazo langu ni kuprint hizo pakti za Juice SouthAfrica then nazipaki mwenyewe.
  Kutokana Tanzania hapa tuna matunda ya kutosha kwahiyo ninadhamiria kutengeza QUALITY products na ku-supply kwa bei nzuri.

  Naombeni ushauri wa vitu gani vitavyohitajika kusajili kampuni ya kutengeza vinywaji/chakula na Wizara ya Afya na TBS wanaweza kuniwekea vikwazo gani kwa mjasiriamali mimi mchanga mwenye mtaji mdogo, ninayetaka kutoka kwa njia hii!. Tafadhali naombeni maoni au mawazo yenu kwenye hili swala.

  Natanguliza Shukrani.
   
 2. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,853
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  Cheap printing ya packets ni china.South Africa ni garama sana.Unatakiwa uwe registered na TDFA,TBS na uwe na leseni ya biashara na usajiriwe pia na Brela.Unatakiwa kuwa na formula yako ya juice ambayo inajumuisha (uzito wa kimiminika (viscosity) au Urojo wake,taste,colour,utamu(kiasi cha sukari etc.unaweza wasiliana na Chuo cha SUA wana ujuzi wote huo,pia utaitaji unga wa muhogo kwa wingi tu kwani juice zote packed unga huu utumika katika uzalishaji wa juice.
   
 3. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,156
  Likes Received: 1,683
  Trophy Points: 280
  Mpaka yatimie yote hapo nina uhakika 500% atapoteza pesa nyingi sana.....alaf bado hajaanza uzalishaji na kuuza....faida itakua ya kubahatisha sana coz ujue fika competition ni kubwa sana nnje huko watu wanataka vitu quality !! Kwanini watu wanunue kwako wasinunue kwa wengine ?? Hilo swali ukiweza kulijibu vizuri na gharama zako za uzalishaji zikawa ndogo....hapo faida utaiona !! Pia hiyo juice utaiuza sh. ngapi ?? Bei ina uwiano na quality unayo offer, ukizingatia competition ?? Una gurantee na supply ya hayo matunda ?? Kiwanda chako kitakua na hot or cold fill process ?? Kuna umuhimu wa kiwanda chako kiwe na human clinical studies/research/report ni jinsi gani hiyo bidhaa ita play role kwenye maisha na afya za wanadamu. Bidhaa yako iwe na good ORAC scores (Oxygen Radical Absorbance Capacity). The higher tha orac scores the better is the product. Binafsi hiyo biashara bado. Unahitaji uwe umejipanga sana, kama uko fit we endelea mkuu...Position yourself to earn the maximum profits possible (Profit mode). Risk ni lazima kwa kila mjasiriamali lakini wakati mwingine inabidi utulize ubongo ufikirie kwa makini sana !! Nimependa fact kwamba unapenda ujasiriamali....ni kitu kizuri sana. Tumia mtaji wako kwa busara sana..sikukatishi tamaa mkuu ila kwa ushauri wangu fikiria kitu kingine !!!
   
 4. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila mimi nakushauri pia ujaribu kufikiria suala la biashara ambayo ni ON GOING BUSINESS kuliko hiyo NEW BUSINESS kwakua unamtaji mdogo.

  Ila kama ni Enterprener wa kisawasawa (ability to risk) ,Kwa kawaida faida huja baada ya long run not a short run (remember Fixed cost and variable cost analysis) .utaweza kufanikiwa kama Utaanza kufanya tafiti ya kina na kutengeneza business plan ya kitaalamu na Pia ku scan mazingira yote ya hiyo biashara (SWOT analysis ya hiyo Industry)
  Mengine ni umakini kwenye
  1. Cost analysis or cost benefit ratio (Utatumia makisio/makadirio yenye sura ya uhalisia kidogo)
  2. Competitors analysis (Mkt share, Sales volumes,Profitability,Strategies,Mahitajiyasoko, target customer,segmentation)
  4. Marketing tools (Product development,pricing analysis,Promotion &Advert strategies, Distribution network)4P's
   
 5. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,570
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Kiongozi fuata ushauri wa Chipukizi! Unaweza pia kupata ushauri kutoka SIDO iliyo karibu nawe.
   
 6. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2012
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 560
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 60
  ASANTENI SANA WADAU WOTE KWA KUTOA USHAURI WENU WA KITAALAMU. NAUZINGATIA USHAURI WENU
  Asante sana kwa mwongozo Chipukizi, Senior Manager, Fyong'oxi, Sometimes
  Blessings.
   
Loading...